05 December 2011

Ninamlaumu Mzazi!!!

Wadau eti ni kwa kiwango gani mzazi anawajibika katika maisha ya mtoto?

Jumatatu njema na abarikiwe kila atakayepitia hapa.

7 comments:

emu-three said...

Mzazi anawajibika kila hatua ya mtoto, hadi hapo atakapojitegemea, na kuwa mzazi. Baada ya hapo yeye atawajibika tu kama mshauri, ...

Swahili na Waswahili said...

Dadake kwangu mimi naona kama anawajibika wakati wote wa maisha yake,bali tuu baadhi ya majukumu yanakikomo/kupungua pale mtoto anapoanza kujitegemea.Baraka kwa wote!

Goodman Manyanya Phiri said...

"Namlaumu mzazi wangu" ni neno la mjinga kwani kama amekuwezesha kuelewa maana ya "lawama" mzazi wako amekupa yote basi....

KWANINI WEWE USIREKEBISHE BASI PALE UNAPOMUONEA MZAZI WAKO LAWAMA? Au unafikiri mwenye kushughulika na dunia ni mzazi wako tu nawe ukae kazi yako kusubiri sahani ya ugali hadi ukubwani?

WISDOM said...

Kwa mawazo yangu, mzazi hujitahidi sana kumlea mtoto wake vema, kwa nyanja zote. Baadhi ya watoto hufuata walofundishwa, wakati wengine huyapuuza pindi wanapojitegemea. Jibu la suala hili, nadhani halihitaji mtu kuwa na digrii ya chuo kikuu kulijua. Mungu awape hekima nyingi kila mara na muitumie vema daima.

Mija Shija Sayi said...

Asanteni wazazi wooote hapo juu, lakini labda tujiulize je wazazi wote hulea watoto wao ipasavyo? Vipi wale wanaoingia na kutoka nyumbani, vipi wanaoachia wafanyakazi wa ndani kazi yote ya ulezi? Vipi wale wanaowapenda sana watoto wao na kuwapa uhuru wa kila kitu bila mipaka?

Yasinta Ngonyani said...

Wazazi! mzazi/mlezi hauishi hata ukiwa kumama/kubaba bado mzazi wako atakuwa mzazi tu.
Ndiyo wapo wale wanaowaachia wasaidizi wa ndani wafanye kazi hiyo na hilo ni tatizo kubwa sana na ndiyo hapo watoto wanapokuwa na malezi tofauti. Mija na wengine wote kwa kweli hili swali naona kama linanishinda na naona niachia hapa. Wote mliopita hapa na mtakaopita hapa mbarikiwe sana.

SIMON KITURURU said...

Si watoto hawakuomba wazazi wawazae na ni mivitu tu ya wazazi kimahitajiyao ya kikubwa kuonekana wazazi, KUHESHIMIKA kama WAZAZI katika JAMII, woga wa kuzeeka bila msaada,....... au tu hata kukiri kwa kuzaa kuwa hawakujizuia tu mihamu yao ya kiutu uzima labda ndio tatizo na kwa hiyo labda ni haki ya mtoto kulaumu WAZAZI?

Na si wazazi wasinge mzaa mtoto atakayefanya dhambi , LABDA mtoto huyo asingekuwepo kwaaajili ya kuchomwa jehanamu kisa kazaliwa kisa hamu za wazazi na kufikia kuchomwa na akasirikaye MUNGU WA AMANI ambaye ana kitu JEHANAMU?

Naendelea kuwaza!:-(