10 November 2009

THE MIRIAM.... "MIRIAM MAKEBA"



Wadau kama tunavyojua leo ni siku ya MIRIAM MAKEBA, leo ametimiza mwaka mmoja kamili tangu afariki dunia, na kwa kumuenzi mama yetu ninawaletea historia ya maisha yake ili kwa pamoja tuweze kumfahamu tangu alipoanza hadi kufanikiwa sana katika maisha yake. Karibuni.

Miriam Makeba ni mwanamuziki mashuhuri sana na mwanaharakati kutoka Afrika kusini. Alizaliwa 04-03-1932 Johannesburg. Baba yake Caswell Mpambane Makeba alikuwa ni kabila la xhosa na Mama yake Christina Nomkomendelo Jele alikuwa ni mswazi.Miriam ni mtoto wa sita na wa mwisho kwa mama yake, na wa kwanza na wa mwisho kwa baba yake. Mama yake aliolewa na Makeba baada ya ndoa yake ya kwanza na bwana Mahlangu kuvunjika wakiwa tayari na watoto watano ambao ni, Joseph, Hilda, Mizpah, Ethel na mmoja aliyefariki akiwa mchanga.Familia yao ilikuwa ni masikini sana. Baba yake ambaye alikuwa ni mwalimu kitaaluma hakuwa na kazi yoyote, kwani katika kipindi hicho cha utawala wa kikaburu ilikuwa ni ngumu sana kwa mwalimu mwafrika kupata shule ya kufundisha. Mama yake alikuwa anafanya kazi za ndani kwa wazungu na wakati mwingine kuuza pombe ya kienyeji(umqombothi) ili kuihudumia familia. Wakati huo ilikuwa ni kinyume cha sheria kwa mwafrika kunywa au kutengeneza pombe ya aina yoyote ile lakini hata hivyo ilikuwa ikitengenezwa na kunywewa kwa kificho. Kutokana na hali hiyo polisi wa kizungu walikuwa wakivamia mara kwa mara makazi ya waafrika ili kuwakamata wasiotii amri hiyo ya kunywa na kutengeneza pombe. Ilikuwa ni pale Miriam alipofikisha umri wa siku 18 tu tangu azaliwe, polisi walivamia maeneo ya waafrika na kufanikiwa kumkamata mama Miriam akiuza pombe, bila huruma wala kujali kwamba ana mtoto mchanga walimbeba hadi mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela. Hakuwa na jinsi ya kumuacha Miriam, alimbeba Miriamu wake na kwa pamoja kukaa jela kwa miezi sita. Hivyo basi Miriam akiwa katika umri mdogo kabisa aliweza kuionja jela.Walipotoka Jela walikuta baba (Makeba) amepata kazi katika kituo cha kuuza mafuta cha Shell, hivyo maisha yao yakawa na nafuu. Maisha yaliendelea vizuri hadi mwaka 1938 ambapo Mzee Makeba alifariki dunia, Miriam akiwa na umri wa miaka 6. Taabu ikarudi palepale, na kwa vile kipato cha mama yao hakikuweza kutimiza mahitaji ya watoto wote sita, ikabidi ahamishie watoto wake kijijini kwa bibi yao aliyeitwa MaVilakazi, (huyu ni mama mzazi wa mama yake na Miriam). Na yeye akabaki mjini kwa ajili ya kazi. Miriam anasema kuanzia hapo ilikuwa si rahisi kuonana na mama yake, muda mwingi alikuwa kazini mjini na kwa vile Miriam alikuwa bado ni mdogo na anayehitaji uwepo wa mama yake zaidi, ilibidi awe anafunga safari ya mjini kila mwisho wa juma baada ya masomo kwenda kumuona mama yake aliyekuwa akikaa kwa wazungu aliokuwa akiwafanyia kazi.Upande wa pili kwa bibi MaVilakazi, familia ilikuwa ni kubwa ya wajukuu 21,(watoto wengine ni wa kaka na dada za mama yake na Miriam). na yenye kipato kidogo, siku nyingine walikula na siku nyingine walilala njaa, lakini maisha yalikuwa yakienda. Miriam anasema kwamba pamoja na hali ile duni pale kwa bibi yake, bibi yake hakuwa na mzaha kabisa na kanisani, kila jumapili ni lazima kwenda kusali utake usitake. Miriam hakupenda sana kutokana na vile bibi yao alivyokuwa akitunza hela na vitu vingi vizuri kwa ajili ya kutoa sadaka wakati nyumbani wanalala na njaa. Wakati mwingine Padri wao aliwapita njiani wakati wa mvua wakinyeshewa bila kutoa hata lifti kwa gari ambalo limenunuliwa kwa sadaka zao. Miriam anasema kitu kimoja kilichomfanya asiache kwenda kanisani kilikuwa ni uimbaji tu, alipenda sana kuimba, na kanisani waliimba sana. Baada ya miaka kupita, mama yake alianza kuchoka na kuugua ugua, lakini alishindwa kuacha kazi kwa vile alikuwa akimsomesha Miriam ambaye ndio alikuwa ameanza chuo, Miriam naye alikuwa amechoka na maisha duni waliyokuwa wakiishi, maisha ya kuvaa 'kauka nikuvae' hali hii pamoja na kuona mama yake akiugua kila mara ikamfanya kufikia uamuzi wa kuacha shule na kutafuta kazi. Alipata kazi yake ya kwanza ya kuangalia mtoto katika familia ya kigiriki, alihamia pale na ulipofika mwisho wa mwezi wa kwanza alilipwa mshahara wake vizuri, mwezi uliofuatia akaambiwa asubiri kidogo kwa vile mwajiri wake alikuwa na matatizo kidogo, mwezi wa tatu mke wa mwajiri wake akamsingizia ameiba vitu ndani kwa hiyo hakuna mshahara. Miriam akaona huu ni uendawazimu, akaamua kuacha kazi. Akapata kazi nyingine kwa wazungu hii nayo ni ya kuangalia mtoto, anasema mambo yalienda vizuri hadi siku moja wakati wa likizo ambapo walisafiri, wakiwa huko wakafikia hoteli ya ufukweni. Hivyo wakati wa jua wao walikuwa wakijianika mchangani na Miriam akapewa kazi ya kukusanya shells kwa ajili ya kazi za sanaa za yule mzungu alizokuwa akizifanya. Siku ya kuondoka ilipofika bila sababu maalumu Miriam akaambiwa apande treni arudi, na wao wakarudi na gari walilojia. Katika ukusanyaji wake zile sheli aliweza kujaza ndoo mbili, hizi nazo aliambiwa arudi nazo kwa treni. Kwa hiyo yeye, mabegi yake na ndoo mbili zilizojaa shells tena katika daraja la tatu la treni!! hakuwa na la kufanya akapanda na kuanza safari ya kurudi, wakiwa njiani wakaambiwa inabidi wabadili treni wakatelemka na kusubiri nyingine. Ilipokuja akaanza kupandisha begi lake la nguo, akachukua ndoo ya kwanza ya shells, alipotaka kuchukua ya pili treni ikaanza kuondoka, haraka haraka akarukia ndani ya treni bila ndoo ya pili. Akaitizama ile ndoo iliyobakia akasema 'katu siiachi hii treni kwa ajili ya hiyo ndoo ya shells, sina hela nyingine ya nauli na hii treni ikiniacha ndiyo itakuwa mbaya zaidi'. Treni ikazidi kukaza mwendo na yeye akazidi kuitizama ile ndoo inavyobakia. Kufika Johannesburg alikuwa akitetemeka kwa hofu, alijiuliza atamwambia nini mwajiri wake kuhusu ndoo ya pili? baada ya kufikiri akaamua hatorudi tena kazini, hivyo akaachana na kazi ile nakuamua kurudi nyumbani.Huku nyumbani hali ya mama yake ilizidi kuwa mbaya, miguu yake ilianza kuvimba hadi kushindwa kutembea, walimpeleka karibu kila hospitali bila mafanikio. Hivyo wakaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji 'isangoma', kule wakaambiwa kwamba kuumwa kwake si bure, mizimu ya kwao imemchagua awe mganga wa kienyeji 'isangoma' ili aweze kuwasiliana nao moja kwa moja na kuwaeleza watu mambo yaliyopita, kutabiri yajayo na pia kutibu wengine. Na kama anataka kupona maradhi yanayomsumbua ni lazima akubaliane na hilo, wote walifurahi na kukubali kwani wanasema kuchaguliwa na mizimu ilikuwa ni kama zawadi. Baada ya kukubali alitakiwa kufuata mchakato wa Ukutwasa. Ukutwasa ni mchakato au hatua za kumfanya mtu kupokea nguvu za mizimu hadi kuweza kuponya wengine (Mganga). Aliondoka na kwenda Swaziland ambako ukutwasa wake ulikuwa unafanyikia. Kutokuwepo kwa mama yake nyumbani kulimfanya yeye kuchukua majukumu ya mama yake, kama kuilisha na kuiangalia familia kwa ujumla. Kwa jukumu hili ilibidi atafute kazi tena na safari hii akaamua kuwa dobi. Wakati huo kulikuwa na wafanyakazi wengi wageni waliokuwa wakifanya kazi nchini, na hao ndio walikuwa wateja wake, kila jumatatu alikwenda kukusanya nguo zao chafu na ijumaa kuwarudishia safi. Haya ndiyo yakawa maisha ya Miriam.Tangu akiwa shule hadi kipindi hiki anachofanya kazi za udobi, Miriam alikuwa na mpenzi wake chotara aliyeitwa James Kubayi au Gooli kama alivyojulikana kwa marafiki zake. Urafiki wao ulikuwa mzuri sana na kila mara walikuwa wote, Gooli alikuwa pamoja naye alipoacha shule, alipopata kazi kwa wazungu na hata sasa wakati mama yake alipokuwa Swaziland. Miriam alimpenda na kumuamini sana kiasi kwamba haukupita muda akapata ujauzito, hapo akiwa na umri wa miaka 17 tu. Anasema alikuwa na bahati sana kwani Gooli hakumtelekeza, alimchukua kumuhamishia nyumbani kwao. Familia ya kina Gooli ilikuwa inajiweza kidogo, mama yake alikuwa akipika pombe kama biashara ya ziada. Akiwa katika familia ya wakwe na mimba mambo yalikuwa magumu kidogo kwani Gooli hakuwepo muda mwingi alikuwa anachukua mafunzo ya upolisi katika mji mwingine hivyo alikuja pale kusalimia tu. Muda wa kujifungua ulipofika alipelekwa hospitali na kujifungua mtoto wa kike aliyemwita Sibongile au kwa kifupi Bongi. Alipotoka hospitali maisha hayakuwa rahisi tena, kazi zote za pale kwa mkwewe alitakiwa azifanye yeye, alikuwa akiamka saa 10 alfajiri kumuosha na kumlisha Bongi, kupika chakula cha wengine na kufanya shughuli zote za ndani na bado Bongi akilala alibaki kuhudumia wateja wa pombe hadi usiku wa manane.Gooli alimaliza mafunzo yake na kurudi nyumbani, lakini alikuwa amebadilika sana tabia, alikuwa mkorofi na mwenye wivu wa kupindukia, alianza tabia ya kumpiga Miriam bila sababu za msingi, Miriam hakuwa na haki ya kusema lolote kwa Gooli, Miriam alianza kusononeka lakini alivumilia, alijua Gooli hampendi tena lakini hakujua ni kwa kiasi gani hadi siku moja alipomfumania na ndugu yake. Miriam alijua amemfumania mumewe kwa hiyo hapo ana nguvu ya kusema lakini badala yake kibano kilimgeukia yeye na kupigwa kipigo cha kifo. Kuanzia hapo alisema imetosha, alimchukua mtoto wake akakodi taksi na kurudi nyumbani kwao bila kuaga. Gooli alimfuata kumrudisha lakini alikuta mama yake amesharudi toka Swazilandi, alimkurupua vibaya sana na toka siku hiyo hakurudi tena na ndiyo ukawa mwisho wa Miriamu na baba mtoto wake kuonana.Miriam sasa akiishi kwa mama yake, hakuwa na kazi yoyote ya kipato zaidi ya kumsaidia mama yake shughuli za Usangoma. Mama yake akaona hali hii haitamfikisha mahali popote mwanae, akamwambia ni lazima abadilishe kabisa mwelekeo wa maisha yake kwa kutafuta kitu cha kufanya. Miriam akaona ni bora aende mjini akaangalie cha kufanya, akamuacha Bongi na mama yake yeye akaenda mjini Johannesburg.Johannesburg alifikia kwa binamu yake aliyeitwa Sonti Ngwenya, Sonti alikuwa na mwanaye wa kiume aliyeitwa Zweli ambaye walikuwa karibu rika moja na Miriam. Zweli na baadhi ya marafiki zake walikuwa wameanzisha bendi ya muziki iliyoitwa Cuban Brothers, wote walijua Miriam anaweza kuimba hivyo siku moja wakamuomba kama atataka kujiunga na bendi yao, Miriam akaona hii itakuwa ni kichekesho lakini akakubali kwa vile alikuwa tayari kufanya jambo jipya katika maisha yake. Akiwa Cuban Brothers walifanya maonyesho sehemu mbalimbali kama makanisani, kwenye sherehe za kuchangisha fedha (fundraising) na sehemu nyingine nyingi. Katika kipindi hicho kulikuwa na ukumbi maarufu sana uliojulikana kama Donaldson Community Centre ambao Cuban Brothers mara nyingi walikuwa wakipiga muziki hapo, huu ni ukumbi ambao watu wengi maarufu na wasio maarufu walipenda kwenda. Siku moja wakiwa katika onyesho Miriam alinong'onezwa na mwenziye kwamba Manhattan brothers wako ndani ya nyumba. Manhattan Brothers band kilikuwa ni kikundi cha muziki kinachojulikana sana wakati huo, kila mtu alipenda muziki wake. Baada ya onyesho Miriam alifuatwa na kijana mmoja na kujitambulisha kwa jina la Nathan Mdledle na kuwa ni kiongozi wa kundi la Manhattan Brothers, Miriam hakuamini macho yake kwamba anaongea na Manhattan brother, wakati akishangaa Nathan akamwambia anapenda jinsi anavyoimba, kama hiyo haikutosha, Miriam anasema almanusura aanguke baada ya kuambiwa anaonaje kama anataka kufanya usaili wa kujiunga na Manhattan brothers. Alikwenda kufanya usaili na kushinda hivyo akapata kazi.



Pichani Miriam na kundi la Manhattan brothers.

Akiwa na Manhattan brothers aliweza kujulikana sana, hii ni kwa sababu kundi hili lilikuwa na kazi nyingi za ndani na nje ya nchi. Anasema Manhattan ilimfungulia milango yake ya mafanikio kwani baada ya kuwa nao makundi mengine mengi yalianza kumfuata ili afanye nao kazi yeye binafsi kama Miriam. Mwaka 1958 alipata bahati nyingine ya kuombwa kujiunga na kikundi cha African Jazz and variety. Hiki kilikuwa ni kikundi kinachozunguka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mwanzilishi wake alikuwa ni mama wa kiyahudi aliyeitwa Sara Silvia. Mama huyu alisema kuwa atahakikisha African Jazz and variet, inakuwa ni kikundi cha kwanza ambacho waafrika wataruhusikwa kupiga muziki mbele ya wazungu. Na kweli ndivyo ilivyokuwa, kikundi hiki kilikuwa kikifanya onyesho kwa wazungu watupu kila Alhamisi katika ukumbi wa Johannesburg city. Mwaka 1959 akiwa bado na African Jazz, alipata bahati nyingine kubwa ambayo tunaweza kusema ndiyo iliyo mtoa. Mtengeneza filamu mmoja kutoka Marekani aliyeitwa Lionel Rogosin, alimuona Miriam akiimba kwenye shoo za African jazz, alipenda sana uimbaji wake na akamuomba aimbe katika filamu aliyokuwa akiitengeneza COME BACK AFRICA. Miriam alikubali na akaigiza na kuimba katika filamu ile. Baada ya hapo Lionel Rogosin aliondoka na kuwaahidi kuwataarifu atakapomaliza kuitayarisha filamu ile. Huku nyuma mwaka huo huo 1959 februari, bahati nyingine ikaja kwa Miriam, King Kong Jazz Opera ilifunguliwa na Miriam akapata nafasi ya kuimba na kuigiza mle kama Joyce "Queen of Back of the Moon".






Wadau historia hii itaendelea wiki ijayo.

28 October 2009

Swali la wiki hii..

Wadau, leo nina Swali linalonitatiza kidogo naomba kuuliza, Ni kwanini Watanzania hatuna utaratibu wa kujifunza lugha za makabila mengine isipokuwa ya kabila yako? Leo karibu kila mtu akiulizwa ataje lugha anazoziongea atataja za kimataifa tu na moja ya kabila lake. Hivi ingependezaje leo Da'Mija nikiulizwa naongea lugha ngapi najibu, naongea saba vizuri ambazo ni Kisukuma, kingoni, kikerewe, kimakonde, kijita n.k na zingine hizi na hizi sio vizuri sana.

Wadau ni swali tu ambalo limenijia kutokana na kaka yangu Matondo Nzuzulima kuniuliza kama bado nakumbuka Kisukuma. Mnasemaje hapo?

***Mwanamke wa shoka - umeziona nyimbo za Kisukuma katika kibaraza changu? Unakumbuka lakini Kisukuma japo kidogo? Nategemea kwamba angalau wimbo wa kwanza utauelewa kwani ni maarufu sana katika harusi. Gonga hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/10/nyimbo-za-kisukuma-hizi-hapa.html

23 October 2009

Hapo Vipi?

Sio kwamba zinauzwa, ni watu wamepaki na kuelekea makazini. Holland kuna baskeli jamani ni balaa, ukitaka watu wakushangae sema hujui kuendesha baiskeli.

Picha nimeipiga wiki mbili zilizopita.



22 October 2009

Zawadi kwa Da' Yasinta na Da'Subi....BONGI MAKEBA.

Da'Yasinta na Da'Subi Kwa heshima na taadhima nawatunuku ZAWADI HII YA BONGI MAKEBA LIVE SHOW enzi za uhai wake. Bongi alifariki mwaka 1985 kutokana na matatizo wakati wa kujifungua mtoto wake wa nne.

21 October 2009

Nani huyu??

Wadau wapenzi huyu nani?

17 October 2009

Harry Belafonte Na Miriam Makeba - "Malaika"

16 October 2009

Patrice Lumumba.



Lumumba alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kweli katika Afrika yetu, hebu angalia hii video uone yaliyomkuta baada ya kukamatwa na Jeshi la Mobutu. Inasemekana hadi leo hii haijulikani mwili wake ulipopelekwa. Kama kuna mdau yeyote mwenye habari zaidi karibu ukumbini utujuze kwa kina.

08 October 2009

Rogers "The Tiger" Mtagwa ndani ya PAY PER VIEW pekee Oktoba




Hali ya uchumi iliulazimisha mwaka huu kuwa na mapambano machache saana ya kulipia (Pay Per View) na katika mwezi huu, kutakuwa na pambano moja tu ambalo katika pambano kuu (main event), anasimama nyota wa ndondi toka Tanzania Rogers "The Tiger" Mtagwa.
Roger mwenye rekodi ya (26-12-2) na anayeshikilia nafasi ya 9 ya ubora wa ndondi kwa uzito wake katika orodha inayotambuliwa na Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) atapambana na Juan Manuel Lopez (49-4-1) wa Caguas, Puerto Rico katika kuwania mkanda wa Lopez katika uzito wa WBO junior featherweight. Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa WaMu Theatre uliopo eneo maarufu la Madison Square Garden jijini New York.
Hii ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa Mtagwa ambaye ameonesha ujasiri na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa ndondi kwa kutwaa ubingwa wa NABF na USBA katika uzito wa Feather na pia kwa kuonekana kuboreka kila ajapo ulingoni kiasi cha kuwafanya wengi kuliona pambano lake la mwaka jana dhidi ya Thomas Villa kama PAMBANO LA MWAKA 2008. Katika pambano hilo lililopiganwa Tucson Arizona, Mtagwa alishinda kwa KO ya raundi ya 10.
Tazama / attach http://www.youtube.com/watch?v=-sPXABfEvW0
Tujiunge kwa pamoja kumshangilia (kwa watakaoweza) na kumuombea Mtanzania mwenzetu anayefanya vema sasa katika ulimwengu wa ndondi aweze kufanikiwa.
Kuwa kwenye pambano pekee la pay per view kwa mwezi huu ni kuonesha thamani yake kwani wapo mabondia wengi wenye majina ambao wameshindwa kuweka mapambano yao kwenye hadhi hiyo.
Kumbuka kuwa nyota kama Yuriorkis Gamboa toka Cuba atapigana katika pambano la utangulizi usiku huo dhidi ya Whyber Garcia katika kuwania umiliki wa mkanda wa WBA "regular" featherweight title unaoshikiliwa na Gamboa kwa sasa. Nyota wengine waliopata kushikilia mikanda ya dunia ambao watapigana kwenye mapambano yasiyo ya kulipia ni pamoja na Jermaine Taylor vs Arthur Abraham watakaochuana Oct 17.
Tunamtakia Rogers Mtagwa pambano jema

JIPATIE TOVUTI BURE KABISA.

Kuzingatia umuhimu wa kuwa na tovuti, na ya kwamba ni gharama sana hapa TZ
kupata tovuti, na tena watu wanafanya biashara rasmi kwa barua pepe za
bure kama yahuu na giimeili, hii yote inaonesha ukosefu au gharama kubwa
ya kupata tovuti.
Sisi tumedhamiria kubadili uelekeo mzima wa upepo, na tumepata wasamaria
wema na sasa rasmi tumefanikiwa kuleta ufumbuzi na neema kwa waTZ kwa
suala la tovuti na anuani rasmi za barua pepe.
Na sasa kwa awamu ya kwanza kwa kuanzia tu, WATU 100 WATATENGENEZEWA
TOVUTI BURE. Watu 100 kwa maana ya mtu binafsi, kampuni, biashara,
shirika, asasi zisizochukua faida (NGO), kikundi, duka, mjasiriamali,
saluni, shule ama Saccos n.k. BASI KILA ALIYEDHAMIRIA KUWA NA
WEBSITE/TOVUTI ajiunge na utaratibu huu wetu atengenezewe TOVUTI MOJA BURE
KABISA.
TOVUTI HII YA BURE itamfanya mhusika aweze kupata anuani rasmi za barua
pepe, yaani kama yeye ni Mwanahawa wa Vinyago Suppliers anatengenezewa
anuani zake za barua pepe mfano mwanahawa@vinyagosuppliers.co.tz n.k
kadiri ya atakavyo, nyingi apendavyo. Ataimiliki tovuti na kuiendesha
yeye.
Kumbuka kwa awamu hii ya kwanza TUNATOA BURE TOVUTI 100 TU kisha awamu ya
pili tutatangaza tena. Hebu fikiria kwa mkupuo tukipata tovuti 100 kwa
maana ya kwamba tunakuwa na kurasa mia moja zinazoelezea
watu/kampuni/vikundi mbalimbali na shughuli zao hapa Tanzania, hii ni
hatua kubwa sana na inaongeza maingizo ya utafutaji wa vitu toka Tanzania
katika search engines na tunasogea mbele taratiibu.
Hakuna vigezo vya kupata huduma hii ya bure, na tutahudumia kwa mujibu wa
FIFO (first in first serve/out) wa kwanza kuja, wakwanza
kutoka/kuhudumiwa. Maelezo na ufafanuzi zaidi tafadhali tembelea
http://www.tovutiyangu.com ujisomee huduma hii kwa undani. Zipo pia huduma
na bidhaa mbalimbali kwa walio na tovuti tayari.

Ahsante sana.
Admin,
tovutibure (at) tovutiyangu.com
http://www.tovutiyangu.com

03 October 2009

Hamisi Kitambi Mwanamuziki aliyesahauliwa..



Wadau ujumbe muhimu kutoka kwa MSEMAKWELI.

Baada ya kupata ajali amesauliwa! hakuna huduma ya matibabu! wadau tumsaidie Mwanamziki huyu!

Hamisi Kitambi ni mmojawapo wa wanamziki wakongwe na hadhina waliobakia hapa nchini Tanzania, bwana Hamisi Kitambi mtunzi wa nyimbo nyingi mojawapo ya nyimbo zake ni ule wimbo mzuri maarufu kwa jina "Mpenzi wangu mwenye rangi ya Chungwa" kwa wale wenye kumbukumbu wanajua radha ya utamu wa wimbo huo..
veteran huyu Hamisi Kitambi amefanya kazi na bendi nyingi zikiwamo Tabora jazz, Unyanyembe band, penginepo KIKO KIDS,labda Dar-es-salam Jazz,labda Western Jazz, lakini hadi anapata hajali ya gari alikuwa Juwata (OTTU) Jazz sasa Msondo Ngoma aka Baba ya Muziki, Mwanamziki huyu mkongwe Hamisi Kitambi amepata ajali akiwa katika gari yeye na wanamziki wenzie wa Msondo Ngoma walipokuwa safarini Tanga. Mzee Hamisi Kitambi kama anavyoonekana pichani miguu imevunja na amewekewa vyuma. Kitu cha kusikitisha ni kuwa tangu apate hajali ndio katupwa hana uduma muhimu, na kama tunavyojua mtaji wa masikini ni MIGUU YAKE nayo ndio kama anavyoonekana, Je ni haki kwa mwanamuziki au mwanadamu aliyechangia kujenga msingi wa fani ya muziki nchini kutupwa kama hivi?
Basi hata kama hakuna bima ya kulipwa,hata ubinadamu usiwepo?
Tujaribu kumsaidia mzee wetu huyu mwanamziki mkongwe Hamisi Kitambi anapatikana kwa simu hii Dar 0713576475

25 September 2009

ADHABU..



Watoto hawa wamechelewa shule na adhabu yake ndiyo hii, Wadau vipi hapo?

Picha kwa hisani ya Mzee BARAKA CHIBIRITI.

29 July 2009

OBAMA NAACP SPEECH.. ''Your Destiny Is In Your Hands, no excuses, no, no, no...

23 July 2009

Hakuna kupumzika na The Ngoma Africa Band.



The Ngoma Africa Band aka FFU! Kukiwasha cha moto kingine ndani ya
AFRILU Festival, Ludwigshafen City,Germany siku ya Ijumaa 24.7.

Kamanda Ras Makunja atakiongoza kikosi cha The Ngoma Africa Band aka FFU katika jukwaa lingine la onyesho la AFRILU .Onyesho hilo litakalo fanyika siku ya ijumaa 24.07.2009 jioni katika uwanja wa Ebert Park,mjini Ludwigshafen,huko Ujerumani,ambako washabiki wengi wanasubiri kucheza gwaride na ffu wa Ngoma Africa band.habari za uhakika zinatonya kuwa Karandinga la FFU hao linapiga misele na kwenda kwa kasi kuelekea katika maonyesho hayo!
ambapo washabiki watapata burudani ya aina yake.
Usikose kupata mziki hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kuwasiliana na ffu at http://uk.mc240.mail.yahoo.com/mc/compose?to=ngoma4u@gmail.com

16 July 2009

Nchi za kiafrika ni ngumu kujua nani ni tajiri ...

Nchi za kiafrika ni ngumu kujua nani ni tajiri kwa sababu zifuatazo
1. Watu wanakwepa kodi hivyo serikali ni ngumu kujua pato halisi la kila mwananchi
2. Kukithiri kwa rushwa hivyo kufanya pesa nyingi kufichwa

Kwa Misingi hiyo basi, Serikali inawajua Matajiri wasafi tu na wenye kulipa kodi na hali halisi ya uchumi ni kwamba haiwezekani kuwakadiria kwa hakika,

Katika Tanzania, Tajiri hatajulikana mpaka matatizo hayo yatakapotatuliwa


Jana niliomba msaada wa swali lililokuwa likinitatiza kujua jibu lake. Nashukuru mdau mmoja ametoa jibu (hilo hapo juu) ambalo nimekubaliana nalo kwa asilimia zote, wadau kutokana na jibu lake nimepata swali lingine, HIVI NI KWA NINI NCHI ZA KIAFRIKA ZINASHINDWA KUWEKA KIKAKATI IMARA YA KUHAKIKISHA KODI INALIPWA NA KILA ANAYEHITAJIKA KULIPA? NA NI KWANINI RUSHWA HAITHIBITIWI AFRIKA? NANI WA KULAUMIWA HAPA, WANANCHI AU VIONGOZI? Natanguliza shukrani wadau.

15 July 2009

Who is the richest person in Tanzania?


Leo nikiwa katika treni ya mawazo kama ada ya "Mtakatifu Kitururu" nimejikuta najiuliza nani ni mtu tajiri(wa mali)zaidi ya wote Tanzania. Kwa duniani tunaambiwa ni Bill Gates, wadau sikupata jibu hivyo nalileta swali kwenu. Naombeni msaada wenu. Natanguliza shukrani.

11 July 2009

Ngoma Africa band kupeleka mziki wa moto Ufini !Julai 18. 2009!


Bendi mashuhuri The Ngoma Africa yenye maskani yake nchini Ujerumani, inatarajiwa
kutumbuiza katika maonyesho ya Fest Afrika yatakayo fanyika mjini Tampere, huko Finland siku ya jumamosi 18-Julai-2009,kiongozi wa bendi hiyo Ras makunja atakiongoza
kikosi chake The Ngoma Africa band,aka FFU jukwaani,kikosi iko chenye kujizolea umaarufu kila kukicha kutokana na tabia yake ya kuwapeleka puta washabiki kwa mziki wa dansi,kinatarajiwa kuwasha mziki makali mjini Tampere,Ufini.
Ras Makunja amekaliliwa akisema kwamba The Ngoma Africa imepata hajira kwa wamiliki wa bendi ambao ni washabiki wa bendi kuwa ajira hiyo ni kuwapa burudani ka kukata na shoka! na ngoma africa itafanya kazi yake hiyo!.
Wadau wa Finland aka Ufini na Scandinavia kwa ujumla! waswahili usema! " Chereko Chereko na Mwenye mwana"! tucheze sote katika eneo la Klub,mjini Tampere,Finland.
wasikilize Ngoma africa hapa.

08 July 2009

Kazi ya mikono yangu.



Napenda sana kazi za mikono na hii ni moja ya kazi za mikono yangu. Wadau bado sijakubuhu katika hili naendelea kujifunza polepole. Ni maua ya kupamba keki niliyotengeneza kwa njia ya sugarcraft.

Ras Makunja kuhojiwa VOA


Radio VOA inawaletea mahojiano na Ras Makunja katika kipindi cha "Mziki Kutoka Afrika"
Ras Makunja kujibu hoja za bingwa wa maswali wa VOA!


Radio Voice of America idhaa ya kiswahili inayorusha matangazo yake kutoka mjini Washington DC, inawaletea mahojiano maalumu na kiongozi wa The Ngoma Africa band,Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu",majiano hayo yatasikika wakati wowote leo hii jumatano 8-07-2009 kwa wasikilizaji wa Afrika mashariki na kati,Mtangazaji wa radio VOA Bw.Abdushakur anamuhoji Ras Makunja kuhusu nafasi ya mziki wa dansi katika soko la kimataifa?Pia Misukosuko na mitihani gani? iliyokumbana na bendi hiyo hadi kufikia mafaniko ya kuhurudisha mziki wa dansi kwa kasi kubwa katika imaya ya jamii na washabiki wa ulaya ambako mziki huo wa dansi kwa sasa unatamba! mtangazaji wa VOA Bw.Abdushakur ambaye pia bingwa wa maswali alimuhoji mengi Ras Makunja kuhusu mziki na nyimbo za ngoma africa ambazo mara nyingi zimekuwa na ujumbe au ushauri muhimu kwa jamii,pia miziki wa dansi kwa nini ?umeelekeza kasi kubwa ulaya? Hili kusikiliza mahojiano hayo na majibu ya Ras Makunja pia unaweza kusikiliza katika mtandao wa radio VOA http://www.voanews.com/swahili ingia katika mziki kutoka Afrika.

05 July 2009

Serena bingwa wimbledon 2009




Serena williams amejinyakulia ushindi wa kombe la Wimbledon mwaka huu. Serena alikuwa akichuana na dada yake Venus Williams na bingwa mtetezi wa kombe hilo amemtoa dadayake kwa seti mfululizo 7-6, na 6-2. hii inafanya jumla ya Grand slams 11ambazo Serena amesha shinda hadi hivi sasa. Venus ana Gland slams 7. Hongereni sasa Venus na Serena.

03 July 2009

Serena na Venus Kuunguruma tena Wimbledon final 2009.


Ni kama mchezo wa kuigiza vile, jinsi hawa wadada wawili Venus na Serena wanavyojua kuitikisa dunia ya tenis. Mwaka huu tena wamefika fainali ya Wimbledon, mwaka jana 2008 pia walikuwa ni wao na Venus ndiye aliyeshinda. Nani atashinda mwaka huu bado ni fumbo, mambo yote ni kesho. Kila la heri Venus na Serena.

29 June 2009

The Ngoma Africa band kutingisha jukwaa tena ! AFRIKA FESTIVAL,Goeppingen City,Germany


The Ngoma Africa Band aka FFU!na mdundo wao wa "Bongo Dansi" wanatarajiwa kutingisha jukwaa lingine katika onyesho kubwa la Afrika Festival litakalo fanyika mjini Goeppingen,Ujerumani siku ya jumamosi ya 4 Julai 2009 saa 2.00 Usiku.
Bendi hiyo maarufu na dansi lake linalowatia kiwewe washabiki huko ughaibuni, wanasubiliwa kwa hamu na washabiki katika onyesho hilo.
Wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kuwasiliana kwa kupitia.
ngoma4u@googlemail.com

17 June 2009

Southern Highlands School - Mafinga, Iringa




Ujumbe kutoka kwa mdau Kitova:-

Ninapenda kuwajulisha, kwa watakaohitaji, kuhusu Southern Highlands School iliyopo mji wa Mafinga mkoani Iringa, Tanzania. Hii ni shule ya msingi ya bweni inayotumia kiingereza, yaani english medium boarding primary school, na ambayo tangu kuanzishwa kwake haijawahi kufelisha mtoto.

Hivi sasa Southern Highlands School inapokea wanafunzi kwa madarasa karibia yote.

Kwa walio USA, ukipenda kupata habari zaidi kuhusu hii shule na labda ungependa
kumpeleka mtoto wako au kumfadhili ndugu yako yeyote hapo SHS, basi unaweza kuwasiliana na mkurugenzi wa shule hiyo, ambaye yupo hapa USA kwa muda mfupi, kupitia namba 214-604-1726.

Ahsante.

15 June 2009

Baby manjula afunga mwaka. 10-06-2009.


Kweli siku hazigandi, Baby manjula sasa amefunga mwaka. Mwanangu nakutakia kila la heri katika maisha yako Mungu akulinde, akukuze na akutie maakili mengi uwe wa shoka. Ameni.

06 June 2009

Culture - Riverside. The song that lift me up when i'm down.

YouTube - Culture - Riverside.

For I woke on Saturday morning
Feeling sticky and dirty after work
Took a walk down a riverside

I roll a little spliff
Sat down on a stone and start to cool off
With my burden down a riverside

For I check around the youths
And I try to teach the truth
Lay their burden on the riverside

I walk through every corner
Try to find someone to talk to but I have to
Lay their burden on the riverside

For I walk and I talk
And I linger and I search
Lay their burden on the riverside

And I walk, I met the youthman pocket
And I try to search around them
Lay their burden on the riverside

And I sat down quietly
Watch the fishes circle around the little stones
Lay their burden on the riverside

I cup my ears and I heard the little birds
Whistling in the tree like so
Lay their burden on the riverside

Live good among your neighbor
Like sister and brother and
Come with me a riverside

All you need is pray to Jah, quality
You see secret shall be revealed
Lay their burden on the riverside

(solo)

Jah provides for the birds in the air
And the fishes in the sea so what about me
Lay their burden on the riverside

Look at the crow they toil not neither do they spin
Yet father provide far them
Lay their burden on the riverside

Let us walk and talk
And pray quietly in search
Lay their burden on the riverside

Look at the color of those clothes, oh Jah
Make each and every one individually
Lay their burden on the riverside

Where is the love?
Where is the togetherness too?
Lay their burden on the riverside

I can't take the war and I can't take the shooting
Neither the looting, just
Lay their burden on the riverside

I tried around Rema
Even in The Jungle
To find a quiet rest

Round there in a Nannyville
My heart come to a trail
Lay their burden on the riverside

And I knock, and I search
And I whisper and I preach
Lay their burden on the riverside

Where is the quietness
And the love to be found in some corner?
Lay their burden on the riverside

Let us walk, let us search
Let us examine and let us see
Lay their burden on the riverside.

19 May 2009

African Voices

Wadau kuna hii link nzuri sana msikose kuwa mnaipitia-pitia. African Voices.

13 March 2009

Lucy Kibaki amwaga cheche..

Fungua hapa upate habari kamili.

22 January 2009

I HAVE A DREAM SPEECH.


I am happy to join with you today in what will go down in history as the greatest demonstration for freedom in the history of our nation.

Five score years ago, a great American, in whose symbolic shadow we stand today, signed the Emancipation Proclamation. This momentous decree came as a great beacon light of hope to millions of Negro slaves who had been seared in the flames of withering injustice. It came as a joyous daybreak to end the long night of their captivity.

But one hundred years later, the Negro still is not free. One hundred years later, the life of the Negro is still sadly crippled by the manacles of segregation and the chains of discrimination. One hundred years later, the Negro lives on a lonely island of poverty in the midst of a vast ocean of material prosperity. One hundred years later, the Negro is still languishing in the corners of American society and finds himself an exile in his own land. So we have come here today to dramatize a shameful condition.


In a sense we have come to our nation's capital to cash a check. When the architects of our republic wrote the magnificent words of the Constitution and the Declaration of Independence, they were signing a promissory note to which every American was to fall heir. This note was a promise that all men, yes, black men as well as white men, would be guaranteed the unalienable rights of life, liberty, and the pursuit of happiness.

It is obvious today that America has defaulted on this promissory note insofar as her citizens of color are concerned. Instead of honoring this sacred obligation, America has given the Negro people a bad check, a check which has come back marked "insufficient funds." But we refuse to believe that the bank of justice is bankrupt. We refuse to believe that there are insufficient funds in the great vaults of opportunity of this nation. So we have come to cash this check — a check that will give us upon demand the riches of freedom and the security of justice. We have also come to this hallowed spot to remind America of the fierce urgency of now. This is no time to engage in the luxury of cooling off or to take the tranquilizing drug of gradualism. Now is the time to make real the promises of democracy. Now is the time to rise from the dark and desolate valley of segregation to the sunlit path of racial justice. Now is the time to lift our nation from the quick sands of racial injustice to the solid rock of brotherhood. Now is the time to make justice a reality for all of God's children.

It would be fatal for the nation to overlook the urgency of the moment. This sweltering summer of the Negro's legitimate discontent will not pass until there is an invigorating autumn of freedom and equality. Nineteen sixty-three is not an end, but a beginning. Those who hope that the Negro needed to blow off steam and will now be content will have a rude awakening if the nation returns to business as usual. There will be neither rest nor tranquility in America until the Negro is granted his citizenship rights. The whirlwinds of revolt will continue to shake the foundations of our nation until the bright day of justice emerges.

But there is something that I must say to my people who stand on the warm threshold which leads into the palace of justice. In the process of gaining our rightful place we must not be guilty of wrongful deeds. Let us not seek to satisfy our thirst for freedom by drinking from the cup of bitterness and hatred.

We must forever conduct our struggle on the high plane of dignity and discipline. We must not allow our creative protest to degenerate into physical violence. Again and again we must rise to the majestic heights of meeting physical force with soul force. The marvelous new militancy which has engulfed the Negro community must not lead us to a distrust of all white people, for many of our white brothers, as evidenced by their presence here today, have come to realize that their destiny is tied up with our destiny. They have come to realize that their freedom is inextricably bound to our freedom. We cannot walk alone.

As we walk, we must make the pledge that we shall always march ahead. We cannot turn back. There are those who are asking the devotees of civil rights, "When will you be satisfied?" We can never be satisfied as long as the Negro is the victim of the unspeakable horrors of police brutality. We can never be satisfied, as long as our bodies, heavy with the fatigue of travel, cannot gain lodging in the motels of the highways and the hotels of the cities. We cannot be satisfied as long as the Negro's basic mobility is from a smaller ghetto to a larger one. We can never be satisfied as long as our children are stripped of their selfhood and robbed of their dignity by signs stating "For Whites Only". We cannot be satisfied as long as a Negro in Mississippi cannot vote and a Negro in New York believes he has nothing for which to vote. No, no, we are not satisfied, and we will not be satisfied until justice rolls down like waters and righteousness like a mighty stream.

I am not unmindful that some of you have come here out of great trials and tribulations. Some of you have come fresh from narrow jail cells. Some of you have come from areas where your quest for freedom left you battered by the storms of persecution and staggered by the winds of police brutality. You have been the veterans of creative suffering. Continue to work with the faith that unearned suffering is redemptive.

Go back to Mississippi, go back to Alabama, go back to South Carolina, go back to Georgia, go back to Louisiana, go back to the slums and ghettos of our northern cities, knowing that somehow this situation can and will be changed. Let us not wallow in the valley of despair.

I say to you today, my friends, so even though we face the difficulties of today and tomorrow, I still have a dream. It is a dream deeply rooted in the American dream.

I have a dream that one day this nation will rise up and live out the true meaning of its creed: "We hold these truths to be self-evident: that all men are created equal."

I have a dream that one day on the red hills of Georgia the sons of former slaves and the sons of former slave owners will be able to sit down together at the table of brotherhood.

I have a dream that one day even the state of Mississippi, a state sweltering with the heat of injustice, sweltering with the heat of oppression, will be transformed into an oasis of freedom and justice.

I have a dream that my four little children will one day live in a nation where they will not be judged by the color of their skin but by the content of their character.

I have a dream today.

I have a dream that one day, down in Alabama, with its vicious racists, with its governor having his lips dripping with the words of interposition and nullification; one day right there in Alabama, little black boys and black girls will be able to join hands with little white boys and white girls as sisters and brothers.

I have a dream today.

I have a dream that one day every valley shall be exalted, every hill and mountain shall be made low, the rough places will be made plain, and the crooked places will be made straight, and the glory of the Lord shall be revealed, and all flesh shall see it together.

This is our hope. This is the faith that I go back to the South with. With this faith we will be able to hew out of the mountain of despair a stone of hope. With this faith we will be able to transform the jangling discords of our nation into a beautiful symphony of brotherhood. With this faith we will be able to work together, to pray together, to struggle together, to go to jail together, to stand up for freedom together, knowing that we will be free one day.

This will be the day when all of God's children will be able to sing with a new meaning, "My country, 'tis of thee, sweet land of liberty, of thee I sing. Land where my fathers died, land of the pilgrim's pride, from every mountainside, let freedom ring."

And if America is to be a great nation this must become true. So let freedom ring from the prodigious hilltops of New Hampshire. Let freedom ring from the mighty mountains of New York. Let freedom ring from the heightening Alleghenies of Pennsylvania!

Let freedom ring from the snowcapped Rockies of Colorado!

Let freedom ring from the curvaceous slopes of California!

But not only that; let freedom ring from Stone Mountain of Georgia!

Let freedom ring from Lookout Mountain of Tennessee!

Let freedom ring from every hill and molehill of Mississippi. From every mountainside, let freedom ring.

And when this happens, when we allow freedom to ring, when we let it ring from every village and every hamlet, from every state and every city, we will be able to speed up that day when all of God's children, black men and white men, Jews and Gentiles, Protestants and Catholics, will be able to join hands and sing in the words of the old Negro spiritual, "Free at last! free at last! thank God Almighty, we are free at last!"

ABAMA INAUGURATION SPEECH.

Wadau hapo chini ni hotuba aliyotoa Obama siku aliyoapishwa kuwa Rais wa Marekani.

My fellow citizens:

I stand here today humbled by the task before us, grateful for the trust you have bestowed, mindful of the sacrifices borne by our ancestors. I thank President Bush for his service to our nation, as well as the generosity and cooperation he has shown throughout this transition.

Forty-four Americans have now taken the presidential oath. The words have been spoken during rising tides of prosperity and the still waters of peace. Yet, every so often the oath is taken amidst gathering clouds and raging storms. At these moments, America has carried on not simply because of the skill or vision of those in high office, but because We the People have remained faithful to the ideals of our forbearers, and true to our founding documents.

So it has been. So it must be with this generation of Americans.

That we are in the midst of crisis is now well understood. Our nation is at war, against a far-reaching network of violence and hatred. Our economy is badly weakened, a consequence of greed and irresponsibility on the part of some, but also our collective failure to make hard choices and prepare the nation for a new age. Homes have been lost; jobs shed; businesses shuttered. Our health care is too costly; our schools fail too many; and each day brings further evidence that the ways we use energy strengthen our adversaries and threaten our planet.

These are the indicators of crisis, subject to data and statistics. Less measurable but no less profound is a sapping of confidence across our land - a nagging fear that America's decline is inevitable, and that the next generation must lower its sights.


Today I say to you that the challenges we face are real. They are serious and they are many.

They will not be met easily or in a short span of time. But know this, America - they will be met. On this day, we gather because we have chosen hope over fear, unity of purpose over conflict and discord.

On this day, we come to proclaim an end to the petty grievances and false promises, the recriminations and worn out dogmas, that for far too long have strangled our politics.

We remain a young nation, but in the words of Scripture, the time has come to set aside childish things. The time has come to reaffirm our enduring spirit; to choose our better history; to carry forward that precious gift, that noble idea, passed on from generation to generation: the God-given promise that all are equal, all are free, and all deserve a chance to pursue their full measure of happiness.

In reaffirming the greatness of our nation, we understand that greatness is never a given. It must be earned. Our journey has never been one of short-cuts or settling for less. It has not been the path for the faint-hearted - for those who prefer leisure over work, or seek only the pleasures of riches and fame. Rather, it has been the risk-takers, the doers, the makers of things - some celebrated but more often men and women obscure in their labor, who have carried us up the long, rugged path towards prosperity and freedom.

For us, they packed up their few worldly possessions and traveled across oceans in search of a new life.

For us, they toiled in sweatshops and settled the West; endured the lash of the whip and plowed the hard earth.

For us, they fought and died, in places like Concord and Gettysburg; Normandy and Khe Sahn. Time and again these men and women struggled and sacrificed and worked till their hands were raw so that we might live a better life. They saw America as bigger than the sum of our individual ambitions; greater than all the differences of birth or wealth or faction.

This is the journey we continue today. We remain the most prosperous, powerful nation on Earth. Our workers are no less productive than when this crisis began. Our minds are no less inventive, our goods and services no less needed than they were last week or last month or last year. Our capacity remains undiminished. But our time of standing pat, of protecting narrow interests and putting off unpleasant decisions - that time has surely passed. Starting today, we must pick ourselves up, dust ourselves off, and begin again the work of remaking America.

For everywhere we look, there is work to be done. The state of the economy calls for action, bold and swift, and we will act - not only to create new jobs, but to lay a new foundation for growth. We will build the roads and bridges, the electric grids and digital lines that feed our commerce and bind us together. We will restore science to its rightful place, and wield technology's wonders to raise health care's quality and lower its cost. We will harness the sun and the winds and the soil to fuel our cars and run our factories. And we will transform our schools and colleges and universities to meet the demands of a new age. All this we can do. And all this we will do.

Now, there are some who question the scale of our ambitions - who suggest that our system cannot tolerate too many big plans. Their memories are short. For they have forgotten what this country has already done; what free men and women can achieve when imagination is joined to common purpose, and necessity to courage.

What the cynics fail to understand is that the ground has shifted beneath them - that the stale political arguments that have consumed us for so long no longer apply. The question we ask today is not whether our government is too big or too small, but whether it works - whether it helps families find jobs at a decent wage, care they can afford, a retirement that is dignified. Where the answer is yes, we intend to move forward. Where the answer is no, programs will end. And those of us who manage the public's dollars will be held to account - to spend wisely, reform bad habits, and do our business in the light of day - because only then can we restore the vital trust between a people and their government.

Nor is the question before us whether the market is a force for good or ill. Its power to generate wealth and expand freedom is unmatched, but this crisis has reminded us that without a watchful eye, the market can spin out of control - and that a nation cannot prosper long when it favors only the prosperous. The success of our economy has always depended not just on the size of our Gross Domestic Product, but on the reach of our prosperity; on our ability to extend opportunity to every willing heart - not out of charity, but because it is the surest route to our common good.

As for our common defense, we reject as false the choice between our safety and our ideals. Our Founding Fathers, faced with perils we can scarcely imagine, drafted a charter to assure the rule of law and the rights of man, a charter expanded by the blood of generations. Those ideals still light the world, and we will not give them up for expedience's sake. And so to all other peoples and governments who are watching today, from the grandest capitals to the small village where my father was born: know that America is a friend of each nation and every man, woman, and child who seeks a future of peace and dignity, and that we are ready to lead once more.

Recall that earlier generations faced down fascism and communism not just with missiles and tanks, but with sturdy alliances and enduring convictions. They understood that our power alone cannot protect us, nor does it entitle us to do as we please. Instead, they knew that our power grows through its prudent use; our security emanates from the justness of our cause, the force of our example, the tempering qualities of humility and restraint.

We are the keepers of this legacy. Guided by these principles once more, we can meet those new threats that demand even greater effort - even greater cooperation and understanding between nations. We will begin to responsibly leave Iraq to its people, and forge a hard-earned peace in Afghanistan. With old friends and former foes, we will work tirelessly to lessen the nuclear threat, and roll back the specter of a warming planet. We will not apologize for our way of life, nor will we waver in its defense, and for those who seek to advance their aims by inducing terror and slaughtering innocents, we say to you now that our spirit is stronger and cannot be broken; you cannot outlast us, and we will defeat you.

For we know that our patchwork heritage is a strength, not a weakness. We are a nation of Christians and Muslims, Jews and Hindus - and non-believers. We are shaped by every language and culture, drawn from every end of this Earth; and because we have tasted the bitter swill of civil war and segregation, and emerged from that dark chapter stronger and more united, we cannot help but believe that the old hatreds shall someday pass; that the lines of tribe shall soon dissolve; that as the world grows smaller, our common humanity shall reveal itself; and that America must play its role in ushering in a new era of peace.

To the Muslim world, we seek a new way forward, based on mutual interest and mutual respect.

To those leaders around the globe who seek to sow conflict, or blame their society's ills on the West - know that your people will judge you on what you can build, not what you destroy. To those who cling to power through corruption and deceit and the silencing of dissent, know that you are on the wrong side of history; but that we will extend a hand if you are willing to unclench your fist.

To the people of poor nations, we pledge to work alongside you to make your farms flourish and let clean waters flow; to nourish starved bodies and feed hungry minds. And to those nations like ours that enjoy relative plenty, we say we can no longer afford indifference to suffering outside our borders; nor can we consume the world's resources without regard to effect. For the world has changed, and we must change with it.

As we consider the road that unfolds before us, we remember with humble gratitude those brave Americans who, at this very hour, patrol far-off deserts and distant mountains. They have something to tell us today, just as the fallen heroes who lie in Arlington whisper through the ages.

We honor them not only because they are guardians of our liberty, but because they embody the spirit of service; a willingness to find meaning in something greater than themselves. And yet, at this moment - a moment that will define a generation - it is precisely this spirit that must inhabit us all.

For as much as government can do and must do, it is ultimately the faith and determination of the American people upon which this nation relies. It is the kindness to take in a stranger when the levees break, the selflessness of workers who would rather cut their hours than see a friend lose their job which sees us through our darkest hours. It is the firefighter's courage to storm a stairway filled with smoke, but also a parent's willingness to nurture a child, that finally decides our fate.

Our challenges may be new. The instruments with which we meet them may be new. But those values upon which our success depends - hard work and honesty, courage and fair play, tolerance and curiosity, loyalty and patriotism - these things are old. These things are true. They have been the quiet force of progress throughout our history. What is demanded then is a return to these truths. What is required of us now is a new era of responsibility - a recognition, on the part of every American, that we have duties to ourselves, our nation, and the world, duties that we do not grudgingly accept but rather seize gladly, firm in the knowledge that there is nothing so satisfying to the spirit, so defining of our character, than giving our all to a difficult task.

This is the price and the promise of citizenship.

This is the source of our confidence - the knowledge that God calls on us to shape an uncertain destiny.

This is the meaning of our liberty and our creed - why men and women and children of every race and every faith can join in celebration across this magnificent mall, and why a man whose father less than sixty years ago might not have been served at a local restaurant can now stand before you to take a most sacred oath.

So let us mark this day with remembrance, of who we are and how far we have traveled. In the year of America's birth, in the coldest of months, a small band of patriots huddled by dying campfires on the shores of an icy river. The capital was abandoned. The enemy was advancing. The snow was stained with blood. At a moment when the outcome of our revolution was most in doubt, the father of our nation ordered these words be read to the people:

"Let it be told to the future world...that in the depth of winter, when nothing but hope and virtue could survive...that the city and the country, alarmed at one common danger, came forth to meet [it]."

America. In the face of our common dangers, in this winter of our hardship, let us remember these timeless words. With hope and virtue, let us brave once more the icy currents, and endure what storms may come. Let it be said by our children's children that when we were tested we refused to let this journey end, that we did not turn back nor did we falter; and with eyes fixed on the horizon and God's grace upon us, we carried forth that great gift of freedom and delivered it safely to future generations.

20 January 2009

OBAMA AMEAPISHWA RASMI LEO.


Leo dunia imeshuhudia tukio ambalo lilikuwa likionekana kama ndoto kutokea. Historia imewekwa leo nchini Marekani ambapo kwa mara ya kwanza nchi hiyo itaongozwa na mtu mweusi Barack Obama. Barack Obama aliapishwa leo na kuwa rais wa 44 wa taifa hilo.Marais wengine ni pamoja na:-FUNGUA HAPA
Tunaomba MUNGU awe nawe na akulinde popote uendako. AMEN.

17 January 2009

AJALI ZA BARABARANI ZINATUMALIZIA WAPENDWA WETU BONGO....Ujumbe toka kwa da'Janeth Jesse.

Napenda kuleta dukuduku langu kwa wadau wote wa blog yetu ya jamii ili tulijadili ktk kujenga kuhusu AJALI ZA BARABARANI BONGO,jamani kwakweli tumechoka watu wanateketea imefikia steji sasa na tuseme ENOUGH IS ENOUGH sasa na sisi,haijatimia hata week1 tangia basi la kampuni ya TASHRIFF liwafyeke abiria zaidi ya nusu waliokuwa wakisafiri (30)na wengine 29 kulazwa ktk hospital za muheza teule na bombo tanga,huu ni msiba mkubwa sana UHAI NI KITU CHA THAMANI NAFUU MTU AKUIBIE HELA AU MADINI KULIKO AKUTOE ROHO YAKO.Basi la kampuni hiihii wadau mkumbuke lilishawahi kupoteza maisha ya abiria (78) lilipofunikwa na maji meneo ya kibanda muheza tanga.KITU GANI kifanyike wadau kuepuka vifo vya kizembe vya namna hii?dereva kaua kakimbia ni mhuni anakabidhiwa chombo kilichobeba roho za watu,kwa uzoefu wangu wa kuishi bongo miaka mingi naamini karibia nusu ya waendesha magari daresalaam mjini hawana leseni na nusu ya waendesha vyombo wanaendesha wamelewa,ni kawaida kuwakuta watu wamepaki magari yao bar wanakunywa pombe kisha wanaendesha,jamani jamani tunauana jama.HILI JESHI LA POLISI KITENGO CHA TRAFFIC utawakuta wote wana vitambi kwa rushwa na kutafutia watu leseni kwa njia za mazabe.JK MAISHA BORA NI PAMOJA NA SHERIA KALI ZA BARABARANI KWANI ZINAHUSU UHAI AMBAO NI KITU CHA THAMANI KULIKO CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)....mungu ibariki tanzania mungu ibariki afrika. mdau wa kwasemgaya safarini DENMARK mara1

01 January 2009

HERI YA MWAKA MPYA 2009!!!!


Wadau wote duniani ninawatakieni kila la heri katika mwaka mpya 2009. MUNGU AWABARIKI.

05 November 2008

Behind the Success of every Man, there is a Woman..,Michell Obama... First lady USA 2009-2012


Michell Obama

Hongera Baraka Obama... YES WE CAN!!!!!...


Ameyashinda mauti....

03 November 2008

NIFAHAMISHE.COM....Website mpya kabisa ya habari na burudani.

Nifahamishe.com ni website mpya ambayo inakuja na mambo mbali
mbali kwaajili ya watanzania
Baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye nifahamishe.com ni kama ifuatavyo
->( Breaking news za bongo na duniani ) Habari mbali mbali za Tanzania
na za kimataifa
->Habari katika picha na video
->Live radio
->Online Games
->Habari za burudani na wasanii wa bongo
->Utaweza kusikiliza nifahamishe nonstop bolingo na lingala mix
->Kuuza kwa kuweka tangazo lako bure au kununua nyumba,magari,vitu vya
electronics na kadhalika
->Kushare picha na watanzania duniani

KARIBU NIFAHAMISHE.COM

13 July 2008

Baby Manjula huyu hapa...



Wadau na wanablogu wote kwa ujumla, nina furaha kuwapasha habari kwamba mwezi uliopita June 10 2008, Nilipata mtoto wa kike anayekwenda kwa jina la Manjula. Manjula anaendelea vizuri na muda si mrefu na yeye atajiunga katika ulimwengu wa ku-blogu anaomba baraka zenu wadau.

29 April 2008

Filamu zinazowania tuzo ya Vinara wa Filamu Tanzania zatajwa

Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.
Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.
Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.
Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.
Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.
Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.
Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.
Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.
Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers

30 March 2008

FOMU ZA TUZO ZA VINARA ZATOLEWA.

Fomu za ushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Vinara wa
filamu Tanzania 2007/8 zimeanza rasmi kutolewa jana katika vituo
mbalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutolewa kwa tuzo
hizo.
Tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, zimeandaliwa na
kampuni ya One Game Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya dovu Power Malt.
Mratibu tuzo hizo, Khadija Khalili, amesema kuwa, kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wao, fomu hizo zilichelewa kutoka kwa tarehe ya
awali hivyo kusababisha kuongezwa kwa muda wa kurejeshwa fomu na
kupokea filamu zitakazoshiriki katika tuzo hizo hadi Aprili 18 badala
ya Machi 31 kama ilivyotangazwa awali.
Alisema watengenezaji wa filamu nchini wanakaribishwa kutuma nakala za
filamu zilizotengenezwa kati ya Januari 2007 hadi Machi 31, 2008, kwa
ajili ya kuwania tuzo hizo.
Khalili alisema kuwa, jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18
kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.
Alisema fomu za kushiriki kuwania tuzo hizo zinapatikana katika vituo
vilivyotangazwa awali ambavyo ni ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kwa Omari Mayanga, pia zinapatikana kwa wasambazaji wa filamu
ambao ni Wananchi Wote, GMC, Kapico na Game First Quality.
"Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD na
DVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar
es Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.
Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni Filamu
Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa
Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji
Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,
Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa
Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike
(supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora
kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa
Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi. Pia itatolewa tuzo ya
heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.

13 March 2008

Je serikali inalichukuliaje hili?..


Wadau naomba tuisome habari hii hapa halafu tujadili je serikali ina mpango gani hasa juu ya maalbino? kwa sababu hadi sasa hivi bado sijaona hatua yoyote inayochukuliwa, hivi jamani ni haki wanayofanyiwa wenzetu?

22 February 2008

Kazi mpya za Msanii Hendrix Lilanga.





Msanii mchoraji maarufu anayeendeleza kazi za babu yake, Hendrix Lilanga ametuletea kazi zake mpya za kufungua mwaka. Hendrix amefungua pia ukurasa wa kazi zake katika mtandao wa picha wa flickr, mtembelee ujionee mwenyewe mambo yake. Anuani yake ya barua pepe bado ni ileile hendrylilanga@yahoo.com au unaweza kuwasiliana nami kwa maelezo zaidi juu ya kazi zake tumia dadamija@yahoo.com

21 February 2008

Hongera kwa siku ya kuzaliwa 21/02.



Leo mzee Mugabe na mwanangu wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa, sasa huwa najiuliza sijui na bibie atakuwa na msimamo kama wa babu?, jibu sipati. Lakini yote maisha cha maana Mungu awazidishie maisha marefu. Happy birthday wooote waliozaliwa siku hii.

20 February 2008

Unawafahamu African Mama's?


Basi kama hauwafahamu au hata kama unawafahamu basi jaribu kuwapitia hapa halafu utaniambia mwenyewe kama si wanawake wa shoka hawa.

Je unataka kuwa wa shoka? Fuatilia vidokezo hapo chini.


Wataalamu wanasema kuwa mtu wa shoka si lelemama, inahitaji nidhamu ya hali ya juu katika uendeshaji wako wa maisha ya kila siku. Kwanza kabisa wanakuambia THINK BIG! Endelea msomaji...


Talent: Our Creator has endowed all of us not just with the ability to
sing, dance or throw a ball, but with intellectual talent. Start
getting in touch with that part of you that is intellectual and
develop that,
and think of careers that will allow you to use that.

Honesty: If you lead a clean and honest life, you don't put skeletons
in the closet. If you put skeletons in the closet, they definitely
will
come back just when you don't want to see them and ruin your life.

Insight: It comes from people who have already gone where you're trying
to go. Learn from their triumphs and their mistakes.

Nice: If you're nice to people, then once they get over the suspicion
of why you're being nice, they will be nice to you.

Knowledge: It makes you into a more valuable person. The more knowledge
you have, the more people need you. It's an interesting
phenomenon,
but when people need you, they pay you, so you'll be okay in
life.

Books: They are the mechanism for obtaining knowledge, as opposed to
television.

In-Depth Learning: Learn for the sake of knowledge and understanding,
rather than for the sake of impressing people or taking
a test.

God: Never get too big for Him.

19 February 2008

Wamama..


Hivi ule usemi usemao mafanikio ya mwanaume kwa kiwango kikubwa huchangiwa na mwanamke, ikiwa na maana mkewe ni wa kweli? na kama ni wa kweli je wake za viongozi nao wanaweza kuwekwa katika kundi la wanawake wa shoka?

Nawauliza wadau swali hili kwa vile nimekuwa nikijiuliza sana kama wake wa viongozi ni wanawake wa shoka au vinginevyo. Tusaidiane jamani.

29 November 2007

Kazi mbalimbali za Hendrix Lilanga





03 November 2007

Sanaa ya George lilanga chini ya mrithi hendrix Lilanga.


Pichani ni mimi na Msanii Hendrix lilanga.

Hapo awali nilitoa changamoto ya picha ya sanaa na kuwataka wadau wangu kumtambua mwanzilishi wake. Wadau mmejitahidi lakini bahati mbaya jibu sahihi halikuweza kupatikana. Leo napenda kutoa jibu la swali lile. Sanaa ile ni ya mkongwe marehemu GEORGE LILANGA, lakini imechorwa na Mjukuu wake mkubwa ndugu Hendrix Lilanga ambaye pia ndiye mrithi wa shughuli zote alizokuwa akifanya babu yake.

Nilibahatika kukutana na Hendrix Lilanga hivi karibuni, tuliongea mengi ikiwa ni pamoja na mikakati aliyoiweka katika kutaka kuiendeleza kazi ya babu yake. Kwa kifupi alinieleza kwamba yeye alizaliwa Tegeta mkoa wa Dar es Salaam tarehe 20/10/1974.
Alipata elimu yake ya msingi mkoani Tanga, lakini hakuweza kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na matatizo ya kifamilia. Ndipo mwaka 1993 babu yake aliamua kumuingiza rasmi mjukuu wake katika shughuli za sanaa aliyokuwa akiifanya. Mzee Lilanga alimfundisha shughuli

1. Kuchora Oil Painting katika Carnivals, Hard Boad
2. Water Colour Painting katika Karatasi
3. Batick Picture
4. Goat Skin Drawings
5. Vibuyu ( Callabash Drawings)

Hendrix hakuishia hapo, Mwaka 2007 alihudhuria course ya Graphic katika Chuo cha Enternational Summer Academy Salzburg kilichoko Austria.

Kwa upande wa maonesho ameshafanya maonesho yafuatayo:-
1. Bagamoyo Arts Festival mwaka 1999 Tanzania
2. Art in Tanzania mwezi 11 mwaka 2000
3. Art in Tanzania mwezi 11 mwaka 2001
4. Real Art Gallery mwezi 7 mwaka 2006 Zanzibar
5. Tanart Enterprises mwezi 6 mwaka 2007 Dar es Salaam Tanzania
6. International summer Academy, mwezi 8 mwaka 2007 Salzburg Austria.

Kwa sasa anaendelea na shughuli za sanaa za michoro na kufundisha wasanii chipukizi mbinu mbali mbali katika mambo ya sanaa kwa ujumla. Yuko mbioni kutengeneza website yake ili watu wengi waweze kufaidika na michoro ya sanaa afanyazo. Na anapatikana kwa anuani hii hendrylilanga@yahoo.com

Ajali barabarani nchini....na Born again Pagan

Nimepokea maoni maridhawa kutoka kwa baba yetu mpendwa BAP, hebu tuyasome na kujadili kimapana anayosema, endelea ndugu msomaji...

Hivi karibuni, katika mojawapo ya blogu nyingi mashuhuri za wa-Tanzania, niliahidi kwa kuwaomba wanakijiji kujipa muda wa tutafakuri na kuchangia suala la ajali barabarani na jinsi ambavyo tunaweza kupunguza “balaa” hili ambalo linaendelea kutusibu siku hadi siku, mchana na usiku.

Ingawa ni wanakijiji kama wawili hivi walichangia, sikukata tamaa.

Nazidi kuwaombeni tujaze blogu hizi kwa maoni yetu kuhusu maafa ya ajali barabarani. Blogu hizi zinasomwa na wengi, wakiwemo viongozi wa serikali, wabunge wetu, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya serikali.

Napenda kurudia mchango wangu wa awali kuhusu ajali nchini mwetu, ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kutokwa na Naibu Waziri Salome Mbatia. Mhariri wa gazeti maarufu nchini la kila siku aliandika, “…taifa limeghubikwa na majonzi makubwa kufuatia kifo (cha Naibu Waziri Salome Mbatia) kilichotokana na ajali ya gari eneo la Kibena, Njombe mkoani Iringa Alhamisi.”

Lakini yatubidi kuzingatia kwamba si Salome Mbatia peke yake aliyekufa katika ajali hiyo. Dereva wake na utingo wa lori nao walikufa.

Na sio ajali hiyo tu iliyotokea siku hiyo na kusababisha mauaji! Karibu watu kama kumi hivi walikufa kwa ajali barabarani siku hiyo! Lakini kifo cha Naibu Waziri Salome Mbatia kimepewa kipaumbele zaidi ya vifo vya wengine. Sababu zinaeleweka; sina haja ya kuzirudia.

Mhariri huyo alitoa tahadhari kali kuitaka “Serikali na vyombo husika na sekta ya usafirishaji” kudhibiti ajali: “[Y]afaa tatizo hili la ajali za barabarani zinazotokana na uzebe na mwendo wa kasi litizamwe tena kwa makini.
Bado linapoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia wakati zinaweza kuepukwa. Madereva wengi bado wamekuwa ni vichwa maji katika uendeshaji wao barabarani.”

Kauli kama hiyo ya mhariri, sambamba na kauli nyingi za umma zisizotangazwa, inaitaka serikali yetu kamwe isingoje “kifo cha mzaliwa wa kwanza”, kama mtawala Firauni wa Misri, ndipo iamke na kufanya lolote dhidi ya “janga” hili ambalo hudonoa maisha ya wa-Tanzania wetu!

Tumezoea kusema, “Ajali haina kinga!” Lakini ukweli ni kwamba ajali inaweza ikakingika!
Wengine husema, “Ngoja ajali ziwamalize kwa kumwonea Kabwe Zubeir Zitto!”

Hili nitalizungumzia kwa kifupi:

Katika magazeti na blogu nyingi kumeibuka tabaka la washirikina au niwaite “wanajimu wabaya, watabiri mabaya, wenye ndoto mbaya, wenye maono” wenye kungojea “kiyama” kiikumbe serikali na CCM yake.

Wenzetu wanamwomba m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe aombe miungu ya huko kwao Kigoma kuweka breki ili isiwamalize wote wale waliomnyoshea kidole - mizimu ya Kigoma inalipa kisasi!

Wanaoanisha msululu wa ajali ambazo zimetokea kwa baadhi ya viongozi wa CCM kufuatia mzozo wa m-Bunge wetu “kijana” Zitto Zubeir Kabwe eti zinatokana na “kumwonea Zitto”!

Natarajia kuchangia hili la mzozo wa Zitto, kulingana na maoni ya wasomi wetu wawili: Prof. Gidion Shoo (Zitto Hakuwatendea Mema Wananchi,” kwa mujibu wa “Kanuni za Bunge”. Msomi mwingine ni Prof. Shivji (Zitto Kabwe’s Suspension an Episode or an Epitah?)

Kero ya Zitto yaonyesha jinsi ambavyo nchi yetu imejigawa. Kuna ukweli kwamba wote hatuimbi, “Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote; nilalapo nakuota, jina lako ni tamu sana”!

Ni lazima kuna sababu zake, mbali ya vitendo vya rushwa na ufisadi!

Kuna baadhi yetu ambao wamegeuka washirikina na kuonyesha hali ya chini kabisa. Hawa wanaomba mabaya zaidi yawapate wana-CCM, kwa jumla, na hasa wale viongozi waliojeruhiwa katika ajali mbali mbali!

Sioni kama hili ni ombi la kiungwana! Ni matakwa ya wendawazimu kwani endapo CCM inafanya mabaya, kuitakia mabaya nako ni vibaya! Makosa mawili hayajengi au hayazai haki!

Kumtakia mwenzako kifo ni sawa na kumwua tu. Leo tunatakiana vifo; kesho tutauana kimacho macho!

Kuna wengine wenye kuamini kuwa ajali “Ni mipango ya Mungu - Mungu kapenda; siku yako ya kufa ikifika, imefika!”

Hili pia yanataka ufafanuzi:

Je, maisha yetu yamewekewa
“blinkers” za “determinism”? Je, hakuna lolote tunaloweza kufanya kuepusha hiyo “determinism”? Mbona tunataka kuingilia kati nguvu za asili (nature) kwa kualika nchini “wachawi wa mvua” kutoka Thailand?

Maisha yanajengeka kutokana na kuoana kwa akili zetu na maingilio ya mazingira tuliyomo. Tunaweza kuyabadili kwa kupata elimu tosheleza na hekima ya kuweza kutafukari na kutafuta njia za kusuluhisha au kutanzua tatizo la ajali barabarani.

Wengine, hasa wadini walokoke huamini kuwa Mungu huadhibu kwa sababu ya dhambi. Hii sio kwa wa-Tanzania tu bali pia wahubiri wengi walokoke duniani, hususani, Marekani.

Mhubiri mmoja mlokoke wa Amerika aliwahi kutamka kuwa Jimbo la Florida lilipatwa na madhara ya kuwaka moto kutokana na dhambi za kisenge na kishoga.

Mlokoke huyo huyo alimshutumu Waziri Mkuu wa Israel kwa kupatwa na mshituko uliomlemaza kuwa ni kwa sababu kagawa nchi ya Palestine - nchi ya Mungu - kwa Wapalestina!

Kisa kingine cha hivi karibuni: Jaji wa “federal” hapa Amerika ameamuru kanisa moja la Ki-Baptist la Westboro - kanisa lenye kuhubiri na kueneza chuki - kulipa faini ya dola millioni 10.9 kwa kushangilia kifo na kukielezea kifo hicho cha askari Lance Cpl Matthew Snyder vitani Iraq Machi 2006 kuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu.

Washirika walokoke wengi wa hapa Amerika wanahubiri ‘injili ya chuki” dhidi ya ushoga na kubagua mazishi ya watu waliokufa kwa ukimwi. Walokole wengine wanaamini kuwa Amerika inapata majanga, kama hilo la 911, kwa sababu wameacha kumcha Mungu!

Je, Mungu anatuadhibu na hizo ajali zitokeazo barabarani?

Pengine hilo la ajali na kudra za Mwenyenzi Mungu nalo linahitaji muda wake maalum wa kutafukari kwa undani, hasa kwa wale wenye kutaka kujua kutoka kwa wanaolielewa vizuri.

Kuna baadhi yetu wenye kuziona na kuzitafukari ajali barabarani na kwinginepo, kama matukio ya kawaida tu. Tusitekwe nyara na fikra za kufungwa macho yetu na akili zetu kuamini kwamba ajali haina kinga; ajali ni adhabu ya Mungu, au ni matakwa mengine ya ushirikina. Ajali husababishwa na/au mchanganyiko wa haya matatu:
dereva, gari na barabara.

Kuna Ripoti ya Mwaka 1994 inayoelezea rasmi na kwa undani kuhusu usafiri nchini. Sijui ni wangapi kati ya matrafiki husika, wamiliki wa magari, maderera na abiria wa kawaida wameipitia ripoti hii?

Kuna vitu vitatu muhimu katika njia za usafiri wa nchi kavu kwa kutumia magari barabarani: dereva, gari na barabara. Kila kimoja kina masharti yake sawa na “social environment”: mshiriki (actor/participant), kusudi (purpose), sheria (rules and regulations), mipaka (boundaries), maadili (morality), siasa (what is to be done), na lugha (technical language).

Dereva: Kulingana na Ripoti hiyo, sababu kubwa ya ajali nchini mwetu hutokana na madreva wenyewe. Ajali za namna hii ni kiasi cha asilimia 76.

Napenda kuongezea kuwa u-mahiri na u-makini wa kuendesha unatokana na mafunzo tosheleza na utahini usiopendelea; dereva kujiandaa vya kutosha kabla ya safari; asiendeshe huku amelewa au amechoka; afuate sheria za barabarani; na uwezo wa dereva kubaini endapo gari lake lina udhaifu au kasoro.

Ajali nyingi za mabasi, malori yetu na magari madogo yetu kugongana vichwa kwa vichwa, kama ajali hiyo iliyotokea na na kuchukua maisha ya wakina Waziri Mbatia, dereva na utingo wa lori.

Hii ina maana kuwa sababu kubwa ni pale dereva wa gari linalofuata kutaka ku-“overtake” lililotangulia karibu na mwisho wa kilima au kwenye kona kali bila kujua kuwa kuna gari lingine linakuja mbele.

Wakati mwingine gari hupata kasoro na dereva kushindwa kuliongoza. Sababu nyingine ni kwa dereva kuchoka na kusinzia sinzia na mwisho kupoteza saiti yake.
Madereva wengine huendesha kulingana na wimbo wa mapenzi wa Daudi Kabaka (Kenya), ambapo abiria anamsihi dereva wa basi aongeze spidi ili abiria afike au awahi “date” yake:

Dereva,
Choma gari moto;
Nifike upesi
Nikaone mtoto.
Mtoto ananingoja
Stendi ya basi;
Fanya haraka!

Kuna pia baadhi ya abiria wenye kutaka kufika mapema kungali na jua kule waendapo. Abiria kama hao huimiza dereva aendeshe kwa kasi.

Madereva wengine nao wanapenda sana kuendesha kwa kasi ili wapate muda wa kupumzika, na kupata angalau “moja baridi” au kuwaona wapenzi wao huko waendapo au mwisho wa safari.

Madereva wengine ni walevi; hupenda kunywa vileo kabla ya safari na wakati mwingine kupumzika safarini kwenye visima vya ulevi.

Ukiwa Dar es Salaam, mabasi ya kwenda katika mikoa mingine yanaitwa “mabasi ya kwenda mikoani”, kana kwamba Dar es Salaam si mkoa.

Kuna mabasi mengine, kwa mfano, huondoka Dar kwenda Mwanza kupitia Nairobi (Kenya) huwa yana madereva wawili tu. Kuna pia mabasi yanayoondoka Dar es Salaam kwenda Lubumbashi huko Kongo (Kinshasa) kupitia Kitwe (Zambia).

Habari za kuaminika zinaeleza kuwa wakati mwingi madereva huchoka kuendesha na kuanza kusinzia sinzia na huku wakiendesha.

Kuna madereva wengine wenye ka-tabia ka kuendesha magari kana kwamba wana-“enjoy the cruising moment.”

Madereva wengine vichwamaji huwazuia wenzao wasipite; ni kama umewatukana. Hivyo huendesha kwa ujeuri kana kwamba kuna ugomvi au vita.

Madereva wengine, hasa kwenye barabara zetu zisizo na lami, wanapenda sana kutangulia kuepuka au kuogopa mavumbi yanayoachwa na gari liliotangulia. Huwa ni mashindano.

Kuna wengine, hasa wamiliki, hupenda sana kushindana kuwa wa kwanza kuchukua abiria au shehena kabla ya wenzao. Tabia hii ni ya kawaida kwenye barabara zetu nyingi.

Dereva wa basi ataliendesha basi lake kwa “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” ili awahi kuchuma. Na mara nyingine basi linaweza kupata ajali.

Barabara nyingi hazina maafisa wa trafiki. Na kama wapo wengi wanahongwa; na wananyamaza, kana kwamba mambo yote ni sawia. Lakini ukificha maradhi, kifo kitakuumbua.

Wamiliki wa magari na madereva wamewaweka wakuu wa trafiki wa wilaya na mikoa mikononi. Hata kama afisa wa trafiki mdogo akimkamata mhalifu, kesi yake itafutwa na “wakubwa”.

Barabara: Ripoti hiyo hiyo inaelezea kuwa ajali asili mia 7 husababishwa na matatizo ya barabara.

Napenda kuongezea kuwa barabara zetu ndo hivyo tena; zilitengenezwa wakati magari yalikuwa ni ya serikali au machache kwa ajili ya abiria.

Ieleweke wazi kuwa hakuna uwiano wa moja kwa moja kati ya barabara nzuri na kupungua kwa ajali.
Huko Ulaya kufika mwaka 1648, barabara zake nyingi zilizokitengenezwa tangu enzi za Warumi zilikarabatiwa kukabili mapinduzi ya viwandani yaliyoleta magari ya kukokotwa na farasi hadi mwingilio wa magari ya sasa.

Huko Ulaya, Ujerumani wakati wa Hitler ikawa ya kwanza kuwa na “autobahns” “highways”) kukidhi mahitaji wa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo na endapo kutatokea vita.

Nchi nyingi za Ulaya/Amerika na zingine zilizoendelea zina barabara nzuri na pana. Nitatoa mfano mdogo wa hapa Amerika:

New Jersey Turnpike (Highway) ipitayo karibu na Newark Liberty International Airport ina barabara zenye safu (lanes) sita za kwenda upande mmoja. Kwahiyo barabara kuu hiyo ni kama ina barabara 12. “Highways” nyingi zina safu 3.

Kwa kuwa Amerika inaendeshea mkono wa kushoto, safu ya upande wa kushoto ni kwa wale wenye kutaka kwenda kasi bila ku- “exit”. Safu ya katikati ni kwa wale wenye kuendesha mwendo wa kawaida. Na safu ya upande wa kulia ni kwa wale wenye kutaka ku-“exit”.

Pamoja na “administration and management” ya uedeshaji wa namna hiyo, kuna matrafiki wakali wa mikoa (State Troopers) wanaolinda sheria za barabarani. Wengine hufanya kazi zao wazi wazi.

Endapo msafara wa magari unakwenda kwa kasi, gari la trafiki hao litatangulia mbele na kwenda spidi inayotakiwa. Hakuna dereva atakayethubutu kuli-“overtake”!

Kuna wakati madereva iliwabidi kuwasiliana kwa njia ya "Citizen Band - CB" ili kujiepusha na "State Troopers".

Wakati mwingine matrafiki hao hujificha vichakani kando ya marabara na kuwalopoa (kwa njia ya rada) wale wenye ku-“overspeed”, na wakati mwingine kufanya ukaguzi wa ghafula wa gari.

Magari ya kubeba shehena (“rigs” au “long distance trucking or haulage”) haya yana sheria zake kali. Kila dereva ni lazima abebe utambulisho wa kile alichobeba, kinatoka na kwenda wapi, ameanza kuendesha saa ngapi, na amepumzika kwa kiasi gani. Gari lake pia ni lazima lionyeshe ukaguzi uliofanyika.

Na katika mabarabara ya mikoa mingi kuna “weighing stations” za kupima magari hayo yamebeba shehena ya uzito gani, pamoja na kuchunguza mambo mengine muhimu ya ki-trafiki.

Dereva mwenye hatia, hutozwa faini pamoja na kupoteza pointi fulani kutoka kwa leseni yake, hadi kiasi cha kutoruhusiwa kuendesha.

Gari: Ripoti hiyo niliyotaja hapo juu inaeleza kwa ajali asili mia 1 husababishwa na gari lenyewe.
Napenda kuongezea kuwa baadhi yetu wanaweza kusema gari haliui; anayeua ni dereva, sawa na kusema kuwa bunduki haiui; anayeua ni mwanadamu.

Gari halina budi kuwa katika hali nzuri ya kuendeshwa. Matairi yawe katika hali nzuri na kiasi cha upepo uliojazwa, na viungo vingine muhimu vya gari vichunguzwe mara kwa mara kuona na kuhakikisha kuwa havina kasoro. Gari ni lazima lifanyiwe “servicing”.

Kuna ka-tabia ka kupenda kutunza pesa kwa madai kwamba gari bado linakwenda. Wamiliki hawapendelei kukarabati magari yao.

Ajali nyingi zinazotokea huwa ni za mabasi mapya. Hii haina maana kuwa basi jipya halipati ajali.

Mengine huanguka kwa sababu ya spidi (ku-“overtake”) na kujaza abiria na shehena (overload).

Mara nyingi mabasi ya namna hiyo hushindwa ku-“balance” kutokana na mshituko wa kona au kwa ghafla kujaribu kukwepa wakati wa ku-“overtake”.

Nchini Amerika ni Jimbo la Connecticut peke yake lenye 55 m.k.s. (majimbo mengi yanaendesha 60, 65, 70 na 75 m.k.s.). Lakini takwimu za spidi na ajali hazikubaliani. Hakuna uwiano kati ya spidi kali na kutokea kwa ajali!

Pengine hii ni kwa sababu ya huduma za haraka za ambulance na hospitali katika kunusuru waliojeruhiwa. Kukosekana kwa huduma za namna hiyo nchini Tanzania kunawafanya waliojeruhiwa kutokwa damu sana. Lakini hapa Amerika endapo itatokea ajali, basi magari huwa yanavaana nyuma kwa nyuma.

Kumekuwepo na ajali nyingi za mashangigi nchini mwetu. Lakini hatuna utafiti yakini wa kuonyesha au kuelezea ni mashangigi ya aina gani au modeli gani, ua magurudumu ya aina gain hupasuka pasuka na kusababaisha ajali.

Wakati mwingine, gari au matairi yake huwa vina hitilafu ambazo madereva wengi hawazifahamu!

Ajali nyingine hapa Amerika zimesababishwa na hililafu, kama nilivyoelezea hapo juu. Ikibainika kuwa aina au modeli fulani ya magari au matairi ndio yenye makosa, basi aina au modeli au matairi hayo yatarejeshwa viwandani.

Je, Tanzania itahakikishaje kuwa hitilafu kama hizo, na makosa mengineyo yanadhibitiwa?

Yasemekana Tanzania yetu ni maskini haiwezi kutengeneza barabara kama za Ulaya/Amerika au kuwa na teknolojia ya kisasa ya kudhibiti nidhamu ya uendeshaji na upakizi.

Nakubalina na hilo hapo juu.
Lakini kuna mengi ya kufanya kudhibiti ajali barabarani.

Mabasi kutoka na kurudi Mwanza/Dar yanayopitia nchi ya jirani ingefaa yawe na madereva wanne. Mmoja kati ya Dar na Arusha (apumzikie Arusha); Arusha na Nairobi (apumzikie Nbi); Nairobi na Tarime (apumzikie Tarime); na Tarime na Mwanza (apumzikie Mwanza). Kila dereva aweze kuendesha kwa muda wa kati ya masaa manane na masaa kumi hivi.

Mabasi yanayokwenda Lubumbashi (Kongo-Kinshasa) nayo yadhibitiwe kikamilifu: Dar hadi Iringa; Iringa hadi Tunduma; Tunduma hadi Kitwe. Kitwe hadi Lubumbashi.

Kuhusu madereva, sioni sababu kwa nini kusiwe na matrafiki wa tarafa au wilaya. Hawa matrafiki wetu waheshimike na wapokezane zamu toka tarafa hadi tarafa au toka wilaya hadi wilaya.

Na kama madereva watathubutu kuwahonga, watahonga mpaka lini? CID, TAKUKURU. na Usalama wa Taifa viwashughulikie!

Yafaa sana mabasi yawekewe ratiba na yazifuate ili kuzuia hiyo “marathon” ya uchu wa kuchuma pesa.

Tuwape madereva mafunzo bora ya usanii elekevu wao kupitia semina, majopo au mikutano sawa na “refresher courses” za kuzidi kunoa umahiri wa kuendesha.

Pengine haitawezekana kuwakutanisha maderera wetu huko Ngurdoto Hotel au Bagamoyo!
Lakini tunaweza kupitia kwenye restauranti za “Mama Ntilie” ili nao wapate mtaji wa kuendeleza ulishaji mijini kwa walalahoi.

Kwa wale madereva wanaoendesha wakubwa, mara nyingi kumekuwepo na malalmiko ya hao madereva kutopata muda wa kupumzika wawapo safarini.

Badala ya kumwambia dereva aende akapumzike na aje amchukue wakati fulani, dereva huyo analazimika kungojea kwenye gari bosi wake amalize shughuli rasmi au za ubinafsi hadi zaidi ya usiku wa manane! Dereva anaambiwa kuanza safari ndefu asubuhi na mapema, tuseme kurudi Dar es Salaam. Na wakati mwingine madereva hao hata posho hawapati vizuri!

Tatizo la kupakia abiria na shehena nyinginezo zaidi ya kilichoruhusiwa, limesababaisha ajali kwa vyombo vetu vya usafiri si barabarani tu bali pia relini, angani na majini.

Gari la moshi lilishindwa kupanda miinuko na ghafla ku-“reverse” na kurudililipotoka. Ndege zetu nyingine zimeshindwa kuruka shauri ya uzito wa shehena (magunia ya vyakula na matunda). Meli, boti, mashua na mitumbwi yetu imezama shauri ya uchu wa pesa kutokana kujaza sana abiria na shehena.

Umuhimi wa “servicing” uzingatiwe na kuelezeka kwa msemo wa mambo ya uganga, “Wakia moja ya kinga ni bora kuliko tani ya tiba.”

Tanzania si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure. Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ya 60 ni wa nini, kama sio kuzidi kutonesha kidonda cha umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.

Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya umma (serikali) ambayo ilikuwa imetuna, mithili ya mwenye kitambi.

Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!

Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the State) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge (the State) na State ijenga nchi. Kwa kifupi, chama tawala cha siasa ndicho kiliunda State ijenga nchi. Matokeo ya kuota kitambi kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi.

Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya ummana ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo! Ubinafsi tuliouona kwa darubini ya ujamaa kuwa kama dhambi, leo hii ni nyenzo muhimu ya kuleta eti maendeleo!

Tunalipendelea sana Jiji la Dar es Salaam. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake. Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga.

Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.

Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri mjini hapo Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “makao Makuu ya Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka,licha ya kutojua ni mapesa mangapi Mamlaka ya Mji wa Dodoma ilitumia kuwakopesha wafanyakazi wake kujijengea nyumba zao binafsi! Tuache kuhamia Dodoma! TAKUKURU mnayajua hayo!

Itatubidi tuunde utaratibu wetu wenyewe wa madaraka mikoani ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar,ikiwa ni pamoja na watu kusafiri kwendaDar es Salaam kwa ajili ya kununua vitu na huduma.

Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu. Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:

Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.

Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; Sheria (Katiba na Utawala Bora); pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa.

Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.

Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi.

Kigoma: Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki.

Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko). Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama mji wa huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” (Tanzania, Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini). “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake!

Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwamja wa ndege wa kimataifa unaendelea kujengwa mjini Mbeya. Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini.

Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.

Kila fungu litasimamiwa na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na”manifesto” ya “chama tawala” (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa.

Afisa huyo asaidiane na tawala za mikoa. Wakuu wa mikoa na maafisa wao wasaidizi (hadi wilayani) wafanye kazi karibu zaidi ili kufanikisha wajibu wao kwa wananchi.

Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.

Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.

Sambamba na kupunguza wingi wa wizara, juhudi ifanywe pia kupunguza idadi ya wa-Bunge wetu! Wa-Bunge wengine “hulala sana”! Sioni sababu kwa nini kila wilaya isiwe na na m-Bunge mmoja tu wa kuiwakilisha katika Bunge la Taifa, Dodoma!

Shughuli za “wa-Bunge” wa Seriali za Mitaa wapewe hadhi na majukumu makubwa ya kusimamia maendeleo katika sehemu zao za majimbo ya uchaguzi, kulingana ana usemi wa serikali za mitaa wa nchi moja iliyoendelea: “Using local people, with local knowledge to serve the local area”.

Huku tukitilia mkazo wa sera ya “madaraka mikoani” (kama kweli bado inatekelezwa), mikoa yetu haina budi kushiriki zaidi katika kupanga na kutekeleza hayo ya “maisha bora kwa kila m-Tanzania”, ikiwa ni pamoja na kudhibiti athari za ajali barabarani.

Naamini Tanzania si masikini; ni tajiri! Fikiria leo hii tunajivuna kuwa tu nchi ya tatu katika Bara la Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu!

Michanga ya dhahabu inachimbwa na kusafirishwa nchi za nje. Makapuni ya kigeni kwa muda wa miaka mitatu ya kuvuna dhahabu yetu bila kulipa kodi.

Yanaweza kuichimba usiku na mchana kabla ya miaka hiyo mitatu kuisha. Miaka mitatu iishapo, ili yaanze kulipa kodi, aidha yanaweza kulalamika kuwa yatafunga migodi kutokana na uhaba au ugumu wa kuchimba dhahabu yenyewe.

Au wakati mwingine makampuni hao yanatishiwa na wakubwa wenye kutaka kuila Tanzania kwa kuyalazimisha kuwahonga ili waidhinishe mikataba hiyo na kuanza kulipa kodi. Hii inayafanya makampuni hayo kuuza “business” kwa wamiliki wengine wa kigeni au kuunda kampuni mpya yenye jina tofauti!

Tatizo hili lipo pia katika mikataba ya gesi yetu. Utajiri wa madini na gesi yetu umeingiliwa na unyarubanja unaotekelezwa na wawekezaji wa kigeni Makampuni hayo yamepewa dhahabu ya bure.

Mikataba tunatiliana na hao wawekezaji wageni ikiwa na kipengere cha “production sharing agreement”, psa (kugawana uzalishaji).

Lakini inaonekana kuwa wanaonufaika na kipengere hiki ni wawekezaji, ambao kila mra huongeza vikampuni vingine vya kigeni vidogo vidogo na kunufaika.

Je, huo si “unyarubanja”?

Hakuna hata kikampuni cha wazawa kinachonufaika na kipengere hicho, kama ilivyo katika mikataba ya madini na gesi yetu. Labda, Tanzania iko pembeni mwa kipengere hicho!

Tangu mkataba wa kwanza kusainiwa (na pengine mpaka sasa hivi) kuna kutafuta “production sharing agreement”, psa (kugawana uzalishaji). Si ajabu mzozo wa Buzwangi umetokana na “production sharing agreement”, kama ilivyo mikataba mingi ya madini na gesi yetu!

Ukifungua http://www.globeinvestor.com/servlet/story/RTGAM.20071030.wbarrick1030/GIStory/ utapata ripoti ya mgomo unaoendelea huko kwenye Mgodi wa Barrick. Mwisho wa stori hii kuna para moja juu ya vile walivyovuna mwaka uliopita:

“The mine, which Barrick acquired in 1999, produced 330,000 ounces of gold last year at a total cash cost of $339 (U.S.) an ounce. It had proven and probable reserves of 11.2 million ounces as of the end of last year.”

Sijui kama wameanza kulipa kodi au kutupatia 3% (royalities) zetu? Hata kama wakitupa kiasi hicho, Tanzania itapata dola ngapi? Fanya hesabu!

Mwisho, naipongeza serikali kwa juhudi zake za kuwapa msasa kidogo madereva. Lakini hii haitoshi kabisa. Naomba juhudi hii isiwe ndani ya majengo tu bali huko nje barabarani ambako ajali hutokea.

Matrafiki wafanye hiyo kwa maadili ya hali ya juu (mithili ya madaktari na wahubiri dini) ili kuokoa maisha na mali ya wa-Tanzania.

Hivi karibuni tulizawadishwa na serikali ya Amerika (kupitia mfuko wa Rais wa Millennium Challenge Corporation - MCC) ya zawadi (“grant”) ya dola 698 milioni kuboresha mabarabara nishati na maji nchini kwa kipindi cha miaka mitano.

Pili, kulikuwa na habari kutoka Makao Makuu ya African Development Bank mjini Tunis kuwa Benki hiyo imetoa kiasi cha dola za ki-Marekani million 92 (72%) (serikali ya Tanzania itagharimia 28%) kwa ajili ya kutengeneza mabarabara ya mikoa ya Dodoma na Singida ili kuuunganisha mikoa na mikoa ya kasikazini hadi Kenya.

Je, ki-mapatano, mapesa hayo yatatumikaje katika kudhibiti baadhi ya mienendo mibaya yetu inayosababisha ajali barabarani?

25 October 2007

Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Amefariki dunia.


Ilikuwa jana jioni majira ya saa kumi na moja na nusu jioni ambapo mama yetu mpendwa waziri Salome Joseph Mbatia alikutwa na mauti akiwa kazini. Watanzania tumeipokea habari hii kwa masikitiko makubwa kwani mara nyingi ajali hizi zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva na serikali kutokuwa wakali na makini katika sheria za barabarani. Kwa mara nyingine tena tunaiomba serikali iache kuzembea katika suala hili la matumizi ya barabara. Kwa habari zaidi Soma hapa.



Pichani juu ni ajali yenyewe ilivyokuwa.Mungu amlaze mahali pema Amina.

Picha kwa hisani ya Haki Ngowi

21 October 2007

Sanaa hii ni ya nani?



Unajua mara nyingi mtu au kitu hutambulika kutokana na mtindo wake, Leo nina swali juu ya picha hapo juu, Je sanaa au michoro ya jinsi hiyo ni ya Msanii gani Tanzania?

01 October 2007

Malkia Nzinga Mbande wa Angola.


Nikiwa katika harakati ya kukusanya habari za wanawake waliotia fora duniani, nimeona niirudishe habari hii niliyoiandika hapo nyuma 2005 wakati nikianza kublogu hii ni kuwapa fursa wale ambao hawakuweza kuisoma nao wapate kumfahamu mama huyu, haya endelea...

Kama ukibahatika sasa hivi kukutana na Mreno, wewe jifanye kama unamchokoza juu ya wanawake wa afrika kwamba hawana lolote na hawawezi lolote, uone atakavyokushangaa, na bila shaka atakutupia swali kwamba unaishi dunia gani wewe?

Wasomaji msishangae, kwani aisifiae mvua...imemnyea. Hii yote imetokana na mwanamke mmoja jasiri, shupavu, mwenye akili sana na asiyetaka kuonewa wala kudharauliwa, si mwingine ni Malkia Nzinga Mbande. Mwanamama huyu aliyezaliwa mwaka 1583 na kufa 1663, alikuwa ni mtoto wa chifu na aliishi kipindi ambacho biashara ya utumwa ndio ilikuwa imepamba moto kwelikweli, kwa bahati mbaya baba yake alifariki na hivyo kaka yake mkubwa bwana Ngola Ngoli Mbandi akarithishwa madaraka ya baba yake. Mm! kaka huyu bila shaka aliguna kwa kujua kabisa kasheshe analotakiwa alikabili la kuwazuia wareno kuingia nchini kwao, lakini afanyeje na yeye ndio mwanaume na kama inavyojulikana kwa wengi mwanaume anaweza kila kitu na daima si mwoga, ikabidi ayavae madaraka huku akijua kabisa yeye ubavu wa kukabiliana na wareno hana na ni
mwoga kufa.

Dada yake, Nzinga baada ya kuona kaka yake anasua-sua ikabidi amwambie, kaka ni lazima uchukue hatua juu watu hawa na kuwazuia kuingia kututawala, lakini kwa vile kaka yake alikuwa mwoga ikabidi amwombe dada yake amsaidie, mara moja bila kuchelewa mwana mama Nzinga akaanza kuchukua hatua za utekelezaji na akafanikiwa kuwashawishi wareno katika kuandika mkataba wa makubaliano ya amani.

Tarehe ikapangwa ya kuweka saini makubaliano hayo, Kaka mtu kwa woga akakataa kwenda hivyo ikabidi Nzinga amwakilishe, akaenda na watumishi kadhaa lakini walipofika ndani ya ukumbi Nzinga akagundua kwamba hakuwekewa kiti yeye kama kiongozi wa nchi yake isipokuwa gavana wakireno peke yake, mwanamama akaona dharau gani hii? mara moja akapiga kofi na mmoja wa watumishi wake akaja mbele yake na kuinama magoti na mikono chini, Nzinga akakaa juu yake, kwa hiyo suala la gavana kukaa kwenye kiti peke yake likawa ngoma droo. Gavana akamtizama yule mama bila kummaliza na kubaki na aibu ya kuzidiwa maarifa tena na mwanamke, bila shaka alibaki akijiambia duh! kumbe wanawake nao wamo!!!

Nzinga baada ya kugundua kwamba kaka yake si kiongozi mzuri na hawezi kila kitu, alimfunga na kujitangaza kwamba yeye ndiye atakayeshika nchi kinyume na desturi ya nchi yao kwamba mwanamke haruhusiwi kushika wadhifa wowote wa uongozi katika serikali, minong'ono ya hapa na pale ilitokea lakini haikufika mbali kwani Nzinga alithibitisha ujasiri wake kwa vitendo. Na ni hapo ndipo umalkia wake ulipoanzia.

Kwa muda wa miaka arobaini ya uongozi wake, wareno walishindwa kuitwaa Angola hadi alipofariki, mwanamama huyu alijulikana na kuogopwa sana na ulaya nzima kwa mbinu zake thabiti za kijeshi, alijulikana kama mwanamke mpiganaji, jasiri na mwenye akili.
Hebu fikiria wareno, pamoja na kuwa na silaha imara na za kisasa ukilinganisha na za Malkia Nzinga, lakini walishindwa kuiteka Angola hadi Malkia Nzinga alipokufa.

Huyu kweli ni mwanamke wa shoka, na nina amini kila mwanamke anaweza kuwa mwanamke wa shoka, pale atakapoamua kufanya jambo kwa moyo na kuondoa uwoga. Hapa duniani kila jambo linawezekana, tatizo liko kwetu sisi wenyewe kutanguliza woga na kutokutaka kusumbuka.

27 September 2007

Babu Kaduma amefariki dunia.


Babu Kaduma kama wengi tulivyozoea kumwita, hatuko naye tena duniani. Kifo chake kimetokea leo mchana katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa. Tutamkumbuka sana kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika sanaa za maonyesho nchini na nje ya nchi. Mungu amlaze pema Amina.

24 September 2007

Tunaomba mawazo yako.

Wadau, tukiwa katikati kabisa mwa shughuli yetu ya kuunda Jumuiya ya blogu za Tanzania, sasa katiba ya mwanzo au tuseme ya awali imetoka, tunachokuomba ndugu msomaji ni kwamba ipitie uisome kwa makini halafu toa maoni yako juu ya kuibooresha zaidi. Jumuiya yetu inaamini kwamba kidole kimoja hakivunji chawa na ndiyo sababu tukaona haitoshi kwa viongozi peke yake kumaliza kila kitu katika kutengeneza katiba hii, tunaomba sana tena sana tusaidiane katika hili. Karibuni sana, bonyeza hapa uchangie.

Nimerudi..


Sekunde, dakika, masaa, siku na sasa miezi kadhaa imepita tangu da'Mija nitoweke ghafla mtandaoni. Mambo mengi yamepita hapo katikati yaliyonifanya nishindwe kuonekana kama ilivyo kawaida yangu, lakini hata hivyo nashukuru Mungu ameniwezesha kurudi salama salimini kwa wadau wangu.

Naomba nichukuwe nafasi hii kuwashukuruni sana kwa hongera na heri mlizonitakia katika maisha yangu mapya ya familia, Mungu awabariki sana.

Nimerudi jamani

13 July 2007

Nyapara na Manamba.. waraka toka kwa Tungaraza MtiMkubwa.

Siku moja nilipata kuangalia filamu ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Marehemu Kapteni Jean Baptist Bokassa. Baada ya kuitazama ile filamu nikashikwa na tafakuri juu ya tabia za binadamu hususani pale wanapokuwa na madaraka.

Jambo moja nililolibaini katika tafakuri yangu ni kwamba wanaadamu wengi wanapenda madaraka. Zaidi ya hivyo madaraka yanaweza kulevya vibaya kuliko pombe kali au bangi. Watu hupata madaraka ama kwa kuzaliwa kwenye koo iliyopo madarakani mathalani wafalme, malkia, masultani na watemi, au kwa taaluma, au kwa kuteuliwa, au kupigiwa kura, au kwa kujipachika, au kwa kunyang'anya, au kwa mizengwe.

Ili kujikweza kimadaraka watu hunakshi nomino zao na badala ya kuitwa majina yao huwa wanaitwa Mtukufu Rais, Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Spika, Waziri, Naibu, Katibu, Mkuu, Mzee, Baba wa Taifa, Ofisa, Dokta, Profesa, Mtakatifu, Mchungaji, Askofu, Muinjilisti, Kateksiti, Maalim, Alhaji, Shehe, Imam, Walii, Maulana, Ayatollah, Chifu, CEO, Mheshimiwa Balozi, Jenero, Afande, Kamanda, Mtaalam, Bwana, Bibi, na kadhalika.

Madaraka humpa mtu uwezo wa kuelekeza muelekeo wa tabia za wale anaowaongoza hali kadhalika mfumo, utaratibu, na muundo wa taasisi anayoiongoza. Madaraka yanaweza kujenga, kubomoa, au kuharibu tabia ya mtu au taasisi. Mifano ya taasisi na watu waliojengwa, kubomolewa au kuhitilafiwa tabia kwa sababu ya madaraka ni mingi sana. Pia madaraka huweza kutukuza au kudhalilisha. Wapo watu kwa sababu ya umakini wao katika madaraka nomino zao zilinakshiwa Utakatifu na wale waliopotosha madaraka yao walinakshiwa Udikiteta au Fashisti.

Madaraka hujenga tabaka la viongozi na maamuma. Mfano wa haya makundi ya viongozi na maamuma ni kama yale wahubiri na waumini, wanasiasa na wananchi, viongozi na wafanyakazi, afande na kuruta, na kadhalika. Kuna wakati utawasikia wale walio madarakani wakisema "..Watu wangu wako wapi?.." "..Vijana wangu wanahitaji..." ...Watu wangu tuliwaahidi kuwajengea zahanati.." na kadhalika.

Wiki kadhaa zilizopita niliandika kuhusu muelekeo wa Mheshimiwa Spika na Naibu wake na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Tanzania la sasa. Ukifuatilia utaratibu wa hoja, maswali, na majibu bungeni hutasita kukubaliwa kuwa bunge letu limekuwa kama la Nyapara na Manamba. Mfano mmoja huo hapo chini:


Spika azuia maswali ya afya magerezani

Basil Msongo, Dodoma
HabariLeo; Thursday,July 12, 2007 @00:04
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta jana alizua gumzo bungeni baada ya kuzuia Wizara ya Mambo ya Ndani isijibu maswali matatu ya nyongeza kuhusu hali ya afya magerezani ikiwamo Ukimwi na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Alitoa uamuzi huo wakati Naibu Waziri, Lawrance Masha akijiandaa kuyajibu baada ya kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA) aliyetaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha Ukimwi hausambai magerezani hasa kwa watoto waliochanganywa na watu wazima kutokana na uhaba wa jela za watoto.

Kabla ya Spika Sitta kuzuia majibu ya nyongeza, Masha alisema si kweli kuwa wafungwa wanaandamwa na maradhi ya kuambukiza magerezani ukiwamo Ukimwi. Akiuliza swali la nyongeza, Mhonga alimuuliza Naibu Waziri endapo atakuwa tayari kubadili kauli hiyo endapo mbunge huyo atampatia ushahidi kuthibitisha kukithiri kwa magonjwa ya kuambukiza magerezani ukiwamo Ukimwi.

Mbunge huyo pia aliuliza ni bajeti kiasi gani imetengwa kukabiliana na Ukimwi magerezani. Hapo Spika akaamuru swali hilo lisijibiwe. Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema) alisema, taarifa ya Tume ya Jaji Kissanga ilibainisha kuwapo kwa tatizo hilo katika magereza takriban yote nchini hivyo akaitaka wizara hiyo ieleze endapo taarifa ya tume hiyo si sahihi.

Spika aliamuru pia swali hilo lisijibiwe hali iliyozua gumzo miongoni mwa wabunge hasa wa kambi ya upinzani. Kabla ya uamuzi wa Spika, Masha aliliambia Bunge kuwa serikali imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa Ukimwi hausambai magerezani ikiwa ni pamoja na kuzuia aina yoyote ya ngono magerezani na kuwatenga wafungwa na mahabusu wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa Masha, watoto wanatengwa na watu wazima magerezani ingawa Mbunge Mhonga alisema kuna jela tatu tu za watoto nchini, na moja ya vijana. Alisema viwango vya maradhi magerezani si tofauti na katika jamii kwa kuwa katika kila gereza kuna huduma ya tiba kwa ajili ya wafungwa.

Ili kudhibiti magonjwa ya kuambukiza magerezani, askari kusimamia kazi ya kuwanyoa wafungwa na kutaja vifaa vinavyotumika kuwa ni mikasi, nyembe, brashi, mafuta maalumu ya kunyolea na sabuni.

03 July 2007

ASANTENI KWA KURA ZENU.

ASANTENI SANA.

Born Again Pagan anayo haya machache kwa Marehemu Amina Chifupa

Nikiwa mmojawapo wa wanaume Watanzania wapendao kutekeleza na kudumisha mwito wa "kuwawezesha wakina mama na usawa wa jinsia" ("womenn empowerment and gender equality"), napenda sana kutundika katika blog ya "mwanamke wa shoka" katika kumkumbuka Mama Mtanzania, Mbunge, ambaye ametuacha hivi karibuni, kwa shahiri lifuatalo:

Amina Chifupa, Hadithi Yako Itabaki Siku Zote!
Copyright: Born Again Pagan, New York, 2007

Mawinguni yako sauti
Ilitapakaa ki-FM shuti
Kuwatia vijana na watoto buti
Hadithi yako itabaki siku zote!

Ulitekenya fikra za vijana
Kuzipanua bila kubana
Kukubali kushindwa hapana
Hadithi yako itabaki siku zote!

Amina Chifupa ukaingia ndoa
Kwa Mpanganjila bila doa
Wazushi macho kukodoa
Hadithi yako itabaki siku zote!

Amina Chifupa kama dua
Bungeni ulitua
Hoja ya nguvu kutozua
Hadithi yako itabaki siku zote!

Dhidi vilevya jitihada yako
Imehamasisha mapambano
Yaendelea hayo mapambano
Hadithi yako itabaki siku zote!

Wengine vibaya walikuandika
Bloguni nyingi kukubandika
Kwa fimbo kukutandika
Hadithi yako itabaki siku zote!

Kiafya kunyauka kuja
Ukaondoka Dodoma - Lugalo kuja
Hukuachia kutoa hoja
Hadithi yako itabaki siku zote!

Kero wizi wa mitihani
Hukuachia ingawa kitandani
Kupitia kwa swaibu hadi Dodomani
Hadithi yako itabaki siku zote!

Hatujui pengine ulielezeka
Ugonjwa wako kutoelezeka
Kwa wasio karibu kuuweka
Hadithi yako itabaki siku zote!

Siyaoni sasa mabaya yakiandikwa
Na fimbo za udaku kutandikwa
Mazuri tu hubandikwa
Hadithi yako itabaki siku zote!

Kama vyako vilemba
Mazuri yanalemba
Kutoka kila upande kupamba
Hadithi yako itabaki siku zote!

Kama yako mavazi
Mabaya si mema malazi
Pumzika kama bora malezi
Hadithi yako itabaki siku zote!

Mlimbwende Amina Chifupa
Umevunja yetu mifupa
Kutuachia tupu chupa
Hadithi yako itabaki siku zote!

Umetuacha bumbuwazi
Lango kubwa wazi
Kuingia hata udaku-mainzi
Hadithi yako itabaki siku zote!

Maneno ya udaku mzito
Yamekuwa ujauzito
Kuzaa zaidi udaku mzito
Hadithi yako itabaki siku zote!

Amina Chifupa wa Baba
Amina Chifupa wa Mama
Mbunge mpendwa wa Tanzania
Hadithi yako itabaki siku zote!

29 June 2007

Usisahau kupiga kura. 29 na 30 June 2007.

Wasomaji wangu ingawa bado tuko katika majonzi mazito ya kuondokewa na kipenzi chetu, lakini tusisahau upigaji kura unaendelea hapa. Swali je umeshapiga kura??

26 June 2007

Katutoka kama mchezo...


Bado siamini kama Mbunge Amina katutoka. Lakini yote tunamuachia Mungu, tunaomba Mungu ailaze roho yake mahali pema, Amina.

20 June 2007

Fide ajisemea.." ..Ukishindwa kukasirika cheka..

Jumamosi iliyopita Watanzania tuligubikwa furaha baada ya timu yetu ya taifa kuifunga timu ya taifa ya Burkina Faso goli 1-0. Nderemo, vifijo, na halahala nyingine za furaha ya ushindi wa Taifa Stars ziliashiriwa kwa namna anuai mojawapo ikiwa ni ya uzuru wa wachezaji wa Taifa Stars bungeni mjini Dodoma.

Katika uzuru huo wa Taifa Stars bungeni Dodoma jumla ya shilingi milion 322.5 zilichangwa kama bahashishi ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars. Miongoni mwa wachangiaji walikuwemo Wananchi, Wapenzi wa soka, Vigogo = Waheshimiwa Wabunge na Mawaziri, Wafanyabiashara, pamoja na Wizara mbali mbali.

Moyo huu wa 'harambee' pengine unaweza kukuchekesha au kukukasirisha. Kama UKISHINDWA KUKASIRIKA CHEKA:

The ‘harambee’ continued during luncheon at which Infrastructure Development Minister Andrew Chenge said his ministry and institutions under it were topping up their earlier pledge (70m/-) by 30m/-.
Other pledges were made by Industries and Trade Minister (30m/-), Labour, Employment and Youth Minister John Chiligati (10m/-) while Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi pledged 15m/-. He also pledged a further 15m/- from his personal companies.
Singida Urban MP Mohammed Dewji gave 30m/- while the proprietor of TIOT Company pledged 10m/-. Dodoma residents contributed 25m/- on the spot at the airport. Team captain Shadrack Nsajigwa received the money from the prime minister on behalf of his colleagues
.

Kwa habari kamili gonga hapa.

13 May 2007

Nani kama mama?

Leo ni siku ya mama, tusaidiane kumsikiliza mzee Nico Mbarga halafu utaniambia mwenyewe.

07 May 2007

Bongo Niu Yoki...

Habari hii chini inaletwa na mwanaharakati MtiMkubwa...haya endelea.


Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, Maubungo Plaza, Mayfair Plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile la Kibiti watasha wenyewe wanabloo! Na neshino stediumu mpya ikiisha litakuwa hamna tena Afrika nzima!

Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi! Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Maselebriti wa vipaji vya kitaaluma, kisanii, kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!

Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama wakati tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio la Arusha kwa kuwa bepari au kabaila kwa sababu ya kumiliki tivii! Eee bwana na magari mengine hata ughaibuni hamna sijui mabaluni, maviieksi, Mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!

Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli na yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa inteki, yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!

Siku hizi simu siyo big dili! Unaambiwa nilikuwa Nanjumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea na sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za TTCL ilikuwa uende kibanda cha simu tena ukikikuta nzima una bahati sivyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi teksi meseji au ukiona namna gani vipi unanda intaneti unatuma imeli!

Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua bomba gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu!

Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Siulimuona nanihii, alipoondoka kwenda ughaibuni alikuwa na mimba hiyoo mashavu utafikiri anapuliza moto! Karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete zako. Kuna majamaa hapa Bongo wanaishi kama mtoni asubuhi wanapata brekifasti ya masoseji, hambagi, juisi na chai ya maziwa matupu au uji uliopikwa na unga wa keki ukatiwa na mapande ya siagi na krimu! Lanchi chikeni chipsi na kuku, dina steki hevi grili pateto au raisi! Yaani wee acha tu, Bongo New York.

Na manjagu wanakula mavitu hevi siyo kama enzi za Mahita tangu kaja Said Mwema manjagu wanatia vitu vya kimtoni maksi sijui mabelti, yaani we acha tu!

25 March 2007

Sijui wewe? ....MtiMkubwa auliza.

Kuna jambo ukiliona unaanza kulitilia maanani na kulitafakari, jingine unaliona ajizi na kulipuuza, jingine unalistaajabia, jingine linakutia tabasamu, jingine linakutia hasira na kukukasirisha, jingine linakuchekesha unaanza kucheka. Miye jambo hilo hapo chini limenichekesha! Sijui wewe?



::Habari za Tanzania Ijumaa Mar 23, 2007

Shekhe jino kwa jino na Mchungaji kuhusu Dito

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Kamati ya Maimamu ya Kuokoa Mali za Waislamu Tanzania Shekhe Khalifa Khamis, amemjia juu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akimtaka aache kuingilia masuala ya mahakama katika kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Ditopile Mzuzuri.

Sheikh Khalifa alitsema hayo jana kutokana na kauli za hivi karibuni za Mchingaji Mtikila ambazo amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akieleza kupinga hatua ya Bw. Ditopile kufunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia na kutaka afunguliwe ya mauaji ya kukusudia.

"Tunashangazwa sana na kauli hizi za Mtikila, akiwa kiongozi wa kisiasa. Katika Uislamu, sheria inasema mtu yeyote anayetuhumiwa kuua iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ni lazima ashitakiwe. Ditopile ameshitakiwa basi tuiachie mahakama.


"Kauli za Mtikila kuwa mashitaka aliyopaswa kufunguliwa Bw. Ditopile ni ya mauaji ya kukusudia hazina msingi, kwa sababu yeye hana nguvu wala dhamana ya kuingilia utaratibu wa mashitaka na mwenendo wa mahakama," alisema.

Akifafanua zaidi suala hilo, Shekhe Khalifa alisema watu wote wanaomfahamu Bw. Ditopile wanaujua unyenyekevu wake na namna alivyokuwa kipenzi cha watu.

"Ditopile si jambazi na wala si mtu katili, wanaomfahamu tangu akiwa mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Lindi, Pwani na Tabora, wanamjua jinsi alivyo mtu mwenye bashasha na mkarimu. Kilichomtokea ni dhahiri halikuwa jambo la kukusudia," alitetea Shekhe Khalifa.

Alimtaka Mtikila aache kuingilia masuala yasiyomhusu na kuhoji uanaharakati wa mwanasiasa huyo katika matukio mengine.

"Hivi karibuni kesi ilitokea Songea. Kuna kijana alikutwa na meno ya tembo akafungwa miaka minane. Padri akakutwa na kosa kama hilo akafungwa dakika 45 tu. Mbona Mtikila hakukata rufa
Habari Zinazoshabihiana
• Mufti avunja uongozi BAKWATA 16.02.2007.
• Kesi ya Dito sasa yaingia msikitini 21.03.2007.
• Shekhe, wafuasi 15 mbaroni kwa kuzuia mazishi 04.01.2007.

20 March 2007

"Kusi na Kaskazini"...... Busara toka kwa MtiMkubwa.

Watu wa pwani wakifikwa na jambo kama misiba ya mfululizo, mfumuko wa maradhi, uzazi wa mfululizo na kadhalika ulisawirisha jambo hilo na msimu wa hali ya hewa ya wakati huo linapotokea jambo. Kwa mfano, utawasikia wazee wa Kiswahili wakisema "..Kaskazi na joto..Maanake limekuwa joto kama tunafanya masaili ya kuingia jehanamu.." Kaskazi ni msimu ulio kati ya mwezi kumi na mbili (Desemba) na mwezi wa tatu (Machi). Kipindi hiki maeneo ya pwani ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja, Pemba, na Mombasa huwa na joto kali sana na kadri unavyoenda kaskazini joto hilo huzidi!

Kusi ni msimu unaoanza mwezi wa tano (Mei) hadi Mwezi wa kumi (Oktoba). Miezi hii kwa kawaida ni miezi ya mavuno na biashara ya mazao ya misimu shambani. Kipindi hiki utawasikia wazee wa Kiswahili wakisema "..Kusi akiisha bila matamasha siyo kusi.." Kwa kuwa wakulima wanakuwa wanauza mazao yao basi ndiyo kipindi cha kuwatoa jandoni vijana wa kiume na kuwanema wanawali, hali kadhalika kufunga ndoa kwa wachumba wapya na wale wenye kufunga za mitaala. Kipindi hiki hali ya hewa huwa siyo ya joto. La hasha siwezi kusema kwamba huwa ni baridi aidha.

Zama za kale pepo za kusi na kaskazi zilikuwa zikitumiwa na wafanyabiashara. Madau yaliyosheheni bidhaa mbali mbali toka Uarabuni hususani yale ya Washihiri toka Hadhramauti (Yemen), madau ya Wahindi na mengine toka Uajemi yalikuwa yanakuja msimu wa Kaskazi na kutia nanga kwenye bandari za Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Bagamoyo, Saadani, Tanga, Kilwa, Mafia na Mtwara. Kusi ikianza madau hayo yalikuwa yanaondoka na bidhaa mbali mbali toka kwetu na kuzipeleka nchi za mbali kuziuza. Hadi leo hii ukiwa Dar es Salaam, Bagamoyo, Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Kilwa na Mtwara bado unaweza kuyaona madau lakini siku hizi si mengi yanayotoka nchi mbali zaidi ya Visiwa vya Komoro na Kenya.

Kusi na Kaskazi ya miaka karibuni imekuja na mageuzi ya itikadi za kisiasa za nchi nyingi za Ulaya. Februari 2005 huko Denmark wanasiasa vijana wa vyama vya The Danish people have voted to keep the current centre-right political coalition of the Venstre (The Liberal Party), Det Konservative Folkeparti (Conservative People's Party) na Dansk Folkeparti (Danish People's Party) wenye kufuata itikadi za mrengo kulia walinyakua uongozi wa kisiasa toka kwa wanasiasa wazee wa itikadi za mrengo wa kushoto. Nayo kusi ya mwezi Septemba 2006 ikakileta chama cha Moderate madarakani nchini Sweden na kuwaangusha Social democrates baada ya kuwa usukanini kwa miaka 12. Jana tarehe 19 Machi, nchini Finland vyama vya mrengo wa kulia vya Centre na Conservative vimechukuwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa wabunge hivyo kutakiwa kuunda serikali mpya ya mseto yenye itikadi za mrengo wa kulia.

Azma ya insha hii ni kutaka tukumbuke kwamba zile zama za kukinga mkono SIDA, DANIDA, na FINIDA ndiyo zinagota. Tukipanda ndege kuja kaskazini tuje na mikataba ya biashara tusije na mabakuli yetu ya michango au makabrasha ya ombaomba. Jinginewe, ningekuwa karibu na viongozi wetu ningewashauri wakae na kutafakari upya mahusiano na wanordic kwa sababu kusi na kaskazi zimewasogeza kwingine hawapo tena kule kwa mwanzo kwa wafadhili/wahisani na wafadhiliwa/wahisaniwa!

16 March 2007

Miriam Makeba

Miriam Makeba ni mwanamuziki mashuhuri sana na mwanaharakati kutoka Afrika kusini. Alizaliwa 04-03-1932 Johannesburg. Baba yake Caswell Mpambane Makeba alikuwa ni kabila la xhosa na Mama yake Christina Nomkomendelo Jele alikuwa ni mswazi.

Miriam ni mtoto wa sita na wa mwisho kwa mama yake, na wa kwanza na wa mwisho kwa baba yake. Mama yake aliolewa na Makeba baada ya ndoa yake ya kwanza na bwana Mahlangu kuvunjika wakiwa tayari na watoto watano ambao ni, Joseph, Hilda, Mizpah, Ethel na mmoja aliyefariki akiwa mchanga.

Familia yao ilikuwa ni masikini sana. Baba yake ambaye alikuwa ni mwalimu kitaaluma hakuwa na kazi yoyote, kwani katika kipindi hicho cha utawala wa kikaburu ilikuwa ni ngumu sana kwa mwalimu mwafrika kupata shule ya kufundisha. Mama yake alikuwa anafanya kazi za ndani kwa wazungu na wakati mwingine kuuza pombe ya kienyeji(umqombothi) ili kuihudumia familia. Wakati huo ilikuwa ni kinyume cha sheria kwa mwafrika kunywa au kutengeneza pombe ya aina yoyote ile lakini hata hivyo ilikuwa ikitengenezwa na kunywewa kwa kificho. Kutokana na hali hiyo polisi wa kizungu walikuwa wakivamia mara kwa mara makazi ya waafrika ili kuwakamata wasiotii amri hiyo ya kunywa na kutengeneza pombe. Ilikuwa ni pale Miriam alipofikisha umri wa siku 18 tu tangu azaliwe, polisi walivamia maeneo ya waafrika na kufanikiwa kumkamata mama Miriam akiuza pombe, bila huruma wala kujali kwamba ana mtoto mchanga walimbeba hadi mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela. Hakuwa na jinsi ya kumuacha Miriam, alimbeba Miriamu wake na kwa pamoja kukaa jela kwa miezi sita. Hivyo basi Miriam akiwa katika umri mdogo kabisa aliweza kuionja jela.

Walipotoka Jela walikuta baba (Makeba) amepata kazi katika kituo cha kuuza mafuta cha Shell, hivyo maisha yao yakawa na nafuu. Maisha yaliendelea vizuri hadi mwaka 1938 ambapo Mzee Makeba alifariki dunia, Miriam akiwa na umri wa miaka 6. Taabu ikarudi palepale, na kwa vile kipato cha mama yao hakikuweza kutimiza mahitaji ya watoto wote sita, ikabidi ahamishie watoto wake kijijini kwa bibi yao aliyeitwa MaVilakazi, (huyu ni mama mzazi wa mama yake na Miriam). Na yeye akabaki mjini kwa ajili ya kazi. Miriam anasema kuanzia hapo ilikuwa si rahisi kuonana na mama yake, muda mwingi alikuwa kazini mjini na kwa vile Miriam alikuwa bado ni mdogo na anayehitaji uwepo wa mama yake zaidi, ilibidi awe anafunga safari ya mjini kila mwisho wa juma baada ya masomo kwenda kumuona mama yake aliyekuwa akikaa kwa wazungu aliokuwa akiwafanyia kazi.



Upande wa pili kwa bibi MaVilakazi, familia ilikuwa ni kubwa ya wajukuu 21,(watoto wengine ni wa kaka na dada za mama yake na Miriam). na yenye kipato kidogo, siku nyingine walikula na siku nyingine walilala njaa, lakini maisha yalikuwa yakienda. Miriam anasema kwamba pamoja na hali ile duni pale kwa bibi yake, bibi yake hakuwa na mzaha kabisa na kanisani, kila jumapili ni lazima kwenda kusali utake usitake. Miriam hakupenda sana kutokana na vile bibi yao alivyokuwa akitunza hela na vitu vingi vizuri kwa ajili ya kutoa sadaka wakati nyumbani wanalala na njaa. Wakati mwingine Padri wao aliwapita njiani wakati wa mvua wakinyeshewa bila kutoa hata lifti kwa gari ambalo limenunuliwa kwa sadaka zao. Miriam anasema kitu kimoja kilichomfanya asiache kwenda kanisani kilikuwa ni uimbaji tu, alipenda sana kuimba, na kanisani waliimba sana. Baada ya miaka kupita, mama yake alianza kuchoka na kuugua ugua, lakini alishindwa kuacha kazi kwa vile alikuwa akimsomesha Miriam ambaye ndio alikuwa ameanza chuo, Miriam naye alikuwa amechoka na maisha duni waliyokuwa wakiishi, maisha ya kuvaa 'kauka nikuvae' hali hii pamoja na kuona mama yake akiugua kila mara ikamfanya kufikia uamuzi wa kuacha shule na kutafuta kazi. Alipata kazi yake ya kwanza ya kuangalia mtoto katika familia ya kigiriki, alihamia pale na ulipofika mwisho wa mwezi wa kwanza alilipwa mshahara wake vizuri, mwezi uliofuatia akaambiwa asubiri kidogo kwa vile mwajiri wake alikuwa na matatizo kidogo, mwezi wa tatu mke wa mwajiri wake akamsingizia ameiba vitu ndani kwa hiyo hakuna mshahara. Miriam akaona huu ni uendawazimu, akaamua kuacha kazi. Akapata kazi nyingine kwa wazungu hii nayo ni ya kuangalia mtoto, anasema mambo yalienda vizuri hadi siku moja wakati wa likizo ambapo walisafiri, wakiwa huko wakafikia hoteli ya ufukweni. Hivyo wakati wa jua wao walikuwa wakijianika mchangani na Miriam akapewa kazi ya kukusanya shells kwa ajili ya kazi za sanaa za yule mzungu alizokuwa akizifanya. Siku ya kuondoka ilipofika bila sababu maalumu Miriam akaambiwa apande treni arudi, na wao wakarudi na gari walilojia. Katika ukusanyaji wake zile sheli aliweza kujaza ndoo mbili, hizi nazo aliambiwa arudi nazo kwa treni. Kwa hiyo yeye, mabegi yake na ndoo mbili zilizojaa shells tena katika daraja la tatu la treni!! hakuwa na la kufanya akapanda na kuanza safari ya kurudi, wakiwa njiani wakaambiwa inabidi wabadili treni wakatelemka na kusubiri nyingine. Ilipokuja akaanza kupandisha begi lake la nguo, akachukua ndoo ya kwanza ya shells, alipotaka kuchukua ya pili treni ikaanza kuondoka, haraka haraka akarukia ndani ya treni bila ndoo ya pili. Akaitizama ile ndoo iliyobakia akasema 'katu siiachi hii treni kwa ajili ya hiyo ndoo ya shells, sina hela nyingine ya nauli na hii treni ikiniacha ndiyo itakuwa mbaya zaidi'. Treni ikazidi kukaza mwendo na yeye akazidi kuitizama ile ndoo inavyobakia. Kufika Johannesburg alikuwa akitetemeka kwa hofu, alijiuliza atamwambia nini mwajiri wake kuhusu ndoo ya pili? baada ya kufikiri akaamua hatorudi tena kazini, hivyo akaachana na kazi ile nakuamua kurudi nyumbani.




Huku nyumbani hali ya mama yake ilizidi kuwa mbaya, miguu yake ilianza kuvimba hadi kushindwa kutembea, walimpeleka karibu kila hospitali bila mafanikio. Hivyo wakaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji 'isangoma', kule wakaambiwa kwamba kuumwa kwake si bure, mizimu ya kwao imemchagua awe mganga wa kienyeji 'isangoma' ili aweze kuwasiliana nao moja kwa moja na kuwaeleza watu mambo yaliyopita, kutabiri yajayo na pia kutibu wengine. Na kama anataka kupona maradhi yanayomsumbua ni lazima akubaliane na hilo, wote walifurahi na kukubali kwani wanasema kuchaguliwa na mizimu ilikuwa ni kama zawadi. Baada ya kukubali alitakiwa kufuata mchakato wa Ukutwasa. Ukutwasa ni mchakato au hatua za kumfanya mtu kupokea nguvu za mizimu hadi kuweza kuponya wengine (Mganga). Aliondoka na kwenda Swaziland ambako ukutwasa wake ulikuwa unafanyikia. Kutokuwepo kwa mama yake nyumbani kulimfanya yeye kuchukua majukumu ya mama yake, kama kuilisha na kuiangalia familia kwa ujumla. Kwa jukumu hili ilibidi atafute kazi tena na safari hii akaamua kuwa dobi. Wakati huo kulikuwa na wafanyakazi wengi wageni waliokuwa wakifanya kazi nchini, na hao ndio walikuwa wateja wake, kila jumatatu alikwenda kukusanya nguo zao chafu na ijumaa kuwarudishia safi. Haya ndiyo yakawa maisha ya Miriam.




Tangu akiwa shule hadi kipindi hiki anachofanya kazi za udobi, Miriam alikuwa na mpenzi wake chotara aliyeitwa James Kubayi au Gooli kama alivyojulikana kwa marafiki zake. Urafiki wao ulikuwa mzuri sana na kila mara walikuwa wote, Gooli alikuwa pamoja naye alipoacha shule, alipopata kazi kwa wazungu na hata sasa wakati mama yake alipokuwa Swaziland. Miriam alimpenda na kumuamini sana kiasi kwamba haukupita muda akapata ujauzito, hapo akiwa na umri wa miaka 17 tu. Anasema alikuwa na bahati sana kwani Gooli hakumtelekeza, alimchukua kumuhamishia nyumbani kwao. Familia ya kina Gooli ilikuwa inajiweza kidogo, mama yake alikuwa akipika pombe kama biashara ya ziada. Akiwa katika familia ya wakwe na mimba mambo yalikuwa magumu kidogo kwani Gooli hakuwepo muda mwingi alikuwa anachukua mafunzo ya upolisi katika mji mwingine hivyo alikuja pale kusalimia tu. Muda wa kujifungua ulipofika alipelekwa hospitali na kujifungua mtoto wa kike aliyemwita Sibongile au kwa kifupi Bongi. Alipotoka hospitali maisha hayakuwa rahisi tena, kazi zote za pale kwa mkwewe alitakiwa azifanye yeye, alikuwa akiamka saa 10 alfajiri kumuosha na kumlisha Bongi, kupika chakula cha wengine na kufanya shughuli zote za ndani na bado Bongi akilala alibaki kuhudumia wateja wa pombe hadi usiku wa manane.




Gooli alimaliza mafunzo yake na kurudi nyumbani, lakini alikuwa amebadilika sana tabia, alikuwa mkorofi na mwenye wivu wa kupindukia, alianza tabia ya kumpiga Miriam bila sababu za msingi, Miriam hakuwa na haki ya kusema lolote kwa Gooli, Miriam alianza kusononeka lakini alivumilia, alijua Gooli hampendi tena lakini hakujua ni kwa kiasi gani hadi siku moja alipomfumania na ndugu yake. Miriam alijua amemfumania mumewe kwa hiyo hapo ana nguvu ya kusema lakini badala yake kibano kilimgeukia yeye na kupigwa kipigo cha kifo. Kuanzia hapo alisema imetosha, alimchukua mtoto wake akakodi taksi na kurudi nyumbani kwao bila kuaga. Gooli alimfuata kumrudisha lakini alikuta mama yake amesharudi toka Swazilandi, alimkurupua vibaya sana na toka siku hiyo hakurudi tena na ndiyo ukawa mwisho wa Miriamu na baba mtoto wake kuonana.




Miriam sasa akiishi kwa mama yake, hakuwa na kazi yoyote ya kipato zaidi ya kumsaidia mama yake shughuli za Usangoma. Mama yake akaona hali hii haitamfikisha mahali popote mwanae, akamwambia ni lazima abadilishe kabisa mwelekeo wa maisha yake kwa kutafuta kitu cha kufanya. Miriam akaona ni bora aende mjini akaangalie cha kufanya, akamuacha Bongi na mama yake yeye akaenda mjini Johannesburg.





Johannesburg alifikia kwa binamu yake aliyeitwa Sonti Ngwenya, Sonti alikuwa na mwanaye wa kiume aliyeitwa Zweli ambaye walikuwa karibu rika moja na Miriam. Zweli na baadhi ya marafiki zake walikuwa wameanzisha bendi ya muziki iliyoitwa Cuban Brothers, wote walijua Miriam anaweza kuimba hivyo siku moja wakamuomba kama atataka kujiunga na bendi yao, Miriam akaona hii itakuwa ni kichekesho lakini akakubali kwa vile alikuwa tayari kufanya jambo jipya katika maisha yake. Akiwa Cuban Brothers walifanya maonyesho sehemu mbalimbali kama makanisani, kwenye sherehe za kuchangisha fedha (fundraising) na sehemu nyingine nyingi. Katika kipindi hicho kulikuwa na ukumbi maarufu sana uliojulikana kama Donaldson Community Centre ambao Cuban Brothers mara nyingi walikuwa wakipiga muziki hapo, huu ni ukumbi ambao watu wengi maarufu na wasio maarufu walipenda kwenda. Siku moja wakiwa katika onyesho Miriam alinong'onezwa na mwenziye kwamba Manhattan brothers wako ndani ya nyumba. Manhattan Brothers band kilikuwa ni kikundi cha muziki kinachojulikana sana wakati huo, kila mtu alipenda muziki wake. Baada ya onyesho Miriam alifuatwa na kijana mmoja na kujitambulisha kwa jina la Nathan Mdledle na kuwa ni kiongozi wa kundi la Manhattan Brothers, Miriam hakuamini macho yake kwamba anaongea na Manhattan brother, wakati akishangaa Nathan akamwambia anapenda jinsi anavyoimba, kama hiyo haikutosha, Miriam anasema almanusura aanguke baada ya kuambiwa anaonaje kama anataka kufanya usaili wa kujiunga na Manhattan brothers. Alikwenda kufanya usaili na kushinda hivyo akapata kazi.



Akiwa na Manhattan brothers aliweza kujulikana sana, hii ni kwa sababu kundi hili lilikuwa na kazi nyingi za ndani na nje ya nchi. Anasema Manhattan ilimfungulia milango yake ya mafanikio kwani baada ya kuwa nao makundi mengine mengi yalianza kumfuata ili afanye nao kazi yeye binafsi kama Miriam. Mwaka 1958 alipata bahati nyingine ya kuombwa kujiunga na kikundi cha African Jazz and variety. Hiki kilikuwa ni kikundi kinachozunguka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Mwanzilishi wake alikuwa ni mama wa kiyahudi aliyeitwa Sara Silvia. Mama huyu alisema kuwa atahakikisha African Jazz and variet, inakuwa ni kikundi cha kwanza ambacho waafrika wataruhusikwa kupiga muziki mbele ya wazungu. Na kweli ndivyo ilivyokuwa, kikundi hiki kilikuwa kikifanya onyesho kwa wazungu watupu kila Alhamisi katika ukumbi wa Johannesburg city. Mwaka 1959 akiwa bado na African Jazz, alipata bahati nyingine kubwa ambayo tunaweza kusema ndiyo iliyo mtoa. Mtengeneza filamu mmoja kutoka Marekani aliyeitwa Lionel Rogosin, alimuona Miriam akiimba kwenye shoo za African jazz, alipenda sana uimbaji wake na akamuomba aimbe katika filamu aliyokuwa akiitengeneza COME BACK AFRICA. Miriam alikubali na akaigiza na kuimba katika filamu ile. Baada ya hapo Lionel Rogosin aliondoka na kuwaahidi kuwataarifu atakapomaliza kuitayarisha filamu ile. Huku nyuma mwaka huo huo 1959 februari, bahati nyingine ikaja kwa Miriam, King Kong Jazz Opera ilifunguliwa na Miriam akapata nafasi ya kuimba na kuigiza mle kama Joyce "Queen of Back of the Moon".

KUONDOKA AFRIKA.

Baada ya muda kupita Lionel Rogosin akaleta habari kwamba filamu yake ya COME BACK AFRICA imekamilika na imepokelewa vizuri hivyo ameiingiza katika Tamasha la Filamu la venice Italia(VENICE FILM FESTIVAL) kwa hiyo anamualika Miriamu Makeba kuungana naye katika kuitambulisha film hiyo huko Venice na Ulaya kote.

Anasema hakuamini macho yake kupata nafasi ya kwenda Ulaya, wakati huo kazi yake ilikuwa ikienda vizuri sana alikuwa bado akifanya kazi na King Kong kitu ambacho ni hatua kubwa sana kwake yeye na sasa anapata nafasi ya kwenda Ulaya? Hakuamini macho yake. Haraka aliomba pasipoti, alisumbuliwa sana hadi kuipata kwa sababu makaburu walijua kila kitu kuhusu Miriam na walijua kwamba ameshiriki katika filamu ya come back Africa, hatimaye alipewa na kuondoka bila kuchelewa, ilikuwa ni mwaka 1959.



Safari yake ilianza na alifika London salama na kukutana na mwenyeji wake Lionel Rogosin na mkewe. Akiwa pamoja na wenyeji wake sasa walianza safari ya kuelekea Venice Italy kwa gari. Walifika Venice wakazindua film yao katika tamasha lile na kwa bahati film yao ikawa ni miongozi mwa film zilizopata tuzo, ilishinda Critic Award.



24 February 2007

Dhambi ya mapenzi kwa jinsia moja.




Kadri siku zinavyoendelea suala la mapenzi ya watu wa jinsia limekuwa likizidi kupanuka, wapo watu wanalolipinga na kusema ni dhambi na wako wanaosema si dhambi kwa vile watu hao hawakuichagua hali hiyo, wamezaliwa hivyo. Watu hawa ambao hujulikana kwa wanaume kama 'Basha na wasenge', na kwa wanawake 'Wasagaji', wamekuwa wakipigania kukubalika katika jamii na hata kupewa majukumu mbalimbali ya uongozi. Wanataka waongoze nchi, wanataka waongoze makanisa bado sijasikia wanaotaka kuongoza misikiti. Hali imekuwa ni ngumu kwao hasa katika hili la uongozi. Swali langu ni kwamba je wanapaswa kupewa nafasi hizi au hapana? na kama suala ni dhambi je hawa wengine wasio wasenge/wasagaji wao hawana dhambi? au kuna dhambi na dhambi ambazo Mungu anakubaliana nazo? Nisaidieni mwenzenu katika hili.

27 January 2007

Nani kama Serena?


Serena Williams, mwanamke wa shoka huyu katika mchezo wa tennis ya wanawake daima hatabiriki. Serena na dada yake Venus William wamesumbua sana dunia ya Tennis katika miaka ya nyuma hadi 2003 kwa kushika namba 1 na 2 ya dunia. Baada ya hapo walianza kushuka ghafla kiasi cha kutolewa hata katika raundi ya kwanza, Serena alishuka hadi namba 95 na Venus 47. Kama kawaida maneno yakaanza...'wajiuzuru sasa wameshazeeka..., na maneno mengine meengi. Lakini mwaka huu bila mtu kutegemea, Serena alijitupa tena uwanjani katika Australian Open ambayo hufanyika kila Januari. Watu tukasubiri labda atatolewa raundi ya kwanza..wapi.., ya pili..wapi, ya tatu.. wapi.., mara robo fainali, Heee! waandishi wakaanza kuandika 'Serena looks dangerous'. Watu wakaanza kufunga midomo, mara fainali tena na mchezaji tishio Maria Sharapova, kama mchezo vile Serena akamsambaratisha vibaya vibaya Maria kwa 6-1, 6-2. Ushindi huu amemzawadia marehemu dada yake Yetunde Price aliyeuawa mwaka 2003.

Ni nani kama Serena?

Kama hamuamini niyasemayo fungueni hapa, na hapa.

21 January 2007

Shiriki mjadala.

Kwa wanablogu wote wapendao maendeleo ya blogu na jamii kwa ujumla, mnakaribishwa kushiriki mjadala wa uundaji wa jumuiya ya wanablogu Tanzania. MtiMkubwa mjadala huu unakuhusu pia. Bonyeza hapa.

Mbio za Hillary Clinton kuelekea 2008.


Mbio za Mama Hillary Clinton, mke wa rais mstaafu wa Marekani Bwana Bill Clinton sasa zinaelekea kutamu. Pata ujumbe mzima hapa.

05 January 2007

Asha Rose Migiro...Hongera mama!!!!!



Sina maelezo ya kutosha kuielezea furaha niliyonayo ndugu zanguni. Naomba fungua hapa na hapa upate habari kamili.

25 December 2006

Mti wa Krismasi..


Krismasi imefika, watu wote duniani tunahaha kupamba nyumba na mitaa yetu kwa miti ya krismasi. Bado sijui vizuri kwa nini sherehe hii inaambatana na miti hii. Ombi langu la leo ni kwa yeyote yule anayejua hasa maana ya mti huu naomba atushushie darasa.

Nawatakia sikukuu njema.

20 December 2006

Mandela kutibiwa zaidi nchini Tanzania..

Tanzania kuwa kimbilio la matibabu ?...Sipati picha kabisa! Hebu msomaji ungana nami kupata picha hii kwamba... "Mandela apelekwa Tanzania kwa matibabu zaidi, Materazzi akimbizwa Tanzania kwa matibabu ya goti au watoto Nigeria wapelekwa Tanzania kwa matibabu ya moyo na mengine mengi"... Hebu hata wewe msomaji pata picha Tanzania ikitoa huduma zote hizo hivi leo hii tungekuwa nafasi gani duniani? Sijui ni ndoto zangu tu, lakini kila mara napata picha kwamba ipo siku na sisi tutapokea watu duniani kuwasaidia badala ya sisi kila mara kupokewa. Kwa maoni yako msomaji unadhani hili linawezekana?

19 November 2006

Shabiki na Ushabiki!

Wasomaji wapendwa, habari hii chini inawajia kwa hisani ya mwanablogu MtiMkubwa.....

Naam,

Hakuna kitu kibaya kama unazi, ushabiki, au umaamuma. Ushabiki unaweza kuwa wa kidini, kiitikadi, kikabila, kirangi, kimichezo, kitaaluma au hata kumshabikia mtu binafsi. Shabiki akiamua kushabikia jambo analoshabikia hata wakitumwa malaika, mitume na manabii kumsilimu hasilimiki.

Siku chache zilizopita nilikutana na shabiki mmoja. Huyo shabiki alipoanza ushabiki wake nilifikiri alikuwa anatania kwa sababu sijawahi kukutana na mtu anayemshabikia mtu kwa namna ya yule shabiki. Sina jinsi ya kumuelezea shabiki mwenyewe lakini ni kijana anayetokea mikoa ya kanda ya ziwa, tena ana lafudhi kali ya kanda ya ziwa, na aliyebahatika kupata ajira serikalini. Tulikuwa tunazungumzia operesheni bomoa bomoa ya RC Kandoro, ndipo huyo shabiki alipoingilia mazungumzo na kusema "..Hiyo yote ni mipango ya JK..Unajua ameunda Wizara ya Mazingira iri kumekishua kwamba jiji rinakuwa safi..Yeye mwenyewe yuko Marekani rakini huku nyuma kaacha maagizo akirudi Wamachinga wawe wameshaondoka.." Miye na jamaa yangu mwingine tukageuka kumsikiliza shabiki. Alipoona tumeonyesha nia ya kumsikiliza ikawa tumefungulia ushabiki "..JK bwana ni mjanja sana. Unajua kamreta huyu kocha iri Tanzania iende woridikapu. Na huo ni mmoja wa mipango yake ya muda mrefu..Na utaona Tanzania itafika woridikapu.." Jamaa yangu akamuuliza "..Tanzania itafika woldikapu kwa sababu ya JK?.." Yule kijana akajibu "..Usifanye mchezo na JK, nyie turieni mtaona..Unajua JK amekwenda Marekani kwenye jenero asembri rakini pia kaenda kuonana na Bush..Yaani Bush anamuadimaya sana JK katika viongozi wote wa Afrika..." Jamaa yangu akaniambia "..Unasikia insaidi storizi hizo?.." Nikamjibu "..Nazisikia.." Yule kijana kusikia hivyo moto ukazidi kumpanda "..Kwa mikakati ya JK bai dhe endi ofu dhisi manthi yaani Septemba umeme utakuwa umerudi nchi nzima..Yaani jamaa anachapa kazi siyo mchezo endi hi izi so krozi tu dhe pipo kwa hiyo anayajua matatizo ya Watanzania kwa karibu zaidi anraiki Mkapa..Mkapa arikubarika inteneshinari rakini rokari hakuwa karibu na wananchi..JK ameshaanza kurudisha njia za kuu uchumi mikononi mwa wananchi, ATC tayari imesharudi harafu sasa hivi anashugurikia mikataba ya madini, yaani kwa kweri katika kipindi kifupi amefanya mambo mengi sana tena makubwa.." Jamaa yangu akamwambia "..Aisee.." Hapo shabiki ndiyo akazidi kupamba moto "..Ingekuwa JK ndiye ariyekuwepo madarakani wakati ure Baba wa Taifa asingefariki.." Niliposikia hivyo ikabidi niingilie mazungumzo "..Hebu tuache ushabiki hapa na tuzungumze yaliyo kweli..Ni kweli kuwepo kwa JK madarakani kunaweza kurefusha au kufupisha maisha ya mtu au watu.." Kabla sijamaliza hoja yangu yule shabiki akarukia "..Na ndiyo maana awamu ya ine sera yao ni Maisha bora kwa Watanzania wote..JK anataka kira Mtanzania awe na maisha bora..Ndiyo maana hapati usingizi kwa kufikiri jinsi gani atawapatia Watanzania maisha bora..Yaani kwa kweri tunaomjua kwa karibu tunaerewa anavyohangaika kuwatafutia Watanzania maisha bora.." Jamaa yangu akamwambia "..Ndiyo hatamu na maana ya uRais kulinda masilahi ya wananchi wake.." Shabiki akajibu "..Rakini siyo maraisi wote wanakumbuka hiro na hapo ndipo JK anapochukua pointi kurinda masirahi ya wananchi..JK bwanaa..Yaani wee acha tu..Baadhi ya watu hawamuerewi kwa hiyo wanamkritisaizi widhiauti eni graundis..Aripoteuwa kabineti wapinzani wakamkritisaizi eti baraza kubwa sana.. Yeye ariunda kebineti kubwa iri kuzidisha efishensi..Sasa hivi ware wariomkritisaizi wameshushuka baada ya kuona jinsi kabineti inavyochapa kazi..Ini Tanzanian histori kabineti hii ni drimu timu..Hakuna kabineti iriyowahi kuundwa kama hii ya sasa hivi, yaani kira ariyepewa wizara inamfiti..Teri mi huu izi ini dhe rongi ministri?! Shemeji yangu Dokta Migiro fits pafektri weri in foreni afeazi.. Mama Meghji -fainansi, bajeti aliyoisoma hata Kenya na Uganda wameomba kopi..Msabaha kwenye madini na nishati humo ndiyo mwake kabisa, unajua mambo ya madini ni grobo biznesi na Msabaha ni mtu dipromasia kwa hiyo atayauza madini kiurahisi na kwa bei nzuri tu...Mramba wizara ya miundombinu, jamaa ni rongi eksipiriensid na JK kamuweka pare makusudi kwa sababu pare panatakiwa mtu mwenye rongi eksipiriensi.." Jamaa yangu akamwambia "..Ahaaa hili baraza kiboko.." Shabiki akarukia "..Harafu ormosti dhe whori kabine au thrii kota ni niyuu fesiz tena ni vijana vijana na akina mama kawapa wizara nyeti zote isipokuwa urinzi..Hapo ndipo anapothibitisha Nguvu mpya, Ari mpya, na Kasi mpya JK bwana ni kiboko..Nyie bwana JK izi dhe prezidenti..Halafu amekubarika na wananchi, ukiangaria historia ya Tanzania ni viongozi wanne tu wariokubarika na Wananchi; Hayati Baba wa Taifa, Hayati Sokoine, Agostini Murema, na JK! Bati Murema disapointedi dhe masizi kwa hiyo femu yake inawitha siku hadi siku.." Wakati anaendelea kutupiga darasa kilongalonga chake kikamuita akasogea pembeni kuongea, alipomaliza akarudi kutuomba radhi kwamba ameitwa ofisini, akaondoka. Miye na Jamaa yangu tukaondoka tukiwa ndani ya gari jamaa yangu akaniambia hayo ndiyo maoni ya wengi.

Leo nimekutana na kipande kingine cha habari. Miye nimekiona kama ushabiki wa yule shabiki wa Kikerewe. Ningelikuwa na namna ningewaomba viongozi wambane huyo tarishi wa Waziri Mkuu wa Malaysia aliyeko nchini Tanzania juu ya mkataba wa IPTL. Halafu pia kumdhibiti asije akatuletea balaa nyingine kubwa zaidi ya IPTL. Ushabiki wenyewe huo hapo chini.

Ziara za JK nje zaanza kuzaa matunda 2006-11-18 10:34:26 Na Joseph Mwendapole

Ziara za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi kutafuta wawekezaji, sasa zimeanza kuzaa matunda kutokana na baadhi ya wawekezaji kuwasili nchini kuangalia mazingira ya uwekezaji. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Mipango na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, alisema makampuni mengi yamekuwa yakiandika barua pepe yakionyesha nia ya kuja kuwekeza nchini. Alitaja baadhi ya wawekezaji ambao tayari wamewasili nchini kuwa ni Benki ya Uwekezaji ya Kuwait, ambayo Mkurugenzi wake, Bw. Jassem Zainal yuko nchini kuangalia mazingira ya kuwekeza. Waziri Ngasongwa alimtaja mwingine kuwa ni Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Bw. Annuary Ibrahim, ambaye ameambatana na wageni hao. Alisema Bw. Ibrahim aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kusaidia kampeni zake za kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini. Dk. Ngasongwa alisema Bw Ibrahim ni rafiki wa kweli aliyekubali ombi la Rais Kikwete kuitangaza Tanzania duniani. ”Kuonyesha kuwa kweli ni rafiki yetu, Bw. Ibrahim leo ametuletea wawekezaji watakaowekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya fedha,” alisema. Alisema wawekezaji hao bado wanaendelea na mazungumzo na serikali ili kuangalia namna ya kuendesha shughuli zao. ”Wamenihakikishia kuwa, mambo yakienda sawa mwanzoni mwa mwaka ujao wataanzisha benki kubwa ambayo itakopesha watu wengi kwa riba ndogo,” alisema Dk. Ngasongwa. Dk. Ngasongwa alisema Korea imeahidi kujenga daraja la Malagarasi kwa dola milioni 25 za Kimarekani ambazo zitatolewa kwa Tanzania kama mikopo nafuu. Alisema wawekezaji wa kampuni ya Samsung na DAEWOO, imeahidi kuwekeza upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Alisema serikali ya nchi hiyo pia imekubali kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme. Akizungumzia ziara ya China, Dk. Ngasongwa alisema serikali ya nchi hiyo imeahidi kusaidia kuongeza uzalishaji katika mradi wa Kiwira hadi kufikia Megawat 200 kutoka sita za awali.

04 November 2006

Huyu ni nani?

22 October 2006

Wangari Muta Maathai.


Wangari Muta Maathai, mwanamke mwafrika wa kwanza kushinda Nishani ya amani ya Nobel tangu kuanzishwa kwake mwaka 1900.

Mwaka 2004, niliposikia mwanamazingira mama mpanda miti, Wangari Maathai ndiye mshindi wa nishani ya Amani ya nobel, nilishindwa kabisa kuelewa ni kwa kigezo gani aliweza kuchaguliwa kuwa mshindi wa tuzo hii ambayo ni moja wapo ya tuzo ya zaidi ulimwenguni. Nilijiuliza "Miti na Amani" wapi na wapi? na kutokana na swali hilo nilianza kumfuatilia kwa makini zaidi mama huyu na ndipo nilipogundua uwezo mkubwa wa akili alionao mama huyu.

Mama Wangari Muta Maathai alizaliwa 01/04/1940 katika kijiji cha Tetu kilichopo Nyeri nchini Kenya. Baba yake bwana Muta Wanjugu na mama yake Lydia Wanjiru Muta ambao walikuwa wakulima, walimpeleka Wangari shule baada ya kaka mkubwa wa Wangari Nderitu kushauri kwamba dada yake ni lazima asome kitu ambacho katika miaka hiyo kilikuwa ni nadra sana, ni watoto wachache sana wa kike walipelekwa shule katika miaka hiyo.

Hivyo alianza shule ya msingi Itithe mwaka 1948 hadi 1951 darasa la kwanza hadi la nne. Akafuatia shule ya Mtakatifu Cecilia mwaka 1952 hadi 1955 darasa la tano hadi la nane. Alimaliza elimu ya msingi na kujiunga na sekondari ya wasichana ya Loreto kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1956 na 1959. Baada ya hapo alibahatika kupata ufadhili wa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya masomo ya juu zaidi, huko alijiunga na chuo cha Mtakatifu Scholastica cha Kansas kwa Shahada yake ya kwanza katika baiolojia ikiwa ni mwaka 1960 hadi 1964, mwaka huo huo 1964 alijiunga na chuo kikuu cha Pittsburgh kwa shahada ya pili ambapo alimaliza mwaka 1965. Mwaka 1966 alirudi nyumbani Kenya na kupata kazi katika Chuo kikuu cha Nairobi kama mtafiti msaidizi.

Mwaka 1969 alifunga ndoa na mfanyabiashara na mwanasiasa Bwana Mwangi Mathai, ambapo walibarikiwa kupata watoto watatu, Wanjira, Weweru na Muta. Kuwa na familia yake mwenyewe haikumfanya Wangari kuacha kujiendeleza kimasomo, kwani mwaka 1971 Waangari alipata PhD na inasemeka kwamba alikuwa ni mwanamke wa kwanza kutoka Afrika mashariki na kati kufikia kiwango hicho cha elimu. Na mwaka 1977 alikuwa Profesa.

MWANZO WA KUWA MWANAMAZINGIRA NA KUINGIA KATIKA SIASA.

Mwaka 1974 Bwana Mwangi Mathai muwewe na Waangari aliamua kugombea ubunge katika jimbo la Langata, Wangari akiwa mkewe ilibidi awe bega kwa bega na mumewe katika kampeni. Bwana Mwangi kama ilivyo kawaida ya wanasiasa aliwaahidi mambo mengi wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutatua tatizo la ajira. Wangari alisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi na hakuyachukulia mzaha. Kwa bahati nzuri Bwana Mwangi alishinda kiti cha ubunge, na ni hapo Wangari aliona umefika wakati wa kuyatekeleza yale waliyokuwa wakiahidi. Akaamua kuunda kampuni binafsi iliyoitwa ENVIROCARE malengo yake ikiwa ni kutaka kutengeneza ajira kwa wananchi, lakini kwa bahati mbaya kampuni haikuendelea kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha. Wakati huo huo Wangari alikuwa ameshaanza kujihusisha na harakati za ukombozi wa mwanamke na tayari alikuwa mwenyekiti wa baraza la Taifa la wanawake Kenya, akiwa kiongozi katika baraza hilo aliendelea kupata malalamiko juu ya shida wanazozipata wanawake katika maisha yao ya kila siku, kwamba hawana maji, kuni wala chakula chao na cha mifugo yao na huwalazimu kutembea mwendo mrefu ili kuvipata hivyo.

Wangari aliyatizama yale malalamiko na kuona kuwa ni matokeo ya ugonjwa mbaya uliyoikumba Kenya na nchi nyingi za Afrika. Ugonjwa wa kuharibu na kutokujali kabisa mazingira, miti kukatwa ovyo bila kupandwa mingine ndio aligundua kuwa na chanzo shida zote wanazozipata wananchi wa Kenya. Hivyo akaja na wazo la kuanzisha mradi wa kupanda miti kwani miti huilinda ardhi mmomonyoko wa udongo, huifadhi vyanzo vya maji, hutoa chakula, mbao za kujengea, kuni na huweza kuwa chanzo kipato na mambo mengine mengi.

Hivyo tarehe 05/06/1977 ambayo pia ilikuwa ni siku ya mazingira duniani, Wangari alizindua rasmi kampeni ya upandaji miti Kenya, yeye na wenziye walianza kwa kupanda miti saba katika bustani ya Kamukunji Nairobi. Na kuanzia hapo Jumuiya vuguvugu ya ukanda wa kijani ilizaliwa (The Green Belt Movement).

Ingawa jambo hili alilolianzisha Wangari ni jema na lina nia nzuri kwa Wananchi lakini si wote walioliunga mkono. Baada ya kusimama na kuonekana hana mzaha kwa kile anachokifanya hasa akiwa mwanamke, upinzani ulianza kujitokeza kuanzia katika familia yake hadi katika serikali tawala kipindi hicho chini ya Rais Daniel Moi.
Kwa upande wa kifamilia, mumewe bwana Mwangi kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi wa kiafrika kutaka kutawala wake zao, hapa ilishindikana kabisa kwani alikuta mkewe ni mtu anayesimama na kupigania kile anachokiamini ni kweli. Matokeo ya haya yote bwana Mwangi aliamua kutoa talaka kwa madai kwamba mkewe ni mkaidi mno, msomi mno mwenye mafanikio makubwa na ni kazi kubwa kumthibiti. Ndoa yake ilivunjika miaka ya themanini.

Kwa upande wa serikali, alipata matatizo kwa vile alikuwa na ujasiri wa kudiriki kuisema serikali ya Moi hadharani bila woga kitu ambacho kilimsababishia kutiwa gerezani mara kadha wa kadha, kupigwa hadi kupoteza fahamu na askari. Lakini katika mambo hayo yote linalokumbukwa zaidi ni lile la miaka ya tisini, ambapo serikali ilitaka kutumia eneo la bustani ya kupumzikia ya Uhuru Park ya Nairobi kujenga jengo la ghorofa 62 ikiambatana na sanamu yake yenye urefu wa futi 60 vyote hivi vikikadiriwa kugharimu dola za kimarekani milioni 200, ambazo nazo ni za kukopwa katika mashirika ya kigeni. Kwa hali moja au nyingine wako ambao hawakulipenda wazo hili lakini kutokana na kukosa ujasiri wa kumkosoa Rais Moi hakuna aliyediriki kupinga. Wangari mwanamke wa shoka alisema hakijengwi kitu hapa. Alikuwa na sababu kuu mbili:
1. Sababu ya kimazingira - kwamba ni kwanini litumike eneo la kupumzikia watu
kujenga ghorofa hilo? ..akaendelea kwamba "Tembo na Vifaru wanatengewa sehemu
za kupumzikia, kwa nini na binadamu wasiwe na sehemu ya kupumzikia?

2. Sababu za kiuchumi - kwamba inakuwaje nchi kama Kenya ambayo watu wake wanakufa
kwa njaa na wakati huo huo inakabiriwa na madeni makubwa, bado inataka kukopa
fedha zote hizo kwa ajili ya jengo moja tu la fahari?.

Msimamo wa Wangari ulifanya mashirika yaliyokuwa yamekubali kutoa fedha hizo kubadili mawazo yao na wazo la kujenga jengo la fahari na sanamu ya Moi kuishia hapo. Kutokana na hili Rais Moi alikasirika sana hadi kuifunga ofisi ya Green belt Movement, ingawa baadaye ilifunguliwa. Na kuanzia hapo alimbatiza jina la 'Mad Woman'. Pamoja na hayo yote bibi Wangari hakukata tamaa kufanya kile alichoamini kuwa anatakiwa kukifanya na hakujua ni kwa kiasi gani kumbe dunia ilikuwa ikimuunga mkono hadi mwaka 2004 ambapo alishangazwa kwa kuchaguliwa kwake kuwa mshindi wa Nishani kubwa ya Amani duniani.

UHUSIANO KATI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA AMANI DUNIANI.

Kama nilivyosema hapo awali kwamba mimi pia sikuelewa uhusiano uliopo kati ya upandaji wa miti na amani duniani, kuna watu wengi ambao pia hili liliwatatiza na kupelekea watu wengi kutaka kujua uhusiano uliopo. Na Bibi Wangari alijibu kama ifuatavyo....
Vita vyote vilivyopo duniani leo ni vita vya kugombea mali asili kama ardhi yenye rutuba, maji, mafuta, madini n.k na watu wamesahau kwamba hivi vyote vinatokana na utunzaji mzuri wa mazingira ambao hupelekea kutokupungua kwa mali asili, na hivyo kila mmoja kupata za kumtosha, hali ambayo inapunguza migogoro ya kunyang'anyana na kufanyiana hila za kuuana. Kwa hiyo basi kwa kupanda miti tu kunaweza kuhakikisha amani kubwa sana duniani, kwani miti italeta mvua, ardhi itapata rutuba, wafugaji hawatatapatapa kutafuta malisho, kuni zitakuwepo za kutosha, chakula cha kutosha, umeme n.k na ni kwa dhana hii pekee ya Bibi Wangari ya kupenda kushughulika na chanzo cha tatizo ndiyo iliyompelekea kupata Nishani ya Amani ya Nobel mwaka 2004. Na kuanzia hapo dunia ilianza kumtafuta ili kupata zaidi busara zake. Miongoni akiwa ni Oprah Winfrey. Hapa pia kuna hotuba yake aliyoitoa mwaka huu katika chuo cha Connecticut kilichopo Marekani, kwa kweli hotuba hii nimeipenda sana na inatia moyo sana hasa kwa wale tunaopenda kusimama katika ukweli wa lile unaloliamini hata kama hakuna anayekuunga mkono.

Mungu mbariki Mama Wangari Muta Maathai.

01 October 2006

Amina Chifupa awe mfano wa kuigwa kwetu sote...

Alipokuwa akiapishwa kumbe alikuwa na lake kichwani

Hivi ingekuwaje kama kila Mtanzania mwenye uwezo kimaisha angejitolea kusomesha japo watoto watoto wawili tu wanaotoka katika familia zisizojiweza? Amina Chifupa ameamua kufanya jambo ambalo nadhani wengi hawakulitegemea, kachukua jukumu la kusomesha watoto 20 wasiojiweza kwa kweli nampongeza sana na ingependeza kama na sisi tungeiga mfano huu japo kusaidia watoto waishio vijijini wanaoacha shule kwa kukosa sare za shule au madaftari na kalamu. Endelea na habari ya Amina hapo chini:-


Amina Chifupa kusomesha yatima
2006-10-01 09:55:33
Na Sabato Kasika na Caroline Mosha wa TSJ

Mbunge wa viti maalum vijana (CCM), Bi. Amina Chifupa, amejitolea kusomesha watoto yatima 20 wa kituo cha kulelea yatima cha (CHAMAWATA) kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo alisema hayo jana wakati akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa yatima wa kituo hicho, vikiwemo vifaa vya shule na magunia kumi ya mkaa.

Mheshimiwa Chifupa alitoa viatu vya shule jozi 60, mabegi 60, soksi jozi 60, Madaftari 400, kompasi 60,kalamu za wino na risasi na rula 60,Kamusi tano za kiingereza pamoja na Malapa jozi 60.
Pia alitoa unit 100,000 za umeme wa Luku.

Kituo hicho chenye zaidi ya watoto 60 ambao ni yatima kilikabidhiwa msaada huo jana mbele ya Diwani wa Kijitonyama Bw. Omary Kimbau na Rais wa Chama cha Kampeni dhidi ya UKIMWI (SGACUD) Bw. Herman Berege.

Katika ahadi ya kusomesha watoto 20, mbunge huyo alifafanua kuwa atawalipia karo ya shule za awali kwa muda wote hadi hapo watakapoanza elimu ya msingi.

”Nilijisikia uchungu sana nilipoambiwa na katibu wa kituo hicho kuwa watoto wengi hawaendi shule kwa sababu hawana ada ya kuwalipia”,alisema Chifupa.

Pamoja na msaada kutoka kwa mbunge huyo kituo hicho pia kilipokea msaada wa shilingi 40,000 kwa ajili ya ada ya wanafunzi wawili na lita 20 za mafuta ya kupikia kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu waliopo kwenye chama cha SGACUD.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo mama mlezi wa kituo hicho Bi. Saida Hassan alisema anawashukuru Mh. Chifupa na wanafunzi kutoka SGACUD kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha.

Naye Diwani wa Kijitonyama, Bw.Kimbau alimshukuru Mh.Chifupa kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Mapema akizungumza na Nipashe baada ya kutoa msaada huo, mbuge huyo alisema kuwa amesukumwa na upendo alionao kwa wahitaji na hivyo akajitolea kuwasaidia yatima wa kituo hicho.

”Mimi kama Mtanzania ninaamini yatima wanahitaji mapenzi na misaada na kutoa siyo utajiri bali ni moyo wa huruma alionao mtu kwa wahitaji wanaomzuguka,” alisema Bi. Amina.

Alisema kuwa kuna vituo vingi vya yatima hapa jijini Dar es Salaam ambavyo vinahitaji msaada, lakini amemua kuanza na hicho cha Sinza na kwamba kadri Mungu atakavyomjalia ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine.

Hivi karibu Chifupa alitoa fedha zaidi Sh. milioni 1.5 kwa timu ya taifa baada iliyoifunga timu ya Burkina Faso.

25 August 2006

The strong black woman has died...


Kwa kweli kuna habari zingine unapotumiwa inakuwa si vizuri kuzisoma na kuzifaidi peke yako. Mfano ni hii habari ya mwanamke huyu wa kiafrika ambaye anapoteza dira na kushindwa kufikia malengo yake bila sababu za msingi kabisa, sijui wenzangu mnasemaje katika hili...Mwandani kaka yangu nakushukuru sana sana sana kwa habari nzito na yenye kutuzindua akili.

The Strong Black Woman Has Died

While struggling with the Reality of being a Human
instead of a myth, the Strong Black Woman passed away.

Medical sources say she died of natural causes,

but those who knew her know she died from

being Silent when she should have been

Screaming, Smiling when she should

have been Raging, from being sick

and not wanting anyone to know

because Her Pain might

inconvenience them.

She Died from an overdose of other people

clinging to Her when she

didn't even have

Energy for Herself.

She Died from Loving Men who didn't

Love themselves and could only

offer her a crippled reflection.

She Died from raising Children Alone.

She Died from the Lies her Grandmother

told her Mother and her Mother told

her about Life, Men & Racism.

She Died from being sexually abused as

a child and having to take that Truth

everywhere she went every day of

Her Life, exchanging the

humiliation for guilt

and back again.

She Died from asphyxiation, coughing up

blood from Secrets she kept trying to

burn away instead of allowing

Herself the kind of nervous

breakdown she was

entitled to.

She Died from being Responsible, because

She was the last rung on the ladder and

there was no one under her She

could dump on.

The Strong Black

Woman Is Dead.

She Died from being a Mother at 15

and a Grandmother at 30 and an

Ancestor at 45.

She Died from being dragged down and

sat upon by un-evolved Women posing

as Sisters and Friends.

She Died from tolerating Mr. Pitiful,

JUST to have a Man around the house.

She Died from sacrificing Herself for

Everybody and Everything when

what She really wanted to do

was be a Singer, a Dancer,

or some Magnificent other.

She Died from Lies of omission because

She didn't want to bring the

Black Man down.

She Died from Tributes from her counterparts

who should have been matching Her Efforts

instead of showering her with dead words

and empty songs.

She Died from Myths that would not allow

Her to show Weakness without being

chastised by the Lazy and Hazy.

She Died from hiding her Real Feelings

until they became Hard and Bitter

enough to invade Her womb and

breasts like angry tumors.

She Died from always lifting something

from heavy boxes to refrigerators

All By Herself.

The Strong Black Woman Is Dead.

She Died from never being Enough of what

Men Wanted, or being Too much for the

Men She Wanted.

She Died from Being too Black and

Died again for not Being

Black enough.

She Died from being Misinformed about her

Mind, her Body & the extent of her

Royal capabilities.

She Died from knees pressed too close together

because Respect was never part of the

foreplay that was being shoved at Her.

She Died from Loneliness in Birthing rooms

and Aloneness in Abortion centers.

She Died in bathrooms with Her veins busting

open with Self-Hatred and Neglect.

And Sometimes when She Refused to die,

when She just Refused to give in, She

was Killed by the lethal images of

blonde hair, blue eyes, being

rejected by the OJ.'s, the

Quincy's, the Cuba's,

& the Kobe's.

Sometimes, She was stomped to Death by

Racism and Sexism, Executed by Hi-Tech

ignorance while She carried the

Family in her belly, the

Community on her

head, and the

Race on her back!

The Strong Black Woman Is Dead!

13 August 2006

Hivi tunasemaje juu ya " Darwin's Nightmare?

MtiMkubwa anasema...........

Ndugu wapenzi,

Nimepata kuitazama filamu ya Darwins Nightmare ambayo imekuwa ni sehemu ya gumzo la kitaifa kwa sasa. Kwa wale ambao hamjapata kuiona tafadhalini naomba itazameni au isomeni hapa japo kwa ufupi ili nanyi muwe na maoni yenu kutokana na kuiona. Nawaombeni tufanye hivyo ili tusije tukawa kama wale waliokuwa wanapinga kitabu cha Salman Rushdie bilia ya kukisoma.

Penye ukweli uongo hujitenga,

Waliosaidia kutengeneza filamu wadakwe-Wabunge

2006-08-12 09:53:52
Na Namsembaeli Mduma, Dodoma

Wabunge wa Bunge la Muungano, wameiomba serikali iwakamate washiriki wote waliohusika kutengeneza au kufanikisha filamu ya The Darwin’s Nightmare(Jinamizi la Darwin), maarufu kama filamu ya mapanki, kufuatia uongo walioutumia katika sinema hiyo kuichafua sura ya Tanzania nje, pamoja na kuwadhalilisha Watanzania.

Aidha, imeombwa iwachukulie hatua kali za kisheria Watanzania wasaliti hao, pamoja na wahusika wengine, badala ya karipio tu, ili wawe mfano kwa wote wenye nia au watakaojaribu kufanya udhalilishaji kama huo ulioonyeshwa kwenye filamu hiyo, mara baada ya uchunguzi unaoendelea juu yao kukamilika.

Sambamba na maombi hayo, wabunge hao, bila kujali ni wa upinzani au chama tawala, wameitaka serikali iandae filamu mbadala itakayoonyesha uwongo uliotumiwa kwenye hiyo ya The Nightmare, ili kuuonyesha ulimwengu ukweli kuhusu Ziwa Victoria na biashara yake ya sangara, kwa kuwa asilimia kubwa ya yaliyozungumzwa ni uzushi.

Lengo jingine lililotajwa ni kuisafisha Tanzania kwa ujumla kuhusiana na kashfa hiyo nzito ya silaha, inayoelezwa kulenga kuiharibia nchi kwa mataifa mengine juu ya amani iliyoigubika.

Hoja hiyo ya kutengenezwa filamu mbadala, licha ya kuungwa mkono na wabunge karibu wote wa Bunge hilo, iliwasilishwa kwanza na Bungeni hapo jana asubuhi na Kambi ya Upinzania kupitia Msemaji Mkuu wao, Bw. Khalifa Suleiman Khalifa.

Aliungwa mkono kwa karibu na Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA).

Vile vile, hoja ya kutengenezwa filamu hiyo nyingine ya kweli ilisemwa Bungeni hapa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Bw. Johnson Mwanyika, wakati akisoma azimio la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu filamu hiyo yenye utata.

18 July 2006

Zima moto..

Yule mwanablogu mwenzetu MtiMkubwa ambaye hapo awali alishawahi kutuletea hoja ya binadamu ni sawa lakini si sawasawa ameibuka tena. Hapa chini ametuletea habari nyingine inayotuonyesha jinsi tulivyo sawa lakini si sawasawa katika kufanya maamuzi ya lipi lakufanya na lipi si la kufanya..endelea hapo chini:-

"Lilipotokea tukio la Septemba 11 kule New York nilikuwa ziarani kikazi mwituni kwenye kijiji kidogo sana. Nilipokuwa katika gari nikielekea mwituni nilikokuwa nikienda kufanyakazi, nilikuwa nasikiliza muziki toka radioni mara ghafla radio ikakata muziki na kutupasha habari kwamba pametokea ajali zisizoeleweka za ndege nchini Marekani na kwamba habari kamili tutazipata kadri muda unavyokwenda. Kumaliza kusikia habari hizo simu yangu ikaanza kuita mfululizo kutoka kwa ndugu, jamaa, na marafiki waliokuwa na haja ya kunipasha habari. Nilipofika kwenye maktaba niliyokuwa nimeitwa kufanya kazi nikakuta televisheni zote zimewashwa na watu wengi wamekusanyika hayo kutazama matukio.

Moja ya mambo niliyoweza kuyabaini katika tukio lile ni jinsi watu wa zimamoto wanavyofanya kazi. Kwamba wakati watu wengine wanakimbia toka ulipo moto watu wa zimamoto wao huenda kule kuliko na moto ili kwamba wakauzime. Hili si jambo la masihara kumuona mtu anakimbilia kule wanapopakimbia wenziye.

Nakumbuka wakati wa vita vya kwanza vya Iraq kuna Watanzania waliokuwa wamejikusanya nje ya ubalozi wa Iraq pale Mtaa wa Umoja wa mataifa mkabala na Kanisa la Mt Magdalena, Upanga, ili wasajiliwe kwenda kupambana na vikosi vilivyokuwa vinaipiga Iraq. Leo katika kuranda kwenye magazeti ya Afrika Mashariki nikakutana na habari ya Waganda wanaoenda Iraq kwa hiari zao kufanya kazi za ulinzi. Hawa nao nawaona kama zimamoto ambao si kwa mapenzi ya kazi wanaenda wanapokimbia wenzao bali kwa sababu dhiki ya akili na mali wanajipeleka kuuzima moto wa Muqtada al sadr na insurgents wengineo. Habari yenyewe hiyo hapo chini:

1,600 guards head to Iraq
ANGELO IZAMA & GRACE NATABAALO
KAMPALA
THE number of Ugandans seeking jobs in Iraq continues to soar despite the prospect of working under extremely high temperatures in a country ravaged by insurgency.

The latest group cleared by the recruitment firm, Askar Security numbers 1,688. The first batch will leave on a chartered flight to the Iraqi capital Baghdad on August 15 to replace 450 Ugandans who will return home after their six-months stint there.

Yesterday Daily Monitor visited their camp on Entebbe Road. Green and blue folders, with the details of each person, were being handed over to the recruits most of them in their 20s and early 30s. The jobseekers, the agency says will be deployed to offer perimeter security to four US bases in Iraq.

“They will be handling weapons and deployed at check points, observatory towers and entry points to US camps called Arlington, Striker and the EODT headquarters,” said Mr Sisto Andama who coordinates external deployment for the company. Vijana wa kazi wakiwa wamejiandaa kuingia kazini.

EOD technology is the American company which contracts Askar to provide guard services to Iraq. The official in charge of the vetting facility, one Luke Ibudiire told Daily Monitor most of the recruits were O’level leavers.

“The ladies are relatively few compared to the men with a ratio of three to ten. We have many graduates, more diploma holders and A’level leavers too,” he said.
Exporting Ugandan labour, which is done by license from the Ministry of Labour, has attracted controversy.

There have been claims in the media of bogus agencies conning unsuspecting people of money promising them job placements in Iraq.
Sources in the industry say one firm run by a minister’s wife who was declared a prohibited immigrant by the US is operating without a license from the Ministry.

Past controversies have sucked in former Presidential Advisor Naava Nabagesera who lost her position at State House after allegations that she was involved in lining up ‘ghost’ jobs abroad. The army and police are concerned that their personnel were deserting their posts for riskier but better paying jobs in Iraq.

Askar sources say the Chieftaincy of Military Intelligence and other security agencies have access to the recruitment process to seek deserters.

08 July 2006

Mwanamke wa shoka amtolea uvivu mkufunzi wa chuo cha sanaa.

Chuo cha sanaa Bagamoyo
Kuna msemo usemao.. 'Mkombozi wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe', hii ina maana kwamba pamoja na harakati zote zinazofanywa na ulimwengu mzima katika kumkomboa mwanamke bado ni mwanamke binafsi mwenye amri ya mwisho ya kuruhusu kuonewa au kutokuonewa.

Leo nimekutana na habari iliyonifurahisha sana ya jinsi mwanafunzi wa kike wa chuo cha sanaa cha Bagamoyo alivyoamua kupambana na uonevu wa mwalimu wake. Habari yenyewe hii hapa chini:-


MKUFUNZI ABAMBWA AKILA NGONO.

Mkufunzi wa Chuo amebambwa live suruali chini, akiwa katika hatua za mwisho kukamilisha kiu ya rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake wa kike ili amfaulishe mtihani.

Soo hilo limemkumba mkufunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (jina linahifadhiwa kwa muda) ambaye kwa sasa Taasisi ya kupambana na Rushwa PCB, ishamtia ndani tangu Julai 2 mwaka huu.

Madai ya tuhuma hizo yaliibuka baada ya mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili Chuo cha Sanaa Bagamoyo, kufeli baadhi ya mitihani yake na kutakiwa kurudia masomo hayo.

Hata hivyo baada ya kuyarudia masomo hayo, mkufunzi huyo alimwita mwanafunzi mhusika na kumtonya kuwa amefeli tena somo moja na ili afaulu anatakiwa kutoa mwili wake afanye naye mapenzi kisha atafanya mpango wa kumfaulisha somo hilo.

Kutoka na ushawishi wa hali ya juu kutoka kwa mkufunzi na kuhofia kurudia mwaka mzima, mwanafunzi huyo alikimbilia PCB kuomba msaada ambao waliset mtego uliofanikiwa kumnasa mkufunzi huyo akiwa ameshalipia gesti ya kufanyia manyanga hayo akisubiria kuweka mechi kati.

Kibosile wa PCB Mkoa wa Pwani Edson Makallo alikiri kuwepo kwa kimbembe hicho na kusema kuwa mkufunzi huyo alikamatwa saa nne za usiku na sasa anasubiria kimbembe chake Mahakamani.

Rushwa ngono imekuwa kero kubwa nchini lakini ni mara chache sana wahusika wamekuwa wakijitokeza hadharani kueleza kilichotokea ili kuikomesha isiendelee.

25 June 2006

Yupi anayepaswa kutolewa bungeni?... anayesinzia kikaoni au aliyevalia??


Hapo majuzi nadhani wote tuliipata hii habari ya mbunge Amina Chifupa kutolewa katika kikao cha bunge kutokana na kofia aliyokuwa amevaa ambayo haikuendana na kifungu kimojawapo cha sheria ya bunge, hivi vifungu vya sheria bado vinanichanganya ina maana kuna vifungu vya sheria vinavyoruhusu kusinzia wakati kikao kikiendelea? nauliza hivi kwa sababu sijawahi kuona mbunge akitolewa kikaoni kwa sababu anasinzia ingawa nusu yao huwa wanasinzia. Hivi ni hadi lini watanzania tutakuwa tukiendelea kukemea mambo mepesi mepesi na kumezea mazito?

Haya habari ya Chifupa hiyo hapo chini kama hukubahatika kuisoma.


Mbunge wa CCM wa Viti Maalum, Mheshimiwa Amina Chifupa leo asubuhi amejikuta akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge wakati kikao kikiendelea.

Zali lenyewe lilianza hivi:
Kikao kilianza asubuhi kama kawaida, waheshimiwa wakaingia ndani ya ukumbi na kila mmoja kuketi kwenye siti yake.

Dua iliporomoshwa ya kuliombea Bunge na Taifa, kama kawaida na baadaye kipindi cha maswali na majibu kikaanza.

Hata hivyo ilipotimu kama saa 3:22 hivi, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Samwel Sitta akasema, ’’ Kabla ya kuendelea namuomba Mheshimiwa Amina Chifupa atoke nje akavue kofia yake,’’.

Baada ya sentesi hiyo, Spika alinyamaza kidogo halafu akaendelea, ’’Ni kwa mujibu wa kanuni za Bunge...Mheshimiwa, unaweza kuvua halafu ukarejea tena...siyo moja kwa moja’’.

Mheshimiwa Amina Chifupa alikuwa amevalia kofia ya pama nyeusi inayomechi na nguo zake.

Baada ya tangazo hilo la Spika, Mheshimiwa Amina Chifupa, alisimama na kutoka nje ya ukumbi.

Hata hivyo Spika amefafanua kuwa suti ya Ulaya ikiwa imekamilika ni ruksa kutinga nayo Bungeni.

Akasema kanuni ya 74 kifungu cha tatu ndiyo inayozungumzia mavazi ya kike Bungeni.

Hata hivyo wakati tunakwenda mitamboni mheshimiwa Chifupa alikuwa tayari amerejea ukumbini akiwa hana kofia hiyo.

24 June 2006

Milima haikutani..............


Kuna ule msemo usemao milima haikutani lakini binadamu hukutana, msemo huu ulifika mahali pake majuzi ambapo ghafla bin vuu nilikutana na wasanii wenzangu katika tamasha la muziki Mundial nchini Uholanzi. Miaka sita iliyopita hapo pichani(amekosekana msanii mmoja bwana Kalulu) tulikuwa ni kikundi kimoja "Sisi Tambala". Pia nilikutana na Mwanamke wa shoka Bi Kidude, lakini kwa bahati mbaya sikuweza kuongea naye sana kutokana na pilikapilika nyingi na muda kuwa mchache sana. Lakini kwa ufupi ilikuwa ni siku nzuri sana. Mungu awabariki wasanii.

04 June 2006

Nini ishara la hili?... Togo yachukua taji la Miss World Cup.


Kama inavyosemeka kwamba nyota njema huonekana asubuhi! basi ndivyo usemi huu unavyoanza kuonyesha dalili zake. Ikiwa ni juma moja tu limebakia kabla ya kuanza kwa sakata la kugombea kikombe cha dunia katika mchezo wa mpira wa miguu, kumefanyika mashindano ya 'ulimbwende' ya kumtamfuta mrembo wa dunia wa kombe hili. Mungu si Athumani Togo imetutoa kimasomaso waafrika. Sasa nauliza je ni nini ishara ya hili?..Waafrika tunaweza kubadili historia au bado ni ndoto?...haya watabiri karibuni tusaidiane kutabiri suala hili.

Endelea hapo chini kwa habari nzima, na hapa burudika na video ya harakati na shamrashamra na hapa ratiba kamili.

Togo wins Miss World Cup contest

Togo has won the World Cup - albeit just the pre-tournament beauty contest.
Student Edwige Madze Badakou, 24, beat representatives of the 31 other finalists to be crowned Miss World Cup.
Contestants paraded in swimwear and evening gowns for a jury which included footballers. It is not clear whether their football knowledge was tested.
Ms Badakou's victory comes after a Togolese voodoo priest predicted glory for the team, widely seen as rank outsiders, in Germany.
Maria Garrido B'aez, 23, of Spain came second, followed by Ecuador's Katty Lopez Saman, 23.
Ms Badakou, who was crowned Miss Togo two years ago, won 2,000 euros ($2,557; £1,370) and the use of a convertible car for a year.
On Thursday, Togo's chief voodoo priest predicted success for the national football team, the Sparrowhawks, at the World Cup in Germany.
"The ancestral spirits say that Togo will go far at the World Cup," Togbui Assiogbo Gnagblondjro III said.
He said that Togo would definitely beat South Korea and France to get to the next round and he would be able to predict the actual scores two days before the matches.
His prediction and Ms Badakou's victory are likely to give hope to fans angered with their players' lacklustre performance and a demand of $200,000 each to take part in the tournament.


__________________________________________________

27 May 2006

Graca Simbine Machel.


Kuna nchi nyingi sana za Afrika ambazo unaweza kuzungumzia historia zake bila kutaja wake wa viongozi waasisi wa mataifa hayo na bado historia ikakamilika. Kwa nchi ya Msumbiji kitu hicho hakipo!. Hauwezi kuelezea historia ya Msumbiji bila kumuhusisha bibi Graca Machel ambaye ni mjane wa Rais wa kwanza wa Msumbiji Ndugu Samora Machel(Mzee wa kombati)

Graca Simbine ni mwanamke mwenye hulka ya upole lakini ni mwenye akili nyingi na makini sana katika utekelezaji wa mambo yake. Ni mtu asiyekurupuka wala kuyumbishwa na mikumbo ya kijamii. Kwa ufupi ni mtu anayefanya jambo kutokana na imani yake inavyomuongoza.

Mwanamke huyu wa shoka alizaliwa tarehe 17-10-1946 katika eneo la pwani ya ukanda wa Gaza nchini Msumbiji. Akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto sita wa mzee Simbine na bibi Nelly ni yeye peke yake ambaye hakubahatika kumuona baba yake kwani alizaliwa majuma matatu baada ya baba yake kufariki. Mzee Simbine ambaye alikuwa akifanya kazi katika misheni ya Methodist hapo kijijini, aliacha maagizo kabla ya kufa kwake kwamba mkewe na watoto wake wakubwa ni lazima wahakikishe mdogo wao (Graca) anakwenda shule hadi masomo ya juu. Alipofikisha miaka 6, dada yake mkubwa aliyekuwa mwalimu alimchukua na kumuingiza shule, anasema dada yake alikuwa ni kama mama yake wa pili kwa jinsi alivyomlea vizuri na kuhakikisha anafanya vizuri katika masomo yake, na kutokana na usimamizi mzuri wa dada yake aliweza kufaulu masomo yake ya msingi na kupewa nafasi na misheni ya Methodist kwenda kusoma sekondari. Anasema akiwa sekondari ndipo alipoanza kubaini ubaguzi uliopo kati ya weusi na weupe kwani darasani kwao alikuwa mweusi peke yake kwa hiyo aliona jinsi alivyokuwa akibaguliwa na kutengwa na weupe. Lakini kama nilivyosema hapo awali kwamba yeye si mtu wa kuyumbishwa hilo la kubaguliwa halikumfanya kushindwa kuzingatia masomo yake na mara nyingi anasema jambo moja lilikuwa likimfariji kwamba hata kama alikuwa akibaguliwa lakini alijua Msumbiji ni ya kwake na si yao na wao wako kwake, hivyo alifanya masomo yake vizuri na kufanikiwa kupata tena ufadhili wa kwenda chuo kikuu cha Lisbon Ureno kusomea Lugha hiyo ilikuwa mwaka 1968.

Akiwa Lisbon alikutana na watu wengi wenye fikra mbalimbali za kimapinduzi, akasikia pia habari za FRELIMO chama ambacho kilikuwa kinapigania ukombozi wa Msumbiji. Graca akajiunga kwa siri katika chama cha FRELIMO, lakini haikupita muda mrefu serikali ya kikoloni ikagundua anachokifanya Graca na hivyo ikaandaa adhabu ya kwenda gerezani pindi Graca atakaporejea Msumbiji. Graca kwa kulijua hilo ikabidi asimalize masomo yake na kukimbilia nchini Uswisi. Mwaka 1973 akiwa bado ulaya akaamua kujiweka wazi kama mwanasiasa na mpigania uhuru wa nchi yake na mwaka uliofuata 1974 chama cha FRELIMO kilimrudisha Afrika lakini nchini Tanzania ambapo ilimpatia kazi ya kuwa mkuu wa shule ya sekondari ya FRELIMO iliyokuwa Bagamoyo, shule hii siku hizi hujulikana kama shule ya sekondari ya Kaole. Chama cha FRELIMO kilikuwa na shule nyingi za sekondari katika nchi huru za Afrika nia ikiwa ni kuwapatia elimu wananchi wake huku harakati za ukombozi zikiendelea. Akiwa Tanzania alijifunza pia mafunzo ya kijeshi ya kujilinda na ni katika kipindi hiki ndipo alipoweza kukutana na mzee wa kombati Samora Machel. Graca na Samora walianza kama marafiki wa kawaida lakini baadaye urafiki ukazidi na kuwa wapenzi wakati huo ikiwa ni miaka mitatu tu imepita tangu Samora afiwe na mkewe wa kwanza Josina Machel.

Harakati za FRELIMO ziliendelea vizuri kwani mwaka uliofuatia tarehe 25-06-1975 Msumbiji ilijipatia uhuru wake kutoka wa Wareno, mwaka huo huo Graca alifunga ndoa na Samora machel.

Kutokana na elimu yake na uzoefu wake wa kufundisha, na jinsi alivyoweza kuishika vizuri nafasi ya ukuu wa shule ya FRELIMO Bagamoyo, serikali mpya ya Msumbiji iliona haina sababu kumnyima Graca nafasi ya uwaziri wa elimu na utamaduni. Akiwa wanamke pekee na wa kwanza kushika nafasi hiyo kubwa anasema kwanza alipigwa na butwaa na kutetemeka hakujua kama ataweza kuimudu au la!...alijifungia siku kadhaa chumbani kwake akili na kujiuliza kama akikataa si ataonekana mdhaifu? na je akikubali halafu asiimudu si watasema '..unaona matatizo ya kuwapa nafasi wanawake..!!' Lakini baada ya kujufikiria kwa muda alifuta machozi na kuchukua kazi!! Lengo lake likiwa moja, kuhakikisha watoto wote wa Msumbiji wanakwenda shule. Kwa mafanikio makubwa alibadilisha kabisa hali ya elimu ya Msumbiji kiwango cha watoto kwenda shule kiliongezeka mara dufu kutoka watoto 400,000 aliowakuta alipoishika wizara hadi 1,500,000 ikiwa ni asilimia 72 zaidi.

Haya popote penye maendeleo adui hakosi kujitokeza, mwaka 1976 kikundi kidogo cha wananchi wa Msumbiji wakaunda chama cha kuipinga Frelimo kilichojulikana kama RENAMO. Chama hiki kilikuwa kikifadhiliwa na wazungu kutoka Rhodesia(Zimbambwe), Afrika ya kusini na Marekani. Wazungu hawa waliunda na kufadhili RENAMO ili kuiadhibu Msumbiji kwa kuisaidia makazi wafuasi wa ANC. Kazi ya kikundi hiki cha RENAMO ilikuwa ni kufanya uharibifu katika sehemu zote za maendeleo ambapo FRELIMO ilikuwa ikifanya mfano, ilibomoa mashule na hospitali zilizojengwa na FRELIMO, iliharibu reli na mengine mengi, jambo hili lilimtingisha sana Graca ukizingatia wizara yake nayo ilikuwa ni kati ya tageti za RENAMO. Mwaka 1984 Samora Machel alikubali kusaini mkataba na wafadhili RENAMO wa makubaliano ya kuacha kuifadhili RENAMO na FRELIMO kuacha kuipa msaada wa makazi wafuasi wa ANC. Inasemeka kwamba kwa Samora kusaini mkataba ule ni kama alikuwa akisaini mkataba wa kifo chake, kwani miaka miwili baadaye tarehe 19-10-1986 alifariki katika ajali ya ndege inayosemekana ilipangwa na hao hao wazungu wa Afrika ya kusini. Samora alikuwa akirudi nyumbani kutoka katika mkutano Lusaka Zambia.

Kifo hiki kwa Graca kilikuwa ni pigo kubwa sana. Hakuamini ilikuwa ni ajali ya kawaida alijua na alisema waliomuua mume wangu ndiyo walewale waliomfunga Nelson Mandela. Maneno haya alimuandikia Winnie Mandela wakati wa msiba kwamba "wanadhani kwa kukata miti mirefu zaidi katika msitu watakuwa wameteketeza msitu wote!! ni wale wale waliomuua mume wangu ndiyo waliomfunga mume wako.."

Kwa miaka mitano mfululizo tangu Samora Macheli afariki, Graca alivaa nguo nyeusi peke yake. Na ilipofika mwaka 1989 alistaafu wadhifa wake wa uwaziri na kujishughulisha na shughuli za maendeleo ya jamii hasa hasa watoto. Mungu si Athumani Mola akaona si vyema Graca kuendelea kuishi peke yake hivyo akamtafutia mwenzi mwingine ambaye pia ni shujaa wa Afrika Bwana Nelson Mandela. Mwaka 1998 Graca alifunga pingu za maisha kwa mara ya pili na Mandela ambaye alitengana na mkewe Winnie Mandela mwaka 1992. Winnie anadai iko siku ataongea juu ya mahusiano ya watu hawa wawili.

Graca alibarikiwa kupata watoto 7, ambapo wawili ni wa kuzaa mwenyewe na watano ni wa wake wawili wa kwanza wa Samora. Hadi leo hii Graca ameweka rekodi ya kuolewa mara mbili na marais wawili mashujaa wa nchi tofauti tena katika ndoa zote akiwa ni mke wa tatu.

26 May 2006

Anna Senkoro aachia ngazi!!


Hatimaye Anna Senkoro ameona isiwe taabu kama siasa yenyewe ndiyo hivi, soma habari hiyo hapo chini ambayo nimeipata katika magazeti ya IPP. Lakini pamoja na hayo yote bado nina swali kwake je angefanikiwa kupewa madaraka ya nchi angeweza kuzimaliza mbio?....haya endelea...

Mwanamke pekee aliyegombea Urais mwaka jana, Bi Anna Senkoro, ameng’oka kwenye chama chake cha PPT-Maendeleo na kusema siasa imemfanya ajulikane, lakini pia imedhoofisha afya yake.

Alikabidhi kadi yake ya PPT jana kwa Naibu Katibu Mkuu wa PPT, Bw. Khamis Ahmed, makao makuu ya chama mtaa wa Wibu, Kinondoni.
Akihojiwa na gazeti hili baadaye juu ya kwa nini ameachana na PPT, mwanamke huyo mlokole wa madhehebu ya Pentekoste, alisema sasa anataka kupumzika.

’’Sasa nataka kupumzika. Nimerudisha kadi leo saa 7:00 mchana. Kwenye siasa siyo vizuri kuwa king’ang’anizi,’’ alisema.

Bi. Senkoro alisema kuna baadhi ya wanasiasa, wamekuwa ving’ang’anizi na wamekuwa wakigombea Urais kwa miaka mingi na kudondoka vibaya, lakini hawataki kupumzika. Hakuwataja.

Alisema alijiunga na PPT miaka mitatu iliyopita na kwamba siasa imemnufaisha, lakini pia imemtia hasara, ikiwemo kuzorotesha afya yake.

’’Siasa imenifanya nijulikane sana na hata wewe mwandishi si umenifahamu kwa sababu ya siasa?,’’ alisema.

Alisema siasa ni mchezo mchafu na kwamba katika kipindi hicho cha miaka mitatu, amepoteza fedha nyingi na pia alipatwa na mchanganyiko wa mawazo (stress), uliomsababishia mshituko wa moyo na baadaye kumfanya apooze sehemu ya mwili.

Hata hivyo, alitamba kuwa ameachana na siasa bila ya kupata madeni makubwa, kwa sababu alijitahidi kupunguza matumizi kwenye masuala hayo ya siasa.

Bi Senkoro alisema baada ya kuachana na siasa, anarejea katika kazi yake ya awali ya kutibu binadamu.

’’Narejea katika kazi yangu ya udaktari,’’ alisema.
Alieleza kuwa kabla ya kujiunga na PPT, alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

12 May 2006

Swali kwa Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete.

Nimeamua kumuuliza swali rais wetu JK kwa vile angalau anafikika hata na akina sisi na pia nimegundua anathamini sana mawazo na maoni ya watu wa aina zote.

Ndugu rais hivi ni kwa nini:-

1. Shughuli zote za kimaendeleo ya nchi zimeelekezwa katika mkoa mmoja tu tena na tena usiokuwa na ardhi ya kutosha?


2. Hivi ingekuwaje kama awamu hii ya nne ingekita nguvu zake zote vijijini ambako ndiko kuna rasilimali kubwa ya kutosha (ardhi), hivi kweli tungeendelea kudharauliwa na kuitwa masikini?

3. Nimesikia hadi leo bajeti ya Tanzania inaandaliwa na nchi za magharibi, jamani hivi kweli bado hatujaweza kuandaa bajeti yetu wenyewe? kama bado hatujaweza ni kwa nini hasa?

Ni hayo tu niliyokuwa nayo yanayoninyima raha ya rohoni.

08 May 2006

Da' Mija na wanawake wa shoka yafunga mwaka!!

Shukrani hoi hoi na vifijo vimuendeee ndugu Ndesanjo Macha popote pale alipo kwani kama si yeye leo hii nisingekuwa naandika haya ninayo yaandika. Ndesanjo ndiye aliyenikurupua huko nilikokuwa na kusisitiza kwamba ni lazima nifungue blogu, nilikwepa kwepa lakini wapi jamaa alikuwa na mimi tu mwishowe nikaona ngoja nikate shauri na leo hii nayaona matunda yake. Sio siri ufahamu wangu sasa umeongezeka-ongezeka.

Labda niwapeni kisa kizima cha Ndesanjo kunibabatiza. Nilikuwa katika harakati zangu mtandaoni mara nikakutana na blogu ya Jikomboe, kuangalia vizuri naona Ndesanjo Macha..nikajiuliza huyu mtu huwa namsikia sikia ngoja nione anafanya nini na humu mtandaoni, basi nikaanza kumfuatilia na kwa kweli makala zake zilinitia nguvu sana nikajisemea peke yangu..'haiwezekani huyu mtu lazima nimjue zaidi'.. basi siku moja nikaona nimtupie kaji-swali ambako kanaonyesha niko kinyume na yeye yaani kama mpinzani wake nione atajibu nini!.. mara nyingi mimi nikiona mtu anafanya vitu vizuri hupenda kujua na anapokoselewa hupokeaje hali hiyo? Wee! nilipata jibu hilo mwenyewe nilitulia bahati mbaya nimesahau hata jibu lenyewe labda kama Ndesanjo unalikumbuka. Basi kuanzia hapo Ndesanjo akajua huyu mtu yuko kinyume na mimi kwa hiyo akawa amekaa mkao tayari tayari, mimi sina hili wala lile siku moja nikatoa maoni katika habari fulani ya "Nimtume nani" nikamwambia labda umetumwa wewe kwani Mungu haangalii mtu fulani ili kumtuma". Sasa hapa nikamchanganya kidogo kwamba huyu Da'Mija yuko upande upi? yuko upande wangu au ananidhihaki?... akanipiga swali Kwani wewe kwako Mungu ni nini au ni kitu gani?? Duh! nikaona haya tena mengine...kaka yangu hapa hakunielewa lakini na mimi sikufanya ajizi nikamuelewesha Mungu ni nini, ni nani kwa jinsi nilivyokuwa nikimuelewa. Baada ya maelezo hayo ndiyo akasema wewe binti ni lazima ufungue blogu yako. Basi nikaona huyu Ndesanjo lazima atakuwa ametumwa na kwangu mimi pia. Hivyo nikafungua blogu yangu. Hadi sasa hivi ingawa sina data kamili, lakini ninaamini huyu bwana ndiyo ameweza kushawishi watu wengi zaidi kufungua blogu zao. Ubarikiwe Ndesanjo, tubarikiwe wanablogu wote.

04 May 2006

Boyz 11 men sasa kiboko!!


Haya tena, ahadi ndio zinazidi kumiminwa na uongozi wa awamu ya nne. Hivi majuzi wakati wa sherehe za mei mosi ambapo kitaifa zilifanyikia Shinyanga Ndugu rais ameahidi kushughulikia suala zima la mishahara, sasa sijui ni ya kweli au la! na ni kwa kiwango gani itaongezwa bado sina hakika.. MtiMkubwa kaniletea hii habari hapa ili wote tushuhudie hizi ahadi. Soma habari yenyewe hapo chini...



2006-05-02 16:53:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Rais Jakaya Kikwete na Waziri wake Mkuu, Bwana Edward Lowassa, marafiki ambao watoto wa mjini waliwahi kuwaita Boyz ll men, wamewadhihirishia Watanzania kwamba hawana mchezo na wamepania kuboresha hali za Watanzania.

Rais Kikwete alidhihirisha hilo jana wakati anahutubia mamia ya wananchi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, Rais Kikwete, sherehe zilizofanyika kitaifa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage.

Katika hali ambayo inaonyesha Rais amepania kutofanya mambo ya danganya toto katika uongezaji wa mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi, alitangaza mikakati kadhaa.

Mosi: Alisema ataunda tume itakayotoa hali halisi ya maslahi ya watumishi iliyopo Serikalini na kwenye mashirika ya umma.

Rais alisema tume hiyo pamoja na mambo mengine, itashughulikia uchambuzi wa mishahara na maslahi ya watumishi hao.

Kwa mtaji huo, ’watemi’ Serikalini na katika mashirika ya umma ambao siku zote wanapigania kuongezwa kwa maslahi yao wenyewe, sasa wataumbuka.
Pia madaraja makubwa ya watumishi walionacho na akina pangu pakavu tia mchuzi, yataondoka.

Na kwa upande mwingine, watumishi wasio na nafasi ambao hali zao zimedhoofu kutokana na maslahi duni, watatamba katika uwanja wa haki na usawa.

Rais Kikwete alisema tume hiyo ataitangaza rasmi wiki ijayo na anataka kabla ya mwaka huu kuisha iwe imemaliza kazi hiyo.

Alisema mara baada ya Tume kumaliza kazi na kumpa mapendekezo, hataweka usiku na badala yake atayashughulikia mara moja na kutoa uamuzi juu ya hatua za kuchukua.

Pili: Rais ametaka Mabaraza ya Kisekta ya mishahara ya Kima cha Chini cha mishahara yaundwe mengi ili kushughulikia maslahi ya kundi hilo.

Kwa mtaji huo, kilio cha muda mrefu cha walalahoi huenda kikapungua.
Kwa muda mrefu, wafanyakazi wa kima cha chini wamekuwa wakilalamika kwamba ’wako jangwani’ kutokana na maslahi duni.

Tatu: Rais alisema suala la ajira amelishikia bango na kwamba mikakati inakamilishwa na muda si mrefu Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana italifahamisha Taifa.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuongeza ajira kwa Watanzania na kwamba imedhamiria kuweka mazingira mazuri ambayo yatawezesha kukuza ajira nchini ili Watanzania wanufaike na kupunguza dhiki ya maisha.

Nne: Rais pia alizungumzia suala la kuajiriwa kwa wageni katika nafasi ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania.

Alisema Serikali itakuwa makini na yenye ukali kwa ajira za aina hiyo.
Kwa kauli hiyo, malalamiko yaliyozagaa kwamba kuna Ma TX feki wanafanya kazi ambazo hata Wabongo ambao hawakwenda shule wanaweza kuzifanya, yatapungua.

Wananchi mbalimbali walioongea na gazeti hili kuhusu hotuba ya Rais walisema serikali ya awamu hii ni kiboko na kama yote yaliyoahidiwa yatatekelezwa, hali za Watanzania zitainuka.

27 April 2006

Eti siku ya mtu kuzaliwa ni ya nani?..mama au mtoto?


Pichani juu ni mimi na kaka yangu na chini ni mzaa chema.

Hapo kipindi cha nyuma nilipata kuzua mjadala na mshairi maarufu wa kikundi cha Parapanda Mgunga mwa Mnyenyelwa juu ya hasa ni nani mwenye haki ya kuiita siku yake, je ni mama au mwana? kwa mujibu wa Mgunga anasema siku ya mtu kuzaliwa ni haki ya mama na kama ni sherehe au pongezi zote anayetakiwa kupewa ni mama. Hili nimelikumbuka leo kwa vile ni siku yangu ya kuzaliwa..., haya wewe unasemaje? ni nani anayetakiwa kupewa pongezi katika siku za kuzaliwa?

"Unapokuwa mwanamke mweusi duniani..." Hotuba aliyotoa Winnie Mandela Chicago Marekani.


Mwezi uliopita Winnie Mandela kwa heshima zote alialikwa na jamaa wa V-103'Expo huko nchini Marekani (Chicago) kuhutubia juu ya Nafasi ya mwanamke mweusi duniani, Winnie aliandaa hotuba nzuri sana lakini tofauti na matarajio yake watu waliacha kumsikiliza na kwenda kuangalia maonyesho mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika ukumbi huo na yeye kutokana na utovu ule wa nidhamu akaamua kukatisha hotuba.

Ni hotuba nzuri na sana nimeona niwawekee hapa ili wote tuisome. Mwandani asante kwa kuniletea habari hii nimeona si bora kuifaidi peke yangu.

14 April 2006

Bibi Mohamed!..Mwanamke wa kwanza nchini kushika madaraka ya uwaziri. Hongera MtiMkubwa kwa kutegua.




Kwanza niwashukuru wachangiaji wa mada hii, na pia tumpigie makofi ya pongezi MTIMKUBWA Tungaraza kwa kutegua kitendawili hiki mapemaaa! Huyu jamaa ana kumbukumbu za karne. Pia ninamshukuru bwana Michuzi kwa kuibua mjadala mwingine juu ya kina mama na uongozi katika vyombo vya habari, binafsi nilikuwa bado sijaanza kuifuatilia nyanja ya Habari na nafasi ya wanawake katika kuviongoza vyombo hivyo..."Raha ya blogu jamani".

Haya, Bibi Titi Mohamed alikuwa si mwanamke wa kwanza tu kushika nafasi ya uwaziri nchini, bali pia ni mwanamke wa kwanza aliyejitolea kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana bila kukata tamaa pamoja na kwamba alikubwa na misukosuko mingi. Hapa kuna habari kamili ya jinsi alivyojiunga na harakati hizi za ukombozi. Habari hii aliitoa yeye mwenyewe miaka michache kabla ya kufariki kwake. Na hapa kuna orodha kamili ya mawaziri wanawake wa Tanganyika na Tanzania.

Shujaa Bibi Titi alifariki 5/11/2000 katika hospitali ya NETCARE Johannesburg Afrika Kusini.

09 April 2006

Unamfahamu mwanamke wa kwanza kuingia katika baraza la mawaziri la tanzania?


Pengine kuna haja ya kuwajua mashujaa wetu wa kwanza kabisa waliojitolea kwa mioyo yao yote kuipigania nchi yetu. Wako wengi ingawa leo hii wanasikika wachache tu. Swali langu au tuite mtego wangu wa leo ni kumtaja mwanamke wa kwanza kuingia katika baraza la mawaziri Tanzania wakati huo ikiwa ni Tanganyika na je ni ipi nafasi yake leo katika Tanzania yetu, je anaenziwa kama kina Karume na Nyerere hadi kupewa siku za mapumziko? Kumbuka enzi hizo hadi uweze kushika nafasi ya uwaziri ni lazima harakati zako za kupigania uhuru zilikuwa na za kiwango cha juu.

JE MWANAMKE HUYU NI NANI?

31 March 2006

Lakini hii si ndio Bongo jamani??

Swali linalobeba kichwa cha habari hii lililetwa na bwana Ramadhani Msangi ambaye naye alilipata kutokana na habari iliyoletwa na bwana MtiMkubwa inayosema.. "Aliyenacho ataongezewa..."

Habari hii imezua mjadala mkubwa juu ya nchi yetu na ulinzi wake, juu ya uzembe unaochukuliwa na viongozi mbalimbali duniani hata kama wanapata tahadhari ya uvamizi wa kigaidi. Mijadala ya namna hii mimi huipenda kwa vile huibua mambo ambayo labda hata hatukuwa tukiyafahamu. Ndugu zanguni hili swali la Msangi Mdogo kwangu mimi nalitafsiri kama kwamba hali hii tumeona haiwezekani tena kubadilika, ni kama tumeihalalisha vile... hebu tusome kwanza haya maoni yaliyoletwa na baadhi ya wasomaji halafu tuendelee kutafuta ufumbuzi....kwa kweli halali mtu hadi kieleweke...

MK ......
Kwanza kabisa nakuunga mkono ndugu muandishi wa hii nakala kwa yale yote ya kweli uliyo yasema hapa.

Tanzania na nchi nyingi za Africa mara nyingi hawafuati sheria na katiba za nchi zao kwa kutenda haki kwa raia wao. Ikitokea Kiongozi yoyote yule kusema lolote ili mradi matakwa yake yafuatwe basi kweli lolote lile litatendeka ata watu kufa watakufa.

Ktk nchi yetu ya Tanzania mtu ukiwa masikini basi haki zako zile za msingi utazikosa kwa kunyanyaswa kila kona toka kwa majirani zako, kutoka ktk vyombo vya ulinzi, kupata huduma ktk ma-hospitalini, makazini na mashirika ya umma. Hii imeoneshwa mara kwa mara kwa baadhi ya wanajeshi wetu kupiga raia pale wanapojisikia au kwa kitendo hicho kilichotokea na watu kufa.

Ktk yale yote yaliyotokea na watu wawili kufa ni uzembe wa Serikali yetu kwa kutotoa (kuto-kutengeneza) nafasi nyingi za kazi kwa raia wote ndani ya nchi. Kama kila raia angekuwa na kazi itakayo muezesha kupata ridhiki yake basi haya yasingetokea kwa maana hawa ndugu zangu wangekuwa na mahali pa kufanyia shughuli zao na kujipatia riziki.

Kama haiwezekani kwa kila mtu kupata kazi basi kwanini hawa watu wasiweze kuhalalishwa na kuendelea na kazi zao kama wapiga debe.
Serikali haitoi kazi kwa raia lakini utakuta kila siku wanawasumbua wamachinga ambao wamejitaidi na kujianzishia maisha yao kwa kufanya biashara!Kweli hii inatia hasira sana.

Sijui wana maanisha nini kwa raia! Mimi sio siri nina kerwa sana na mengi yatokeayo Africa na Tanzania.

Baadhi yao hawawezi kuelewa haya mambo (shida) maana wao wamejilimbikizia utajiri mwingi kutokana na rushwa na kuiba pesa za Taifa.Ukweli na ushaidi upo!!

Wengi wa Viongozi wetu hawapo ktk kulitumikia Taifa na wananchi wake bali wapo kama ktk Biashara ili wajitafutie utajiri wao na familia zao na hii imeoneshwa kwa wao kununua nafasi za kugombea Ubunge au kila siku kugombea nafasi moja tu, n.k. na kutoa rushwa kwa raia ili wachaguliwe na wengine ata kuiba kura.Ukweli umeoneshwa kwa wao kuomba kuongezewa mishahara.

Kwa kweli inatia hasira sana, Cha msingi na la maana ni kwa mimi na wewe (wasomaji) kuweza kugombea hizo nafasi zao ili tuweze kusimama na kutetea masilahi ya Taifa na wananchi wake.
Kama mnataka mnabidi mpitie CCM maana kama ukienda Upinzani ni kama unajipotezea muda wako maana wapinzani wote ni kama CCM Pretenders wanao danganya raia.Ushaidi upo!

Kuhusu jeshi kunyanyasa raia hawawezi kulizungumzia hili swala maana wengi wa Viongozi wanaogopa kupinduliwa!

Tanzania kuwa kama Wasierra Leone au Waliberia au nchi kupinduliwa kutokana na wananchi ni Vigumu sana tena sana maana kuna watu wapo masaa 24 ktk kulinda nchi hii. Labda itokee kwa genelari wajuu sana kufanya hivyo na vile vile ni vigumu maana wanajeshi wote wenye vyeo vya juu waliostaafu na wale wapo kazini wanafuatiliwa mienendo yao ya kila siku in details hivyo itajulikana tu kabla ya wao kufanya hivyo.

Kingine vyombo vyetu vya Ulinzi vinapata mafunzo toka Canada, China, USA, UK na kidogo Russia, na nchi zinginezo hivyo wao utoa mafunzo ya hali ya juu ya kuzima mapinduzi ktk nchi kwa maana hiyo ata kama yakitokea nina uhakika zaidi ya asilimia mia mbili (200) yatazimwa chini ya masaa 24.

Ninacho mshukuru Mungu Taifa letu limebalikiwa na Amani ambayo itadumu milele. Kingine, Amani ndio itakayo fanya mimi na wewe au kizazi chetu kiendelea hivyo tudumishe Amani yetu tuliyo nayo.

Ingawa kuna Viongozi wabaya lakini kuna wengi wazuri.Inatia hasira sana lakini tuwe na moyo na JKM maana kuna mengi yatakuja na haya yaliyotokea hayatatokea tena.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.


michuzi......
naomba nichangie kwa kuwa sina upande katika suala hili, kwani kwa mujibu wa maono yangu, nadhani kila upande unastahili lawama.

nikianza na serikali: hivi kuna ubaya gani kuweka sera ya wazi kuhusu biashara ndogondogo na wafanyaji wake? Kuna ubaya gani kuiga wenzetu ughaibuni kwa kutenga sehemu maalumu za kufanya biashara hizo, na sehemu hizo ziwe zinafikiwa kirahisi na sio kama hivi sasa pale karume ama mwenge. nimeona sehemu kama stockholm wana soko la mchana katikati ya jiji, helsinki pia, berlin nimeona pia hali kadhalika london na johannesburg, kuna masoko ya mchana kwa holoi poloi, lakini hakuna ruhusa kufanya biashara popote kama ilivyo dar, kiasi inatia kinyaa.

Kwa machinga: hivi nani kawaambia kuwa mradi wao walipiga kura kuitia ikulu serikali iliyo madarakani maana yake wafanye watakavyo hata kama ni kinyume cha kanuni? kwa nini wanakuwa wabishi na kuwafanya halmasahuri ya jiji waonekane wanawaonea, kuchoma chipsi na kuuza mashati kila sehemu katikati ya jiji? ni kweli wote wanastahili sehemu kufanyia bizness, lakini ni kila sehemu jamani? mtimkubwa na wengineo hebu rudini muone ilivyo shida kukatiza mitaani dar kutokana na vibanda vya biashara na machinga. sisemi nawachukia,ila kama ni maendeleo yaje kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu kama anavyotoa mtimkubwa.

nasema haya sababu hata hii serikali imeyaona hayo na ndo maana imesitisha (haijakatisha) kwa muda wa miezi 6 zoezi la safisha jiji, ila baada ya hapo hakuna maslie. lazima barabara iwe barabara na vibaraza viwe hivyo. we umeona wapi chupi zikauzwa kwenye kibanda cha kituo cha basi? sipendi kuweka picha kama hizo bloguni
kwani nadhani si vyema kila mtu duniani akaona aibu yetu.


F MtiMkubwa Tungaraza...
Muhidin,

Maelezo yako yamenikumbusha fasihi ya kidato cha tatu kitabu cha Ngugi wa Thiongo, This Time Tomorrow. Aibu ya serikali ni kuwa na wauza vyupi katikati ya jiji! Hii mipango ya kuwakarahisha wananchi haikuanza leo: wengi wetu bado tunakumbuka sana halahala za polisi, mgambo, na JKT wakati wa zoezi la kuwahamisha "wazururaji" toka Dar es Salaam kwenda Geza Ulole, Kibugumo, Mwanabilato, Chanika, Chamanzi, Msanga, Mkuranga, Kigamboni na kwingineko koote kwenye makao mapya. Baada ya zoezi hilo likaja zoezi la NGUVU KAZI wananchi wakakarahishwa tena. Akitokea mchunguzi wa mambo ya kijamii (social researcher) kuja kufanya tathmini ya miaka ishirini hadi thelathini baada ya mazoezi hayo sijui kama kutakuwa na matokeo ya mafanikio.

Uchafu kwa fasili yake ni kitu chochote kilichopo mahali pasipohusika. Kama kweli tunataka kusafisha jiji letu kwanza tuanze na kujenga tabia ya usafi miongoni mwetu (personal hygiene). Usafi huu utafanikiwa kwa kuwa kila Mtanzania kujua maana afya bora; kuwa na uwezo wa kula vizuri, kunywa maji safi, kulala mahali pazuri, kuvaa nguo na viatu vizuri, kuweza kununua mswaki na dawa yake. Haya yote yatawezekana ikiwa kama kutakuwa na na uwezo wa kila Mtanzania kuwa na kipato cha kutosha kukidhi mahitaji yake ya kila siku. Kiapto hiki kitapatikana ikiwa tu kama tutaweza kubuni na kuendeleza ajira.

Halafu tukimalizana na suala la usafi binafsi tushughulikie usafi wa mazingira yetu (environmental cleanliness). Uchafu wa mazingira si tu kuwepo kwa Wamachinga katikati ya jiji pia kuwepo mifugo kama kuku, bata, ng'ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo katika maeneo ya wanayoishi watu. Nadhani kwa upande wa ufugaji wa wanyama kama ng'ombe, mbuzi, nguruwe na kondoo haupo mitaa ya Kariakoo, Ilala, na Temeke bali Kimara, Mbezi Shamba na Mbezi Beach, Oyster bay, Msasani, Masaki ya Uzunguni siyo Uzaramoni, Kinondoni, Upanga, Sea View, na Mikocheni zote mbili A na B. Hapa ndipo utakapoona aliyenacho ataongezewa. Mkurugenzi wa Jiji ukimshauri atume vijana wake wakabomoe mabanda ya mifugo yaliyopo hizo sehemu nilizozitaja ndipo utakapojua makali na ubutu wake upo wapi.

Hoja ya nguvu na nguvu ya hoja. Nakumbuka katika masaili fulani Bob Marley alisema "..facts 'n' facts is whole lotta o' bullshit.." Wamesitisha na hawakukatisha. Sawa! Kwa nini kabla ya kufikia hatua ya kutekeleza hilo zoezi hawakutathimini mazuri na mabaya yake (pro and cons)? Wanaelimu ya jamii (sociologists), wachumi (economists), au washauri wengine wowote wa serikali wa mambo ya jamii hawakushirikishwa kuitahadharisha serikali juu ya intended consequencies, latent consequencies, na unintended consequencies za zoezi hili?

Rais Nelson Mandela kwenye shajara yake ya Long Walk to Freedom anasema "..ukitaka kuijua serikali nzuri usiangalie inahusiana vipi na raia wake wa juu bali angalia jinsi inavyohusiana na wafungwa wake walio jela.." Haya mambo ya kuikimbiza na kubomoa biashara za watu mijini ni uonevu, unyanyasaji, na dhuluma dhidi ya Watanzania masikini. Kama kweli kuna zoezi la safisha jiji basi lisiwaache na wafugaji wa Oyster Bay, Kinondoni, Ada Estate, Regent Estate, Upanga, Sea View, Mikocheni A na B, Msasani Peninsula/Masaki, Mbezi zote mbili, Kimara, na kwingineko kokote kusikostahili kuwepo mifugo.

Mungu Ibariki Tanzania,

KABLA SIJAACHANA NAWE NAOMBA UIMBE KWA SAUTI WIMBO HUU WA MAREHEMU MAKONGORO:

"Mpango wa pili wa maendeleo umesema kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa, na kujenga nyumba safi pakulala pawe bora!"HAYA YOTE YATAPATIKANA VIPI SIJUI?


John Mwaipopo...
Awali ya yote nilidhani wasafwa wako Mbeya kumbe wako Kilombelo (mchomekeo tu msijali sana)

Pili nichangie kidogo juu ya maslahi ya wabunge na madaktari. Mosi vyombo vya habari vilitupotosha kuhusu hili. Ingawaje sikubaliani na mapendekezo yao ya kutaka kupanuliwa maslahi, vyombo ya habari vilichukulia lile suala kama kikao rasmi ambacho kilikuwa na ansard na minutes. Kumbe yale yalikuwa mawazo ya wabunge binafsi wawili au watatu. Pengine miongoni mwa wabunge wapo ambao walikuwa na mtazamo tofauti. Wanamtandao wakaleta kwetu kana kwamba lile lilikuwa azimio la wabunge woote - Irresponsibe journalism.

Hata hivyo wabunge kama watanzania wengine walikuwa na haki ya walau kuyasema wanayostahiki kuyasema.Madaktari nao walikuwa na haki kudai walichokuwa wakidai. Kosa lao lilikuwa approach. How come wasababishe vifo kwa kugoma kufanya kazi. Ukiwa muhandisi unafikiri kila tatizo linatatuliwa na nyundo. Sivyo. Serikali ilikuwa sahihi kuwaadabisha kama ilivyofanya. Kwa nini hawakutumia power of compromise from different angles. Kizuri hapa hata serikali ilikuwa inatambua madai yao kuwa ni halali. They had no right to cause deaths to innocent and poor patients. Who stopped them from going anywhere around the world to seek greener pastures? Hapa inakuonyesha walikuwa wanatikisa kibiriti tu huku fika walikuwa wanaujua uwezo wa serikali yao.

Michuzi umechambua pande mbili ki ufasaha sana. Huria si holela.Really wamachinga are causing nausea in the 'beautiful' city. Lakini wa kulaumiwa sana hapa ni Serikali, na katu si hawa holoi poloi (asante kwa msamiati huu). Imekuwa iki-react too slowly and unprofessionally. Yenyewe ndio inatakiwa iwe chachu ya uendeshwaji wa shughuli zoote nchini. Mathalani kuhusu suala hili ingeweza kuweka kodi kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa wa city centre wanaouza bidhaa sawa na zile za wamachinga. Hii ingewafanya ama waache kufanya biashara hii au ama wafanye kwa asara zao. In the meantime, wamachinga ambao wangetengewa sehemu inayofikika wangeondolewa ama kupunguziwa kodi. Niambie mnunuzi asingeweza hata kwenda mathalani Jangwani (sio kwa Yanga).

Suala ninalolipigia upatu na chapuo bila kusita ni hili alilolileta Mti Mkubwa Mkavu Mnene. Safisha safisha ikirejea ianzie kwa wafugaji wa ng'ombe na mbuzi wa Mbezi beach, Masaki, O'bay na Sea View. Mpango wa kuonea samaki wadogo ufe.


mark msaki
nianze na bwana MK usiogope habari ya kufundishwa Urusi. inapokuja suala la living and death, hapo hakuna shule inayotumika. tunapoona nchi zimekuwa na migogoro miaka nenda miaka rudi haina maana kuwa hazikuwa trained kwenye system zake za usalama...unapoongelea suala la amani sijui uko serious au unakoleza mada! hakuna amani kwenye njaa...tuendako ni kwa kuwa makini zaidi maana utandawazi hauruhusu kucheza bao na kupata chakula!! unatoka mzigoni, unapita dukani kununua msosi wa siku hiyo...funga kazi.

Michuzi umesema ukweli na umekuwa fair kuongelea pande zote mbili. kuna swali moja waliuliza juzi wana ?DHW "hivi mnakuwa mmejichimbia wapi?" mtu kupandisha maghorofa wakati maafisa wa ardhi wa sehemu husika wapo...... au kuacha watu wajenge vibanda ili uje wafukuze baadaye...hii kimsingi kwa sehemu kubwa huainisha serekali isiyowajibika...

Mti mkubwa ambao ni mkavu ameainisha kila kitu. kurudia ni kujaza ukumbi wa Da mija bure!! kwa kuongezea mimi ninaona ni ajabu kweli kuwa kila mtu anataka kujibanza DAr...mbona hao wamachinga wakionekana mkoani ni dili? kuna kitu si sahihi - (naona Jk ametoa changamoto Arumeru kuwa mikoa ya pembezoni iangaliwe)....

Mwaipopo mengi ya msingi umeyasema..lakini ukiangalia kiundani zaidi, haina maana kuwa ng'ombe anayekupa maziwa zaidi ndio umuhukumu majani kidogo zaidi...reaction ni reaction...sema matokeo yake ndio huwa tofauti..ina maana mfano kama wabunge wangegoma asingekufa mtu...kufa mtu kwa mgomo ni gauge ya kuonyesha kuwa hiyo fani ni sensitive....japo sisemi kuwa nyengine sio, lakini sensitivity hutofautiana. sipingi maslahi ya wabunge, lakini pia siri ya kuwasahau watendaji pia ni ya kujibu....nimeona waheshimiwa wabunge wameliona hilo na juzi walipigia kelele hazina kulikoni na maslahi mabovu!!! myonge mnyongeni lakini haki yake mumpe....ukichunguza sana suala la wabunge na maslahi lilikolezwa na la ishu ya madaktari ambayo ilitugusa wengi lakini tukabaki kuugulia na kulalama.....


Mk...

Ndugu Mark Msaki sio kwamba naogopa kufundishwa Russia bali hii ndio facts ambapo ukweli wake utaoneshwa pale hilo tukio likitokea.

Vyanzo vya ulinzi vinavyolinda Taifa hili vina macho makubwa ndani ya nchi na nje ya nchi sasa sijui hizo silaha utazipitisha wapi kufanya mapinduzi hayo?

Au wananchi kutumia silaha za jadi ambapo watatwaa eneo gani na kusema ndio nchi wamechukua?

Wanajeshi wetu wapo tayali ktk matukio kama hayo ambapo narudia tena nina uhakika wa zaidi ya asilimia mia mbili (200) yatazimwa chini ya masaa 24.
Nadhani bwana Michuzi atakuwa na marafiki zake wengi wa namna hii (wanao linda taifa hili ndani ya nchi na nje ya nchi) ambapo ukiwauliza watasema kama ninavyosema.(Inategemea maana kazi hii ni kama mtoto, unakula kutokana na umri wako = Unajua mengi kutokana na nafasi yako na kitengo chako)

Mataifa mengi ya Africa unayo yaona yana matatizo ya Vita, Sio kwamba Vita hiyo imeanzishwa na mtu mmoja bali imeanzishwa ktk kushirikiana na Mataifa mengi zaidi ya Africa na ya nchi za nje kwa kudhaminiwa kipesa, wanajeshi (watu kufundishwa na ata kununua au kukodisha wanajeshi wale waliostaafu kutoka ktk Mataifa mengine mengi ya Africa), silaha n.k.

Naomba angalia hili swala kwa undani zaidi utaona ninayo sema.
Mfano: Sir Mark Thatcher na mataifa mengine yaliyotaka kuleta mapinduzi Equatorial Guinea lakini kutokana na Good Intelligence report iliyopatikana kutoka kwa mataifa mengi mbalimbali ya Africa yaliweza kutoa habari kwa Serikali za South Africa,Equatorial Guinea,Zimbabwe, na mengi yaliwezesha kwa Sir Mark Thatcher na wenzake wote kukamatwa na mapinduzi kuzimwa kabla ya kutokea.

Sasa Tanzania tuna macho ya kuona Adui kama Binadamu na Adui kama Taifa lolote litakalo kuwa na mawazo ya kupindua nchi yetu na pale tunapofahamu tunazima hiyo mission yao kabla ya tukio kutokea.

Ndio maana ninakwambia Taifa letu kutokea mapinduzi ni vigumu sana, Hii sio kwamba ninazungumza kufurahisha jamii au kukoleza mada la hasha ninazungumza kwa kile ninachokijua kwa undani zaidi.
Tanzania ni moja ya mataifa ya Africa yaliyokuwa na watu waliokuwa na mafunzo ya namna hii (ya hali ya juu) pamoja na jinsi ilivyotawanya macho yake ktk kulinda Taifa hili Kubwa la baadae ulimwenguni.

Mwisho, Vita zote unazoona Congo, na mahali popote pale Africa ni mikono ya Mataifa mengine ya Africa, Mataifa mengine nje ya Africa kupitia raia wa ndani wa nchi husika na wakimaliza wanachotaka toka kwako (Interests kuisha) wanakuua au ku-support mtu mwingine na Vita inaendelea tu upya.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.


ndesanjo...
Kuna jambo Mti kasema aliulizwa na ofisa wa sirikali. Ofisa huyo alitaka ushahidi wa unyama na ukiukwaji wa haki za binadamu. Watwawala wetu wanapenda sana kukimbilia hilo neno, "ushahidi." Mkapa kuna wakati aliviambia vyombo vya habari/uongo vitoe ushahidi kuwa sirikali yake ina wala rushwa. Kitendo cha kiongozi wa sirikali kutojua kuwa vyombo vya dola Tanzania mara nyingi hunyanyasa wananchi na haki za msingi hukiukwa bila woga wowote kinaonyesha kuwa huyo bwana anatakiwa aongozwe na sio aongoze. Hata Mkapa nilimshangaa sana...rais mzima hajui kuwa amezungukwa na wala rushwa anataka wandishi wa habari wampe ushahidi. Keleuwii!


Ramadhani Msangi...
Lakini hii si ndio Bongo jamani??


F MtiMkubwa Tungaraza...
MK,

Nashukuru sana kwa maoni yako.

Imani ya kwamba pale nyumbani pako salama na pana walinzi ni nzuri lakini tusilale mlango wazi. Nina maana hata kule kwenye vyombo vya usalama vyenye nguvu na ujuzi kuliko vyetu imewezekana kufanya matendo ya kigaidi na kuingizwa silaha! Kwa mifano hai ni September eleventh, milipuko ya mabomu ya IRA, milipuko ya mabomu Israeli, Moscow, Madrid, Ufaransa na kwingineko sembuse Tanzania ambako kitengo cha makonteina bandari kimebinafsishwa pia tumezungukwa na vita Uganda, Burundi, na Kongo. Kongo inaweza kuwa bonge la kichochoro cha kupitishia silaha kuingia Bongo!

Audhu billah hima shetani rajimu, Allah karim! MUNGU ilinde Tanzania.


MK said...
Ninafuhahi kwa kuweza kubadilishana haya mawazo ya ukweli bwana F MtiMkubwa Tungaraza.

Tuanzie 9/11, Kabla ya kumaliza muda wake wa Urais bwana William Jefferson "Bill" Clinton aliweza kupelekewa memo toka CIA na FBI ya kwamba ndani ya USA kuna uwezekano wa kutokea shambulizi kwa kutumia ndege.

Pia CIA iliweza kuitaharifu FAA (Federal Aviation Administration) kuhusu hili swala lakini kutokana na uzembe mmoja au mwingine walipuuza.

Kingine wakati ule CIA na FBI walikuwa hawana uhusiano mzuri wa kubadilishana habari na hivyo kushindwa kuzima hilo tukio.Matokeo yake baadae kiliundwa kitu kinachoitwa Homeland Security chombo kinachoweza kujumuisha intellegence oficials wote toka ktk vyombo vyote ndani ya USA.

Kwasasa hivi anga na Bandari za USA zinalindwa masaa 24 pia kwa ku-scan kila nyumba kuweza kujua kama kuna watu wenye kuleta ujuma.Pia Asilimia kubwa za Computers, simu za ndani ata mobile wana zi-bug ili kusikiliza simu zote za ndani na nje ya USA.

Kwa kifupi 9/11 kilikuwa kitu kinajulikana bali ni uzembe tu wa kiubindamu ulio fanya kutokea.
Mungu awalaze mahali mema peponi Amina wale wote walio patwa haya matatizo.
Kuhusu swala la Israel ni gumu sana maana kuna mataifa toka nje yanayo dhamini hao magaidi na kuua roho za watu wasiokuwa na hatia.Na ndio maana mara kwa mara Israel imeweza kuyashambulia hayo mataifa kwa maneno na Kijeshi.Mataifa hayo ndio juzi tu walimuua waziri mmoja ndani ya nchi moja iliyo karibu na Israel ili nchi hiyo isiwe na Amani (Irudie vita). Sitaki ni yaseme hayo mataifa hapa.

Kuhusu mabomu Moscow ni magaidi wanao toka Chechnya wanafanya hivyo kwa madhumuni ya kuendeleza propaganda ya hiyo state ili iweze kujitenga toka Russia. Kumbuka mwaka 1991 wakati USSR ilipo vunjika mataifa mengi ya muungano yalijitenga ikiwemo Chechnya lakini Russia imekataa kwa hilo swala na mpaka sasa hakuna Taifa linalotambua Chechnya kama nchi bali inatambuliwa kama moja ya state ndani ya Russia.

Ufahamu ya kwamba hawa ni magaidi ambao wengine wanatoka nje nchi na kuingia Chechnya pia wanao husika sio kikundi cha watu mia au elfu moja bali ni watu wengi sana ambapo wana pesa, Silaha na n.k na pia wanapata pesa toka kwa watu au mataifa mengine yanayotaka Russia ipungue nguvu.Russia haiwezi kukubali hili swala kutokea ndio maana serikali ya bwana Vladimir Vladimirovich Putin inapeleka majeshi na ata kuweka budget kupigana hii vita kulinda ardhi yake isipotee kama ardhi nyingine zilizopotea mwaka 1991(Armenia, Azerbaijan, Belarus, Georgia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Russia, Tajikistan, Ukraine, Uzbekistan na Turkmenistan).

Nina uhakika Russia itashinda vita hii kwakuwa nguvu wanayo, sababu wanayo na silaha wanazo.

Kuhusu Madrid, Kwanza naomba nikueleze ya kwamba Tarehe 24/03/2006 ETA imeweza kuweka mkataba wa amani na Serikali ya Spain.

Ktk matukio mengi unayo yaona yantokea ni kwamba habari ya tukio husika uwa infahamika bali kuna uzembe utokea. Vyanzo vya Ulinzi vya Spain vilipata hii habari toka kwa mataifa ya Morocco na Egypt lakini kuto-act haraka na mapema ndio inatokea hao magaidi kulipua. Lakini SIO kwamba wamechukua nchi bali ni kuua watu wasiokuwa na hatia.

Narudia tena, Mungu aweze kuwaweka mahali pema peponi amina wale wote walio kumbwa na mikasa hii ktk hii dunia.

Kuhusu the Provos au jina lingine PIRA (The Provisional Irish Republican Army) wengi wanajua kama IRA ni kundi lililo kuwa linataka kuondoa utawala wa mwiingereza ndani ya Northern Ireland na ndani ya United Ireland.

Kutokana na mawazo yao walidhani ya kwamba watashinda malengo yao kwa kutumia Vita, Lakini July 2005 Dunia nzima imeshuhudia tukio la wao kuacha kutumia Vita (silaha za moto) kama suluhisho ya matakwa yao na kusalimisha silaha zao kwa Serikali ya Uingereza.

Hii ni moja ya Ushindi kwa Serikali ya Uingereza na kwa wale wote wapenda Amani duniani nikiwemo nafsi yangu.

Kuhusu kitengo cha makontena ktk Bandari ya nchi yetu kubinafsishwa usiwe na shaka maana sio kwamba tumewapa haki zote kwasababu kama Taifa tutabaki na asilimia za share ktk hiko kitengo au twaweza kutafuta watu watakao fanya kazi ktk kitengo hiko na kuwakilisha Taifa kwa kila details za kontena na mizigo yote inayo ingia ndani ya nchi na kutoka nje.

Pia kabla ya kubinafsishwa tutaweza kuangalia wale wote walio peleka maombi ya ku-take over na watachambuliwa kwa makini.Pia watu wataajiliwa iwe mfanyakazi wa kawaida au Ma-Boss wa juu watakao fanya kazi kama Spooks ili kupata habari na Taarifa zaidi za kila siku hapo bandarini.

Hii ni kitu cha kawaida kwani mbona USA hii imetokea P&0 imenunuliwa na United Arab Emirates (kampuni inaitwa Dubai Ports World), P&O ilikuwa shirika mali ya uingereza na ilikuwa na tender ya ports zote za USA (New York, Newark, Philadelphia, Baltimore, Miami na New Orleans) lakini United Arab Emirates imenunua P&O ( Peninsula and Oriental Steam Navigation Company) sasa kazi zote zitafanywa na Dubai Ports World.Ingawa hili bado linazungumziwa na Congress na Senate.

Ni lazima tuwe na wasiwasi na Congo, Uganda, na Burundi lakini:

Burundi - Vita siku hizi hakuna bali kuna vikundi vidogo vidogo.Kwa ujumla Vita imekwisha.Kwanza Burundi ni kama mikoa miwili ya Tanzania hivyo technically hawawezi kupigana na sisi na kingine kupindua nchi au nchi kuwa na machafuko na kuwa na dalili za Amani kupotea inabidi kuwe na Silaha nyingi za kuleta mapinduzi hivyo ni vigumu kwa kiwango hicho kuingia nchini kirahisi.

Congo - Machafuko yapo lakini majeshi toka UN yatapelekwa kuleta amani.

Uganda - Museveni Huyu bwana ni diktekta kwa kukaa madarakani miaka Ishirini (20)pia anasamehewa madeni na kupewa mikopo yeye anapeleka kununua ndege za kijeshi Israel.
Kuna machafuko ya LRA (Lord's Resistance Army)kundi linalo ongozwa na Joseph Kony ambaye anapata udhamini toka sehemu mbali mbali ndani ya Africa na nje.

Kwa ufupi mapinduzi hayawezi kufanyika Tanzania. Pia toka tukio la kulipuliwa DSM hali ya Ulinzi wa Taifa umeongezeka mara dufu.

Naona niishie hapa maana nimeandika mengi sana.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.


F MtiMkubwa Tungaraza
Mk,

Asante kwa ujumbe wako.

Awali kabla sijaendelea sana naomba unielewe kwamba nilichozungumzia siyo mapinduzi au machafuko nchini Tanzania. Nilichozungumzia ni tahadhari juu ya kutengeneza watu watakaoweza kuwa waasi kwa sababu za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

Kwa kifupi tu mimi ninafanyakazi na watu waliotoka nchi zilizoathirika na vita. Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana sababu zilizosababisha vita nchini kwao na nani wanaoshiriki katika kupigana vita. Kwa ufupi huwa wananiambia vita vyote vinatokana na kupunjana kiuchumi, tofauti ya itikadi za kisiasa. Pia kwa sababu za kijamii kama ukabila, dini, na rangi. Halafu kuhus kina nani wanaoshiriki kupigana vita huwa wananiambia ni wavulana na wanaume vijana wasio na kazi na wenye elimu ya chini na wanaume wenye umri wa makamo kati ya miaka 35 na 45!

Jingine, ulipozungumzia Chechnya kuna suala zaidi ya kuipunguza Urusi nguvu. Chechnya ina mafuta. Jinginewe zaidi Mchechnya na Mrusi ni watu tofauti wenye dini, lugha, na tofauti zingine za kiutamaduni. Wahusika wakuu wa vita hivi ni Wachechnya wenyewe wakisaidiana zaidi na Waislamu toka nchi za Kiarabu.

Halafu kuhusu Museveni na ndege za kijeshi sina hakika nalo. Lakini sidhani kama katika maadili ya kivita kama anaruhusiwa kutumiwa ndege kupigana LRA.

Halafu suala la Dubai Ports World limesitishwa. Kwa hiyo bado hawajaanza utendaji. Nakuomba fuatilia tena au kama mimi ndiyo sina habari kamili naomba unijulishe.

Halafu unaposema Burundi vita imekwisha na kwamba kuna vikundi vidogo vidogo tu hiyo ina maana vita bado ipo. Sijui fasili nzuri ya vita kwa Kiswahili lakini kwa Kiingereza naweza kusema War is a fight for the gain based on right or wrong reason/s. Mwanamuziki Gill Scott-Heron katika wimbo wake Work for Peace anasema "..Peace is not absence of war. Peace is even the absence of rumours of war.." Kwa hiyo pasipo amani pana vita.

Nisikuchoshe sana bali nakuomba usome tena waaraka wangu. Niliposema Burundi, Uganda na Kongo wanaweza kuwa vichochoro vizuri sana kwa wenye nia ya kuleta mabaya nchini mwetu. Sikusema Burundi inaweza kupigana na Tanzania. Jinginewe tusijisahau sana tukafikiri sisi wakubwa sana. Mtanzania aliyempiga Idd Amin siyo Mtanzania wa leo. Mtanzania yule alikuwa na dhana ya Utanzania chini ya itikadi ya Ujamaa ambayo ilikuwa inamgusa kila sehemu ya maisha yake ya kila siku kuanzia gazeti la UHURU/MZALENDO na DAILY NEWS/SUNDAY NEWS, Idhaa ya Taifa, Biashara na External Service za Radio Tanzania Dar es Salaam. Usafiri wa KAMATA na yale ya mikoa CORETCO, MORETCO na mengineyo, UDA, Reli ya Kati na TAZARA. Wakati ule palikuwa na umoja wa Kitaifa miongoni mwa Watanzania sasa hivi umoja huo umelegea sana kwa sababu ya kutokuwa na itikadi wala sera za kitaifa ya kitaifa. Kuwajibika, Ukweli na Uwazi, Ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya siyo sera wala itikadi hizi ni kauli mbiu ambazo hazijengi uzalendo wala utaifa.

Mungu Ibariki Tanzania.


MK said...
Ni Vizuri ndugu F MtiMkubwa Tungaraza kusema ya kwamba inabidi tuwe na tahadhari ktk kutengeneza watu watakaoweza kuwa waasi kwa sababu za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

Ni kweli machafuko mengi yanatokana na sababu za kiuchumi, tofauti za kisiasa, dini, ukabila, rangi, kijamii n.k. lakini ni kwamba ktk baadhi ya hayo mambo tumejaribu kuyaondoa na kuyavunja ndani ya Tanzania, Kitu kilicho baki ni hiki kitu cha Zanzibar na jinsi baadhi ya vyama vinavyo tekeleza siasa zao nchini Tanzania.

Baadhi ya hivyo vyama vimeshaambiwa fika kuweza kuacha hizo siasa za machafuko (kuwa na mawazo ya vurugu).
Kuhusu Ukabila Baba wa Taifa JK Nyerere aliweza kuliondoa na kuweza kufanya kila mtanzania kujiona ni sawa na kuwezesha kiswahili kuwa lugha ya Taifa ktk ardhi ya Tanzania.

Kuhusu swala la Zanzibar Hon. JK ameweza kupewa ushauri wa juu na ndio maana umeona ya kwamba imeanzishwa wizara ya Union Affairs: Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi under Vice-President's Office itakayo weza kuliangalia hili Tatizo na kulimaliza mapema iwezekanavyo.

Kuhusu idadi kubwa ya Vijana wasikuwa na kazi hili ni kweli na kila mara uwa nalizungumzia nikiwa baadhi ya watu fulani, Lakini hii serikali ya awamu ya nne imeonyesha ya kwamba wanafuatilia hili swala na wanataka kutengeneza nafasi nyingi za kazi na ndio maana juzi juzi umesikia nafasi nyingi za kazi zimetangazwa ktk jeshi na Polisi pia nafasi nyingi zitatangazwa hapo baadae ktk sekta na mashirika ya umma.

Kuhusu swala la Museveni kununua ndege za kivita ni swala ambalo nina uhakika nalo. Hii Vita ni ndefu sana (Miaka 18)ambapo Joseph Kony anapata msaada toka Sudan, Pia vile vile nao Uganda wanawapa SPLA(Sudan People's Liberation Army)msaada kupigana na Serikali ya Sudan, Vile vile Joseph Kony anapata msaada toka DRC (The Democratic Republic of the Congo) ambapo Juzi juzi Museveni baada ya kushinda Uraisi ametangaza ya kwamba ataivamia tena DRC kwa kisingizio cha kuwafuata LRA na kupigana nao huko huko DRC. Pia LRA wanapata misaada toka mataifa mbali mbali ndani ya Africa na nje ya Africa.

Kwa habari za mwaka November 2002 nilizo nazo hii Vita imegharimu Serikali ya Uganda (UPDF) yafuatayo:
1: Matumizi ya jumla ya 367 million USA dollars kwa matumizi ya Kijeshi.

2: Uchumi kukosa pato la Taifa kutokana na Kilimo ambapo wamepata hasara ya 212 million USA dollars.

3: Kupungua kwa utalii na kukosesha hilo Taifa kiasi cha 185 million USA dollars.

4: Kuongezeka kwa gharama za uduma za matibabu kwa jumla ya 138 million USA dollars.

5: Raia wapatao 23, 520 wanakadiliwa kufa kutokana na Vita.
Na watu zaidi ya Million Moja kukosa makazi au kuama makazi yao ktk maeneo ya
Vita.
Maelfu ya kabila la Acholi kuweza kupata vilema vya maisha kutokana na hii Vita.

6: kutokana na hii report ya mwaka 2002 inasemekana, Kuendelea na hii Vita Uganda
itagharimiwa asilimia 10 ya GDP ya nchi yao. Pia October mwaka huo Serikali ya
Uganda ilikata asilimia 25 ya matumizi ya wizara zake zingine na kupeleka nguvu
ktk kudhamini hii vita.

Kuhusu Dubai Ports World hili swala lina utata ndio maana nilisema hapo juu bado linazungumziwa na Congress na Senate ambapo kiongozi wa juu wa white house amesema ya kwamba kunyimwa haki kwa Dubai Ports World kutapeleka "I think it sends a terrible signal to friends around the world, that it's OK for a company from one country to manage the port, but not a country that plays by the rules and has a good track record from another part of the world can't manage the port," Bush said. Akimaanisha ya kwamba kunyimwa haki kwa Dubai Ports World ni kumaanisha ya kwamba ni sawa kwa UK (P&O kabla ya kuuzwa)kufanya kazi ndani ya USA lakini sio kwa United Arab Emirates (Dubai Ports World mmiliki mpya wa P&O) ambapo sio haki, hivyo ni picha mbaya kwa USA kwenda kwa mataifa mengine na kutafanya mataifa mengi ya Arabs kuogopa kuwekeza ndani ya USA.

Congress na Senate inakataa hili swala kutokana Dubai Ports World ni mali ya United Arab Emirates na vile vile wanakataa hili swala kutokana na baadhi ya wale watekaji wa 9/11 ktk zile ndege walitoka United Arab Emirates (wawili ktk United Airlines Flight 175 --> Marwan al-Shehhi, alikuwa ndio pilot na group leader Umri: 23 na Fayez Rashid Ahmed Hassan Al Qadi Banihammad Umri: 28.) Soma hapa kidogo.

Pia kutokana na report ya 9/11 Commission na ya Justice Department zimeonesha kwamba wengi wa magaidi ya 9/11 yalipata pesa na misaada mingi toka ndani ya United Arab Emirates, Sasa wanaona kama hawa watu wakipewa haya majukukumu si ndio magaidi wataingia ktk ardhi ya USA.

Lakini kutokana na Ushauri wa Serikali ya United Arab Emirates imeshauri Dubai Ports World kujiondoa ktk harakati zake hizo za kutaka kufanya kazi ktk ports za New York, Newark, Philadelphia, Baltimore, Miami na New Orleans na tarehe 09/03/2006 Dubai Ports World imetoa tamko rasmi haitaki tena kufuatilia hili swala ingawa hili swala lilikuwa bado linazunguziwa ktk Congress na Senate
Mwisho, Majeshi yetu (Vyanzo vyetu vya Ulinzi) vina uzoefu mwingi wa kuzima mapinduzi na uzoefu wa kulinda amani pia tuna macho ya kuona maadui (wowote wale ktk ndani na nje ya nchi wawe waasi, wenye mawazo ya kuasi au vingine hii kwa kushirikiana na mataifa mbali mbali duniani.) sasa mambo haya yakitokea nina uhakika yatazimwa chini ya masaa 24 au kuzimwa kabla ya kutokea. Ninachosema hapa mueshimiwa F MtiMkubwa Tungaraza ninakijua kwa undani na kwa makini.

Nashukuru sana F MtiMkubwa Tungaraza kuweza kubadilisha habari kati yangu na wewe.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.


F MtiMkubwa Tungaraza...
MK,

Ninafurahi kubadilishan mawazo nawe. Ninafurahi kuwa una imani kubwa sana juu ya vyanzo vyetu vya ulinzi. Hapa nina maswali kadhaa "..Hivi kama kweli vyanzo vyetu vya ulinzi ni kiboko namna hiyo silaha wanazotumia majambazi zinaingiaje nchini? Pili, vinashindwaje kudhibiti matukio ya ujambazi, uingizaji na upitishaji wa madawa ya kulevya kwa mfano makonteina ya mihadarati yaliyokamatwa Romania, na utoroshaji mali kwa mfano makonteina ya mchanga wa dhahabu bandari ya Tanga.."

Halafu ajira katika jeshi, polisi, mashirika na makampuni zinahitaji qualifications za kitaaluma na jeshini na polisi pia wajihi. Tukumbuke kwamba mwekezaji Tanzania hajafungua makampuni yanayohitaji harubu(manual labour)! Kwa hiyo vijana wasiyo na elimu hawahitajiki kwenye uzalishaji mali na utoaji huduma. Wengi wa wawekezaji wamewekeza kwenye rasilimali za asilia kama madini, mbuga za wanyama, na huduma za jamii kama mabenki, mahoteli, usafiri wa anga, na majini. Ardhini hakuna mwekezaji atayejipinda kuwekeza kwenye usafiri wa mabasi au kukarabati na kuboresha huduma reli ya kati, sana sana wanaitamani reli ya TAZARA ambayo kwa mikataba yake hatuwezi kuibinafsisha. Hapa naomba unipe taarifa za kweli(facts) mpango/mipango ya/wa serikali wa kuboresha na kukuza ajira kwa vijana. Wiki iliyopita nilijibu ujumbe kutoka kwa jamaa yangu mmoja aliyeniuliza kuhusu "..mafanikio ya mpango wa maji safi kwa wote ifikapo mwaka 2000.." Ninatumaini hili suala la ajira kwa vijana halitakuwa kama la mpango wa maji safi kwa wote ifikapo 2000.

Kuhusu hali ya usalama Zanzibar hilo ni jambo linlohitaji mikakati ya kweli. Kwa sababu makovu na vidonda vya vilivyosababishwa wakati wa utawala wa sultani, machafuko na mauaji wakati wa uchaguzi wa mwaka 1963/4, mapinduzi ya Januari 1964, machafuko ya 1972 na mauaji ya Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, machafuko na mauaji ya Januari 2000 makovu na madonda haya bado mabichi miongoni mwa Wazanzibari.

Mshairi maarufu wa Kiayalendi William Butler Yeats katika shairi lake la The Second Coming alisema

"...Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannont hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst are full of passionate intesity.."

MK, the Second Coming yaweza kuja popote ulimwenguni. Watanzania kama wanaulimwengu wengine wowote hatuna sababu ya kufikiri kwamba Second Coming kwetu haiwezi kuja. Kuna msemo jihadhari kabla ya hatari ambapo kinyume cha msemo huo ni kwamba mwenziyo akinyolewa wewe tia maji. Watanzania tuna nafasi kubwa ya kuchagua kati ya jihadhari kabla ya hatari au mwenziyo akinyolewa wewe tia maji.

Mkweli kwa nchi yangu,


MK said...
Ni kweli unayo sema muheshimiwa F MtiMkubwa Tungaraza, Silaha wanazotumia majambazi ktk nchi yetu ni baadhi ya Silaha chache zinazotoka nje ya nchi na hii inafahamika kwa baadhi ya wakubwa ndani ya jeshi na ndani ya Serikali yetu!! Kingine utakuta ata namba ya silaha iliyohusika ktk tukio la ujambazi inajulikana ni ya mmliki fulani au maganda ya silaha yanajulikana ni ya aina ya silaha fulani ambapo ndani ya nchi zinamilikiwa eidha na idadi fulani ya watu lakini kutokana na uozo ktk Jeshi fulani utakuta wanakaa kimya (kufumba macho).

Vyanzo vya ulinzi vya nchi hii ukiacha hilo jeshi wanafahamu hayo yote kuhusu silaha chache kutoka nje ya nchi ama baadhi ya watu kufumbiwa macho lakini mimi, wewe au mtu mwingine hauwezi kuingilia kati maana watakumaliza na kukuulia mbali na kuacha familia, ndugu, marafiki zako wakiteseka.

Hizo Silaha ni tishio kwa Raia na Taifa kwa ujumla lakini endapo idadi kubwa ya hizo Silaha (za kutishia mapinduzi) zingepitishwa ndani ya nchi basi hawa vigogo wala rushwa wangeingiliwa kati.
Mtu kuvamia Bank na kuondoka na Million 300 au zaidi sio kazi ya majambazi tu bali ni kazi ya kila Dirty cops na walinzi wa eneo husika au wafanyakazi wa eneo husika.

Hawa watu (Dirty cops) na hayo majambazi yanajulikana yalipo lakini kitu kinachoendelea ni kufichana. Unabidi uelewe ya kwamba kazi hii ya kulinda raia na mali zake ndani ya nchi ufanywa na jeshi lingine yaani kila kitengo kina kazi zake na mipaka yake sasa mfano kama afisa wa PCB au kitengo chochote (State Secret Service, military intelligence, Government Agencies n.k) akijua kwamba Kiongozi mmoja au Mkuu mmoja wa jeshi ni mla rushwa au anafanya Dirty games na aka-report kwa mkuu wake kisha akaambiwa kaa kimya na kupewa kitu kidogo (Pesa) unadhani utafanya nini? Naomba majibu!!

Lakini tumeona ya kwamba JMK ni mtu aliye serious na ndio maana unaona mabadiliko makubwa ndani ya hilo jeshi na ndani ya nchi kwa ujumla na wengine wakipoteza kazi zao au kuamishwa na ninakuadi ndugu F MtiMkubwa Tungaraza kuna mengi makubwa utayasikia labda wasiyaweke wazi kwa wananchi. Yaani watu wana ma-million mengi ya pesa ndani ya nchi na nje ya nchi na ata ukichukua mishahara yao na kuzidisha mara miaka mitano (5) hauwezi kufikia hiyo idadi ya pesa kweli inatisha!!

Mtandao huo wa ujambazi unao sema ni huo ambao unajulikana na kila mtu ktk vyanzo vya ulinzi lakini ni uzembe ktk hilo Jeshi, ndugu yangu wewe unadhani hawa watu hawajulikani? Wengine wanaishi kama Viongozi wa nchi na kulindwa!! Tumshukuru Hon. JMK na bwana Mwema watatuondolea uozo uliojaa ktk jeshi hilo.

Baada ya Serikali kuomba vyanzo vya ulinzi kutoa hiyo idadi ya majambazi na hao wasaidizi wao si umeona haijachukua muda kuweza kutolewa majina yao na wengine kukamatwa, kusimamishwa kazi, kubadilishwa sehemu za kazi, n.k

Muheshimiwa F MtiMkubwa Tungaraza nadhani wewe ni mtu mzima ambaye unaona mbali sana, Hii biashara ya madawa ya kulevya unadhani inafanywa na walala hoi? Hii inafanywa na The Big Bosses ambao wanatoa kickback nyingi na kubwa sana hili walindwe, lakini jalibu wewe na uone kana kwamba ujakamatwa siku hiyo hiyo.

Kuhusu mchanga wa dhahabu unashanga sasa hivi mbona hii ilikuwa siku nyingi enzi hizo ktk migodi yetu ya madini ndege zinabeba na kuondoka nayo, Hii inafahamika lakini ni tatizo za Administration kuweka sheria au kanuni zisizo eleweka. Unadhani mpaka sasa kiasi gani cha madini uondoka nchini na manufaa makubwa wanayapata wachache kuliko yule mlala hoi au mwananchi kwa ujumla aliye karibu na mgodi? Kuna kipindi nilipata habari kwamba bwana JMK na Serikali yake watapitia Contracts zote za haya makampuni na mengine ili kujua kama wananchi na Taifa linapata mazuri yoyote yale sasa sijajua kunaendeleaje!!

Kwa ujumla yote yanajulikana lakini huu ni ule uzembe wa baadhi ya Viongozi wa Africa.Na wakati huo huo ingawa kuna hawa Dirty Cops na Viongozi wazembe pia kuna idadi kubwa ya wana-usalama ndani na nje ya nchi walio wasafi na kufanya kazi kwa bidii ktk kila siku ya Mungu na kulinda Taifa na wananchi wa nchi hii 365/24/7.Pia naomba ipe muda hii serikali ya awamu ya nne na utaona ule uozo unao fanya wote tuonekane tumeoza ukiondolewa.

Kuhusu Investors ni swala zuri sana la kuangalia tukitaka kuweza kushindana na mataifa mengine ktk uchumi wa nchi. Hii inabidi kwa Serios Investors kukaribishwa toka kila pembe ya dunia na kuja kuwekeza nchini kwetu na pia inabidi tuwaangalia wale watakao kuwa wapo tayali kufanya biashara kwa muda mrefu na kila Contracts zitazo ingiwa inabidi ziwe na manufaa kwa taifa na wananchi.

Kingine sio tu kukaribisha wawekezaji bali tunabidi kutoa elimu mbali mbali kwa kila mwananchi maana hakuna mwekezaji atakaye kuja na kuwekeza alafu hakuna wafanyakazi!! Unadhani atakubali kuajiri mtu toka nje ya nchi? Kwanini afanye hivyo? Yeye anataka watu toka nchi husika ili aweze kupunguza costs!! Tatizo hapa hakuna msingi maradufu wa elimu wa kuwezesha watoto wetu kwenda kusoma na hii inachangiwa na umasikini na matatizo mengi sana, Leo hii kama mtoto hajafaulu na kwenda shule ya serikali basi kusoma kumekwisha maana mzazi atatoa wapi pesa (Malaki) kumpeleka mtoto kusoma? Sio ndio inabaki kuamua kumuozesha kama akiwa mwanamke? Kama mwanaume anabaki kuwa mkulima au kuoa!!

Kama Taifa hili linataka kuendelea ktk maisha ya sasa na ya baadae inabidi tuwekeze kwa watoto wetu, Matumizi ya Serikali kudhibitiwa, Tuache rushwa, wizi na ubinafsi kwa Viongozi na wananchi kuangalia familia zao tu na kujilimbikizia utajili mkubwa na kuiba mali za umma au mahali husika afanyapo kazi.Pia tuache uzembe na kufanya kazi kwa bidii.

Mataifa yaliyo endelea ni kutokana ni kwamba raia wote wamesoma na kuelimika na kila mtu ana professional yake.Na gharama za elimu kwa wazawa zinakuwa ni za bei ya chini na sio haya malaki ambapo ni wachache wanao soma hizo shule!! Baada ya kila mtu kuwa na professional yake wote ufanya kazi kwa bidii bila kuibia Taifa na wanakuwa kweli wasafi kila kona ktk kazi zao maana wao ufikiria je kizazi kijacho kitapata manufaa gani? Na ndio hapo wote ufanya kazi kwa manufaa ya Taifa na wananchi!!

Kingine kwa watanzania wengi walio nje ya nchi wakifika hapo walipo wanashindwa kujiendeleza ki-elimu ili kesho na kesho kutwa Taifa liwe na idadi kubwa ya wasomi, Nafahamu maisha ni magumu kwa watanzania walio wengi wa nje lakini ni lazima wakumbuke vitu viwili yaani Pesa na elimu!!

Sasa kama tukiwezesha Raia wetu kusoma na kupata ujuzi wawekezaji watakuja kuwekeza tu na pia Serikali iweke taratibu za kuitangaza Taifa letu kwa zaidi kama mataifa mengine ufanya.Tuchukue advantage kwa Taifa letu kuwa nchi ya Amani maana wawekezaji siku zote uenda mahali penye Amani sasa ni wakati kwa Serikali kuwakaribisha.

Kingine tunabidi tutafute suluhisho la umeme maana nina sikia ya kwamba nyumbani siku hizi hakuna umeme!! Sasa mwekezaji yoyote siku zote atakuja kama kuna bara bara nzuri, mawasiliano mazuri (simu na mawasiliano ya technogy zote, n.k) au kuna umeme wa kuwezesha kufanya production.

Kingine mimi ninashangaa utakuta hizi wizara zipo ktk safari za nje kila siku au Taifa letu lina barozi kila kona ya dunia lakini sijui zinafanya nini? Kwanini wasiweze kutumia mwanya wa hizo safari au huko mahali walipo kuitangaza Taifa na kutafuta wawekazaji walio serious na wa maana wenye capital kubwa ili waje kuwekeza? Kwasababu hakuna maana ya kufunga safari wizara karibia zote kwenda nje kama show ambapo wakirudi Taifa limepoteza mamillion ya Pesa na hakuna la maana linalopatikana na mwananchi wa chini anabaki kuumia na kodi au kulipa madeni ya Taifa!!

Yaani nina uchungu na hili Taifa na wananchi wake hii ni kwasababu ninajua kila kitu kinachofanywa.Nina uchungu kuona watu wanazidi kuteseka kila kukicha na maisha yao hayabadiliki na hii hali ulithiwa toka kwa Babu, Baba hadi watoto lakini wachache ndio wenye maisha ya kifahali.Kama kweli hii nguvu ya JMK itaendelea siku zote basi nadhani tutafanikiwa.Kwa hasira hii niliyo nayo yaani ninaweza kuandika mpaka ukurasa huu ujae lakini naomba niishie hapa kwa leo.

Mwisho, vyanzo vyetu vya ulinzi vina macho makubwa sana na hiyo mifano uliyo sema inajulikana lakini ni uzembe na matamanio ya baadhi Viongozi wa Askari wa juu kushirikiano na hao waharifu.Lakini endapo machafuko au mtu au Taifa lingine likiwa na mawazo ya kufanya mapinduzi au uasi nina uhakika yatazimwa chini ya masaa 24 na hii ndio udhibitisho. Naomba fanya uchunguzi maana siwezi kusema mengi ktk Internet na hapa nimejalibu kudodosa tu kwakuwa natumia MK aka The pretender.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.


11 March 2006

Aliyenacho ataongezewa...



Hii habari imeletwa na Mwanablogu MtiMkubwa. Naomba tuisome vizuri ili tujue kabisa ni wapi tunakoelekea, habari hii hapa chini...

Kuna msemo kwenye maandiko matakatifu ya Biblia unaosema walionacho wataongezewa na wale wenye kidogo watanyang'anywa. Msemo huu unadhihirika sana nchini Tanzania kwa jinsi waliokuwa navyo wanavyoongezewa au wanajiongezea. Siku za nyuma nilipata kutuma ujumbe kuulizia kwamba "..kati ya madaktari na wabunge nani anastahili kulipwa zaidi?.." Niliuliza swali hili baada ya kupata habari kwamba waheshimiwa wabunge walipokutana kwa mara ya kwanza moja ya mambo waliyoyasimamia kidete ni kutaka kujiongezea mishahara. Wabunge walipotaka kujiongezea mishahara wala hawakufukuzwa kazi kama walivyofanyiwa madaktari wa hospitali kuu ya Muhimbili. Suala lao limefunikwafunikwa na umma wa Watanzania haujui hatima ya azima hiyo ya waheshimiwa wabunge. Hii si mara ya kwanza waheshimiwa wabunge kujiongezea mishahara. Mwaka 1975 walipojiongezea mishahara umma haukuridhika. Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakaandamana kupinga azimio la waheshimiwa wa wabunge. Matokeo ya maandamano hayo si kwamba bunge au serikali ilibatilisha ongezeko la mishahara bali iliwafukuza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!

Kuna baadhi ya mambo yanayonikera sana nchini Tanzania. Mojawapo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ufujaji wa nguvu (abuse of power). Ufujaji wa nguvu unafanywa na wazazi majumbani, walimu mashuleni, viongozi makazini, viongozi wa kisiasa, na walinzi wa usalama wa raia. Polisi, FFU, magereza na wanamgambo ni wafujaji wakubwa sana wa nguvu. Mtanzania wa kawaida akimuona moja kati ya walinzi hawa wa usalama huwa anatishika badala ya kujisikia yupo salama. Walinzi hawa wa usalama wa raia wamejenga tabia ya uonevu na dhuluma zilizokithiri dhidi ya Watanzania masikini. Wiki hii tumeshuhudia walinzi hawa wa usalama walivyoshiriki kwenye zoezi la kuwadhibiti wapiga debe na wafanyabiashara ndogo ndogo kwa amri na ridhaa ya serikali. Matokeo ya zoezi hilo limeua raia wawili na kujeruhi raia na polisi ambao idadi yao hatujaijua.

Binafsi yangu nimeliongelea sana suala la ufujaji wa nguvu za vyombo vya dola dhidi ya wananchi na viongozi wa kisiasa, ndugu, jamaa, na marafiki zangu wengi sana. Nilipata kumueleza kiongozi mmoja wa kisiasa kwamba Tanzania akitokea psychopath kama Foday Sankoh wa Sierra Leone atapata wafuasi wengi sana na upesi sana. Kiongozi huyo wa kisiasa akastuka sana na kuniuliza "..atawapataje?.." Nikamwambia "..wale Wamachinga wanaoonewa, kunyanyaswa na kudhulumiwa na vyombo vya dola ni potential recruits wa rebels katika nchi yoyote.." Akaniuliza "..unafikiri Wamachinga wanaonewa kiasi hicho?.." Nikamjibu "..Si kwamba wanaonewa tu bali wanauawa na wanaichukia sana system!.." Akasema "..una ushahidi wowote?.." Nikamwambia "..Ushahidi wa kwanza mauaji ya Kilombero.." Akanijibu "..Hayo yalishughulikiwa.." Nikamwambia "..Nani alinyongwa kwa sababu ya mauaji ya Wasafwa Kilombero?.. Akanijibu "..Ukifuatilia wapo waliowajibika.." Nikamwambia "..Nina hakika hakuna kiongozi yoyote wa ngazi ya juu aliyefukuzwa kazi kwa sababu ya mauaji yale. Hata mauaji ya Shinyanga waliofukuzwa kazi na kuhukumiwa walikuwa ni watendaji wa chini wa juu walilhamishwa hamishwa na wengine wakarudi na kuwa Rais, Makamu wa Waziri Mkuu, na nafasi zingine za kisiasa!.." Akaniambia "..Hatuzungumzii mauaji ya Shinyanga..Nataka ushahidi kama kuna walinzi wa usalama waliowahi kuua Wamachinga.." Nikamwambia "..Tukifuatilia tutapata ushahidi.." Akaniambia "..Usiseme maneno kama haya yanaweza kukutia matatizoni.." Nikamwambia "..Nisiposema na kukuambia mtu kama wewe ili upelekee kwa wakubwa wenziyo, Mtakuja kustuka siku moja Wamachinga watakaposhika silaha dhidi ya vyombo vya usalama..Mtatahayari siku Watanzania wapole watakapokuwa washenzi kama Wasierra Leone au Waliberia!.." Yale niliyoyazungumza na huyo bwana wiki hii yamekuwa. Tafadhali usichoke kusoma habari kaamili hiyo hapo chini kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la Uingereza BBC:

Tanzania suspends street clean-up

Street vendors say moving away from the town centres hits business
A police crackdown on street vendors and bus ticket touts in Tanzania has been suspended for six months after violent clashes left two people dead.
Prime Minister Edward Lowassa said he was halting the operation to allow local authorities and vendors alike more time to prepare for the change.
Vendors and touts have been blamed for a rise in petty crime.
The two deaths occurred on Wednesday in the town of Mwanza along the shores of Lake Victoria in the north.
Four hours of rioting began after police and security guards confiscated vendors' wares and shops and offices in the town were shut down, according to Tanzanian newspaper Mwananchi.
"Many" people were also injured before anti-riot police quelled the violence with tear gas.
Kiosks were also demolished and vendors removed in the capital, Dar es Salaam.
'Adequate preparation'
Mr Lowassa, who originally envisaged completing the clean-up within three months, told the BBC's Swahili service that municipal officials were being given time to plan the clean-up "in a more respectful manner".
With the kiosk's income we could send the children to school and pay for the rent - now we are left with nothing

unnamed street vendor
Vendors facing eviction also needed time to "prepare themselves adequately", he added.
The prime minister said that those traders already moved on would be allowed to continue their business elsewhere because it was the government's policy to "ensure income for everyone".
But vendors complain their new trading spots are not in the town centres and therefore they are being denied their right to a living.
"With the kiosk's income we could send the children to school and pay for the rent," a woman in Dar es Salaam told the BBC as she piled up the remnants of her stand.
"Now we are left with nothing."
The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says the streets of the city looked bare on Friday after the demolitions.
Crimes are often committed in broad daylight in front of the street vendors who do not warn the victims or volunteer information to the police.
Many of the vendors say they were given licenses and paid taxes and they expect compensation from the government for destroying their property.

07 March 2006

Anaishi Royal Palm Hotel....


Hii habari amenisukumia Kaka yangu mkubwa 'MtiMkubwa' kwa vile ni nyeti sana nimeona nami niisukume kwa wananchi wazalendo wenzangu ili tuweze kuijadili kwa kina, haya tuendelee jamani...


Naam,

Tanzania ni nchi yenye miujiza anuai. Tuna miujiza ya kiasili kama vile Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Ziwa Tanganyika na mengineyo. Pia tumejaaliwa kuzua miujiza ambayo yaweza kumstaajabisha hata mtoto mchanga aliyezaliwa leo. Moja ya miujiza hiyo ni ule wa kuuza mali za umma zilizoimarishwa kwa mtaji wa umma wa Watanzania masikini. Mojawapo ya mali za umma zilizouzwa na serikali ya awamu ya tatu ni majumba ya serikali yakiwemo ya mawaziri.

Mengi ya majumba hayo yaliyouzwa ni sehemu kubwa ya historia ya nchi yetu. Kwani majumba hayo yalijengwa na wakoloni wa Kijerumani kabla ya kujiingiza "mdhamini" wa Kiingereza mwaka 1948. Kinachofuatia baada ya kuuzwa au kuuziana majumba hayo "maswahiba" wa serikali ya awamu ya tatu ni kwamba baaadhi ya mawaziri serikali ya nne wamepangiwa kuishi mahotelini makubwa kama wafanyabiashara au watalii. Humo mahotelini wanakula vipsi na kuku, wanaogelea kwenye maswimingi puli, wanaletewa rumu sevisi, na gharama zinginezo nyingi na kubwa!

Nimepungukiwa na ya kuandika lakini naomba usichoke kusoma maelezo zaidi hapo chini:


Uproar over Tanzania's hotel ministers
By Vicky Ntetema
BBC News, Dar es Salaam


Many Tanzanians are outraged by the revelation that dozens of ministers have been staying in luxury hotels since the beginning of the year at the taxpayers' expense.

The Courtyard is popular with tourists at more than $109 a night
All ministers are supposed to be given subsidised housing but the new ministerial homes have not been completed after the existing buildings were sold off to civil servants by the former government.
So some of those named since President Jakaya Kikwete took office last December have been staying in hotels, at a cost of hundreds of thousands of dollars a month.
This expense has been strongly criticised at a time when more than 3m people are on the verge of starvation due to prolonged droughts.
The newcomers into cabinet were given until the end of February to vacate their hotel rooms or pay the bills from their own pockets.
Yet the government has admitted that 36 ministers and their deputies, who come from outside Tanzania's commercial capital, Dar es Salaam, have not yet been re-housed.
Walking distance
Although the government does not want to reveal the exact names of these temporary dwellings, it is an open secret that some of them stay in expensive hotels which cater for top class tourists and international executive high fliers.

It's like home - we serve international cuisine and there is no doubt that security is very high

The Courtyard's Abysai Mashambo
One of these is The Courtyard in one of the upmarket areas of the commercial city of Dar es Salaam, within walking distance of most ministerial office buildings and State House.
Rates for rooms at this five-star hotel range from $109 to $189 per night.
The Courtyard's spokesperson Abysai Mashambo says ministers like this costly hotel for many reasons.
"It's a very quiet place - it's like a home; it's not very far from the city centre; we serve international cuisine - continental, Indian, African and there is no doubt that security is very high," he says.
"The ministers take rooms which suit the budget of the government - because the government pays for them. They don't pay from their pockets."
Not all ministers enjoy the comfort of such luxurious hotels.
At least two deputy ministers are accommodated at the three-star Landmark Hotel, about 7km (four miles) from Dar es Salaam city centre, in the overcrowded Ubungo area.
Most local residents whose houses are dwarfed by this five-storey hotel are either unemployed or have low-paid jobs.
Here the rooms cost about $40 to $60 per night.
Baffled
The scheme to build government quarters started last year under the leadership of retired President Benjamin Mkapa, after most official homes were sold off to civil servants, including ministers, at what were seen as give-away prices.

These houses for ministers and deputy ministers will not be sold

Minister Juma Akukweti
The policy was unpopular and authorities blamed for what many saw as a misuse of public funds.
Many were then baffled by the government's decision to spend taxpayers' money on hotel bills for new appointees, leaving retired civil servants in the affordable state accommodation.
The ministry of infrastructure development last month reassured Tanzanians that ministers would move into their new homes by the end of February.
John Kijazi, the ministry's most senior civil servant, says that the delay has been caused by the construction hitches encountered at the start of building.
He said he could not put a figure on how much the taxpayers will have to cough up to foot the hotel bills until every single minister had moved into their new homes.
Rubble
Builders at the Msasani Peninsula on the outskirts of Dar es Salaam are working tirelessly to complete the finishing touches on some bungalows - the official residences for cabinet members.

The houses will have servants' quarters and large gardens
But one minister and his wife could not wait any longer and have moved in amid the rubble.
I found Minister of state in the prime minister's office in charge of Coordination and Parliamentary Affairs Juma Akukweti and his wife inspecting their three-bedroom house close to the Indian Ocean beach.
"I am quite comfortable. I like the house - the rooms are quite spacious. I have a big family, as an African that's usual. This is enough for my family," he said.
He promised that these newly constructed houses with servant's quarters and spacious back and front yards - some as big as a football pitch - would not be sold off to ministers in 10 year's time.
"These houses for ministers and deputy ministers will not be sold. If one wants to buy a house - ask from a bank. But these ones are not for sale. And that's okay."
With this assurance, I left the happy minister and his family to settle into his new house.




24 February 2006

Winnie Madikizela Mandela.


Duniani kuna watu machachari, tena kuna watu majasiri na wenye misimamo wanaoweza kudhamiria jambo na kujitoa muhanga kwa lolote hadi jambo lake lifanikiwe.

Winnie Mandela ni miongoni mwa watu wa aina hiyo. Mama huyu ambaye nchini kwake amepewa jina la 'Mama wa Taifa' anajulikana duniani kote kwa jinsi alivyoweza kupigania uhuru wa nchi yake hadi kupatikana hata baada ya mumewe Rolihlahla Nelson Mandela kutiwa garezani kwa miaka 27.

Winnie alizaliwa tarehe 26/09/1936, katika kijiji cha Bizana mkoani Transkei Afrika kusini akiwa ni mtoto wa 4 kati ya 8 wa bwana Columbus Mazingi Madikizela na bibi Gertrude Nomathamsanqa Mzaidume.

Baba yake alikuwa ni mwalimu na baadaye waziri wa kilimo na misitu katika serikali ya Transkei wakati huo ikiongozwa na Kaizer Matanzima. Mama yake alikuwa alikuwa ni mwalimu wa sayansi kimu. Familia yao ilikuwa ni yenye furaha hadi Winnie alipofikisha umri wa miaka saba ambapo mmoja wa dada zake alifariki. Msiba huu ulimsononesha na kumfadhaisha sana mama yake kiasi kwamba mwaka uliofuatia naye alifariki dunia. Akiwa na miaka minane na huzuni ya kuondokewa na mama yake, Winnie alikata shauri kwamba yeye ni lazima atakakuwa mwanamke jasiri.

Maisha mapya yalianza kwa Winnie, na sasa alikuwa karibu zaidi na baba yake. Baba yake alitumia muda mwingi kumfundisha historia ya Afrika kusini na utawala wa kibaguzi uliopo, anasema kila wakati alipokuwa akijisomea vitabu baba yake alikuwa akimuainishia habari za kweli na zisizo za kweli ambazo makaburu walikuwa wakiziandika katika vitabu hivyo. Hivyo basi Winnie katika umri wake mdogo alianza kuelewa kwamba nchi yao ina tatizo ingawa hakujua vizuri ni kwa kiwango gani.

Baada ya muda mfupi alianza shule ya msingi hapo hapo kijijini kwao Bizana na baadaye sekondari ya Shawbury. Akiwa sekondari mwaka 1952 alianza kusikia habari za Mandela na harakati zake, Winnie damu ya ukombozi ikaaanza kumuingia akashawishi wanafunzi wenzie kuanza kutumia kauli alizokuwa akizitumia bwana Mandela katika mikutano yake, inasemekana ilibaki kidogo shule ile ifungiwe.

Winnie alimaliza masomo yake ya sekondari na kubahatika kupata ufadhili wa kuendelea na masomo ya juu katika chuo cha Jan Hofmeyer Johannesburg, chuo hiki kilikuwa mahususi kwa masomo ya Ustawi wa jamii. Alimaliza mwaka 1955 na kupata diploma ya mediko sosho weka (Medical social worker). Baada ya hapo alijiunga na chuo kikuu cha Witwatersrand hapo hapo Johannesburg safari hii akisomea Siasa na uhusiano wa kimataifa.

Alipohitimu chuo kikuu alibahatika kupata kazi katika hospitali ya Baragwanath kama mwana ustawi jamii (social worker). Winnie alikuwa ni mwafrika wa kwanza kwa wanaume na wanawake kufanya kazi ya ustawi wa jamii hospitalini hapo. Na ni kutokana na kufanya kazi hospitalini hapo ndipo alipoamua kwamba atakuwa mwanasiasa. Anasema kulikuwa na tofauti kubwa sana katika utolewaji wa huduma kwa wagonjwa wazungu na wagonjwa waafrika, wagonjwa waafrika hawakupewa kipaumbele hata kidogo jambo hili lilimkera sana Winnie. Akiwa bado mfanyakazi wa hapo hospitalini, alipata zoezi la kufanya utafiti kujua takwimu ya vifo vinavyotokea wakati kina mama wanapojifungua. Matokeo yalikuwa kwamba katika kila wazazi waafrika 1000, kuna vifo 10, na hakuna vifo kwa wazazi weupe na kama vipo basi havikutokana na huduma mbaya na duni aliyopata wakati wakijifungua. Vifo hivi kumi kwa waafrika vilitokana na huduma mbaya walizokuwa wakipatiwa waafrika.

Kwa mara ya kwanza mwaka 1957 Winnie alibahatika kukutana na Nelson Mandela, haijulikani ni wapi hasa walikumbana lakini kwa mujibu wa mwandishi mkongwe na rafiki wa siku nyingi wa familia ya Mandela Profesa Fatma Meer, anasema siku moja alipata simu kutoka kwa Mandela akiwaagiza kwenda stesheni kumchukua mgeni, walipofika walimkuta binti mrembo sana akiwasubiri, wakidhani ni ndugu au jamaa tu wa kawaida wa Mandela walimchukuwa na kumpeleka nyumbani ambako alikaa kwa wiki 2 hivi, hawakujua lolote hadi siku moja Fatma alipomkuta Winnie akitoa na kuangalia picha za Mandela katika mkoba wake ndipo akahisi kwamba kuna jambo linaloendelea kati ya wawili hao.

Mwaka uliofuatia 1958 Winnie alifunga ndoa na Mandela kinyume na matakwa ya Mzee Madikizela. Pingamizi la baba Winnie lilikuwa katika mambo mawili:-

1. Umri- Mandela (40) na Winnie (22) wapi na wapi?

2. Siasa- mandela alikuwa amejikita sana katika siasa, hoja ya Mzee Madikizela
inakuja..saa ngapi ataiangalia familia yake?...hali hii ya kuegemea sana katika
siasa ndiyo iliyofanya ndoa yake ya kwanza na Evelyne Mase Mandela kuvunjika,
kwa hiyo alikuwa na wasiwasi kwamba mwanaye anajiingiza katika matatizo.

Kama nilivyosema hapo awali kwamba Winnie ni kati ya watu wanaoweza kushikilia misimamo yao, basi hata hili la ndoa na Mandela hakuruhusu mtu aligeuze, alikubaliana kabisa na hoja za baba yake na hata alipoolewa alijua kabisa anaolewa na mtu wa aina gani. Muda mfupi baada ya kuoana Winnie alijiunga rasmi na chama cha African National Congress (ANC), na bila kuchelewa akaanza kupiga kampeni ya kuipinga serikali ya kikaburu, mwaka huohuo alikamatwa na kuwekwa jela kwa siku 14 akiwa mjamzito, hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutumikia kifungo.

Mwaka 1959 walibahatika kupata mtoto wa kwanza wa kike waliyemwita Zenani, na mwaka uliofuatia 1960 walipata mtoto wa pili pia wa kike waliyemwita Zindzi. Mwaka huo huo 1960, chama chao cha ANC kilifutiwa kibali chake na kupigwa marufuku kufanya shughuli zozote za kisiasa. Waliendelea kukiendesha kwa siri na kama haitoshi Mandela akaamua kufunga safari kwenda katika nchi mbalimbali za kiafrika kuwaomba waungane naye katika mapambano ya kutokomeza serikali ya kibaguzi ya Afrika kusini. Bahati mbaya serikali tawala ililigundua hilo na Mandela aliporudi alishtakiwa na kutiwa ndani hiyo ilikuwa mwaka 1962, Mandela akiwa jela huku nyuma Winnie akapatikana na tuhuma za kuendelea kukiendesha chama cha ANC kinyume cha sheria, adhabu yake ilikuwa ni kuwekwa kizuizini katika mji wa Soweto. Mwaka 1964 mandela akapatika na hatia ya kutaka kuipindua serikali ya kikaburu na akahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Makaburu wakidhani kwa hukumu hiyo watakuwa wamezimisha harakati za ukombozi za chama cha ANC, lakini kwa Winnie ndiyo kwanza mapambano yalikuwa yanaanza, cha kwanza alichokifanya ni kuwahamishia watoto wake nchini Swaziland kwa mmoja wa dada zake ili kuepuka usumbufu. Mwaka 1967 akiwa bado kizuizini aliamua kwenda kumtembelea Mandela gerezani Robben Island aliporudi akashtakiwa na kufungwa kwa mwaka mmoja. Alipomaliza muda wake wa gerezani alitoka na kuendelea kukaa kizuizini huku akiwa amezuiliwa kujihusisha na shughuli zozote za siasa.

Sifa au tuseme tabia moja kubwa aliyonayo Winnie ni ukaidi na kutokuogopa lolote, ingawa mwaka mzima wa 1968 aliumalizia gerezani, lakini alipotoka aliendelea na shughuli za ANC na hata kutembelea maeneo aliyokatazwa kufika. Kutokana na hili mwaka 1970 alikamatwa na kutiwa gerezani kwa miezi 9, alipomaliza alitoka lakini akiwa ameongezewa miaka 5 zaidi ya kukaa kizuizini. Mwaka 1974 muda mfupi kabla ya kifungo chake cha nje kuisha alikaidi tena na kuamua kukutana na mwanaharakati mwingine ambaye pia alikuwa kizuizini, kwa hili akahukumiwa tena kwenda gerezani.

Hatimaye baada ya miaka 13 ya kuwekwa kizuizini na gerezani Winnie aliachiwa huru,
lakini mwaka 1976 baada ya machafuko ya Soweto Winnie alifungwa tena kwa miezi 3 na alipotolewa aliwekwa tena kizuizini kwa miaka 8 safari hii akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Miaka ya themanini ilianza, kwa Winnie hii ni miaka ambayo hawezi kuisahau kwa ulahisi kwani ilikuwa ni miaka ya mvurugiko wa maisha yake binafsi, mwaka 1982 mumewe alihamishwa gereza kutoka Robben island kwenda Pollsmoor karibu na Cape Town, mwaka 1985 nyumba yake ya Brandfort ililipuliwa kwa bomu na hivyo kumfanya kuhamia Soweto ili kuepuka vitendo vya kiugaidi. Kwa kipindi chote hiki Winnie alikuwa akiheshimika sana duniani kote kama mwanamke shujaa na jasiri.

Mtizamo huu wa watu juu yake ulianza kubadilika mwishoni mwa miaka ya themanini, ambapo aliamua kuunda timu ya mpira wa miguu ya Mandela (Mandela United Football Team) wachezaji wote wa timu hii walikuwa ni walinzi wake (bodyguards), kwa bahati mbaya timu hii kiutawala ilisahau wajibu wake na kuegemea upande mmoja wa kumlinda na kumzibaziba Winnie katika mambo ya chini chini aliyokuwa akiyafanya. Muda mrefu haukupita habari zikaanza kuvuma kwamba timu inajihusisha na ubadhilifu wa mali ya umma. Timu nayo ikashtuka na kujizatiti zaidi kwa kufukuza na hata kuua mtu yeyote aliyetaka kwenda kinyume nao. Inasemekana vijana wengi walifukuzwa na kuuawa kwa kuchinjwa kama mbuzi au kwa mtindo wa Necklacing, Soma hapa juu ya Necklace, lakini baya zaidi na pengine linalomsumbua Winnie hadi sasa hivi ni lile la kumuua kijana mdogo wa miaka 14 Stompie Seipei mwaka 1989 kwani hili halikuweza kufichika. Stompie Seipei alikuwa ni mmoja wa vijana katika timu ya Mandela, na kutokana na sababu zisizojulikana ilivuma habari kwamba Stompie alijiunga na timu akiwa ni mpelelezi kutoka polisi. Stompie na vijana wengine watatu walikamatwa walipokuwa kanisani na kupelekwa katika nyumba ya Winnie, huko waliteswa sana na baadaye kuchinjwa kama mbuzi. Shughuli ya uchinjaji ilikuwa ikifanywa na kocha wa timu wakati huo bwana Jerry Richardson ambaye sasa hivi anatumikia kifungo cha maisha. Kwa habari zaidi ya jinsi mauaji na mateso yalivyokuwa yakitendeka soma hapa na hapa ambapo bwana Richardson alieleza ukweli wote. Na kwa tukio hili Tume ya usuluhishi (Truth and Reconciliation commission) iliingilia kati na kuanza kuichunguza timu ile kwa undani zaidi, tume iligundua mauaji mengi yaliyofanyika katika timu hiyo, bonyeza hapa ujionee mwenyewe.

Mwaka 1990 Nelson Mandela aliachiwa huru, mke na mume waliungana bila matatizo hata baada ya Mandela kusikia tuhuma zote za mauaji ya timu ya mpira ya Mandela. Alimuamini mkewe na kumtetea kwa nguvu zake zote. Tatizo lilikuja baada ya Mandela kupata habari kwamba mkewe alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Kijana Dali Mpofu ambaye alikuwa ni mwanasheria binafsi wa Winnie, hapa mzee Madiba alishindwa kumtetea na hata kumsamehe, Mandela na Winnie wakaachana kwa usalama kabisa mwaka 1996 baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka 38, kwa habari zaidi ya kuachana kwa Winnie na Mandela soma hapa.

Hilo la ndoa likawa limekwisha, lakini kesi yake ya mauaji iliendelea na ushahidi wote ulionyesha kwamba Winnie ana hatia ya mauaji lakini bado Winnie hakukubali kukiri. Ni askofu Desmond Tutu ndiye aliyefanikiwa kumshawishi akubali makosa yake na kuyakiri hadharani ili kurudisha heshima yake 'alimwambia watu hufanya makosa..na unapokubali na kukiri kosa mara nyingi heshima yako huongezeka'. Winnie kwa kuzingatia hili aliomba msamaha na hata kukumbatiana na mama mzazi wa Stompie Seipei 'Mrs Joyce Seipei. Hebu soma hapa uone jitihada za askofu Desmond Tutu zilivyokuwa.

Tangu kipindi hicho hadi sasa siri nyingi za Winnie zimekuwa zikiendelea kutoka ikiwa ni pamoja na ya wizi wa fedha benki kwa kutumia za kugushi makaratasi yasiyo halali. Soma hapa ulipate na hilo. Lakini pamoja na hayo yote bado Winnie alikumbukwa katika serikali ya Mandela kwa kupewa nafasi ya uwaziri wa utamaduni, ubunge na hata Urais wa African National Congress Women League (ANCWL). Mwaka 2003 Winnie alijiuzuru nyadhifa zake ANC na kuanza kutumikia kifungo cha miaka 5 kwa makosa aliyoyafanya. Soma hapa kwa habari zaidi.

Ndugu wasomaji, labda kwa ufupi ningesema kwamba Winnie Nomzamo Nkosikazi Madikizela Mandela, hajawahi kuishi maisha ya kawaida ambayo mimi na wewe tumeweza kuishi, na kwa kumwangalia tangu alivyoanza mapambano mpaka anavyomaliza mapambano nimeshindwa kabisa nimuweke katika fungu gani maana mazuri kayafanya na mabaya kayafanya. Jamani hebu na nyiye nisaidieni huyu mama.

19 February 2006

Michuzi...Da Mija huyooo!


Kaka Michuzi, hapo katika picha nashangaa kusoma ujumbe wako kwamba wewe ni Meneja wa kikundi cha muziki wa asili cha Sisi Tambala, lakini mshangao wangu ulipunguka kidogo baada ya kukumbuka habari hii. Nilijiunga na kikundi hicho wakati kikianzishwa mwaka 1998, nikiwa mwanamke wa kwanza na pekee kundini, Enzi hizo tulikuwa watano tu lakini machachari sana ...wengine walikuwa ni Nanjuja Kibiriti, Salumu, Fadhili Mkenda na Kasembe Ungani. Duh! Michuzi umenikumbusha mbali.

Hapo kipindi cha nyuma nilishawahi kupandisha picha yangu, lakini naona imeshapotelea chini kutokana na kupandisha habari zingine, hapa ndipo umuhimu wa Wordpress unapokuja, Leo Michuzi usingepata taabu kuniomba picha, ungekong'oli tu kwenye maudhui ya picha ya Da Mija na kunikuta.

13 February 2006

Changamoto....Ni nani zaidi?.. Winnie au Graca?




Haya jamani, hivi karibuni nitawaleteeni harakati za maisha ya wanawake wa shoka Graca Machel na Winnie Mandela. Wanawake hawa wawili wana mambo mengi yanayoshabihiana katika harakati zao za maisha. Haya, kabla sijawaleteeni undani wao ninawapa changamoto hii ya kujaribu kumtafuta aliye zaidi ya mwenziye. Haya karibuni nami najiweka sawa.